TUNDU LISSU AHOJI KWANINI BUNGE HALIJAAHIRISHWA KUAFUATIA KIFO CHA NELSON MANDELA
Posted in
No comments
Saturday, December 7, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu, Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema),
amehoji kwanini Bunge lilikuwa likiendelea na vikao licha ya kupata
taarifa ya kifo cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela (95)
aliyefariki dunia juzi usiku.
Aliuliza swali hilo kwa Spika Anne Makinda, baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu jana asubuhi.
“Ninaumwa sana, usiku kucha sikulala, nina homa, na hata sasa nimejikongoja tu kuja humu ndani, bado ninaumwa…nimeshangaa kuona msiba wa Bara zima, msiba wa Mtoto wa Afrika nadhani hatutapata mwingine kama yeye (Mandela), bunge linaendelea na vikao vyake kama kawaida…nilitegemea Bunge lingeahirisha kikao hiki walau kwa leo,” alisema.
Akijibu Spika wa Bunge ambaye mapema kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu na baada ya kumaliza kwa dua, alilitaarifa bunge kuhusu kifo cha Mzee Mandela, alisema, “mambo ya nchi yanaenda kwa utaratibu wa nchi.” Lakini alisema kesho, (leo) bunge litatoa azimio la kumkumbuka na kumsifu.
“Tutatoa utaratibu wa kibunge kesho (leo), tutatoa azimio la kumkumbuka na kumsifu. Tunao utaratibu wa kuahirisha vikao vya Bunge lakini kwa hili ni utaratibu wa nchi,” alisema.
Hata hivyo, baada ya kumaliza kipindi cha wenyekiti wa kamati kuwasilisha taarifa za kamati zao, Spika aliwaomba wabunge kusimama kwa dakika moja kumkumbuka Mzee Mandela na kuiombea roho yake ipumzike mahali pema peponi.
CHANZO:
NIPASHE
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :