MSAJILI LIUNDI, SAGAFU WAFARIKI DUNIA
Posted in
No comments
Tuesday, January 14, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
ALIYEWAHI kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji mstaafu George Liundi
(80), amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria na
maumivu ya uti wa mgongo.
Mtoto wa marehemu George Liundi, Taji Liundi alisema baba yake alifariki Jumapili saa 7 mchana.
Alisema baba yake, alifariki dunia wakati wakijiandaa kumpeleka hospitali baada ya kuzidiwa na maumivu.
“Alikuwa anaumwa malaria na alishaanza kutibiwa, hali yake ilianza kuimarika vizuri, lakini alikuwa analalamika maumivu makali ya mgongo ambayo yalisababisha presha kuwa juu,” alisema Taji.
Alisema siku ya Ijumaa na Jumamosi ambazo alikuwa anakunywa dawa za malaria, hali yake haikuwa mbaya kwani alikuwa anakula vizuri.
Alisema maumivu yalizidi, baada ya kugeuka ubavu kitendo ambacho kilisababisha misuli yake kupoteza uwezo.
“Wakati tunamtoa kumpeleka hospitali tukisaidiana na wenzangu, akakata kauli hapo hapo na mpaka tunamuingiza kwenye gari alikuwa ameshapoteza maisha, ila tulienda kupata uhakika zaidi hospitali, tulipofika pale Hospitali ya TMJ wakatuambia tayari amefariki,” alisema Taji.
Alisema familia kwa sasa inafanya mawasiliano na viongozi mbalimbali wa Serikali ili kuweza kushirikiana nao. Akitoa ratiba ya mazishi ambayo yatafanyika siku ya Alhamisi, Taji alisema mwili utatoka Hospitali ya Taifa Muhimbili asubuhi na kupelekwa nyumbani kwa marehemu Keko kwa ajili ya kuagwa na ndugu na marafiki wa karibu.
Alisema shughuli za kuaga zitaanza saa 6:00 mchana, ambapo baada ya hapo mwili utapelekwa Kanisa Katoliki la Chang’ombe kwa ajili ya misa na baadaye kuzikwa katika makaburi ya Chang’ombe.
Marehemu ameacha mjane, Agness Doris Liundi na watoto watatu ambao ni Taji, Beuty na Lulu ambaye yupo masomoni nchini China na anatarajiwa kuwasili leo.

Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :