MAUAJI MAKUBWA YARIPOTIWA SUDAN KUSINI
Posted in
No comments
Wednesday, December 25, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Mtu mwingine kutoka Juba amesema watu wenye silaha kutoka kabila la Dinka walikuwa wakiwashambulia kwa risasi watu kutoka maeneo ya Nuer.Ghasia hizo zimekuja huku kukiwa na hali ya kugombea madaraka kati ya Rais Salva Kiir, kutoka kabila la Dinka, na aliyekuwa naibu wake Riek Machar kutoka kabila la Nuer.
Serikali ya Sudan Kusini imekanusha kuhusika na ghasia za kikabila.Taarifa hizo zimekuja wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza askari 5,500 wa Umoja wa Mataifa katika kikosi cha askari 7,000 wa Umoja wa Mataifa waliopo Sudan Kusini.
Waasi wanaomuunga mkono makamu wa rais aliyefukuzwa Riek Machar walitwaa miji mikubwa wiki iliyopita.Maelfu ya watu wamekimbia mapigano.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :