DC SIHA AITAKA HALMASHAURI YA SIHA KUIMARISHA UKUSANYAJI WA USHURU
Posted in
No comments
Wednesday, January 22, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Na Omary Mlekwa,
Siha
MKUU wa wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro, Dkt Charles Mlingwa amewataka wataalumu wa halmashauri hiyo kuimarisha hali ya ukusanyaji wa ushuru wa aina mbalimbali bila kubugudhi wananchi ili kuongeza mapato ya ndani.
Pia aliwataka wataalamu hao kuwa na takwimu sahihi za walapi kodi wakubwa na wadogo ili kuweza kuweka makisio ya mapato na matumizi yanayoendana na utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo
Akizungumza na wajumbe wa baraza pamoja na wananchi waliohudhuria kikao maalumu cha baraza la madiwani cha kujadili na kupisha bajeti ya mwaka wa fedha wa mwaka 2014/2015 alisema wataalamu wakiimarisha ukusanyaji itasaidia kupunguza utegemezi wa kutoka serikalini.
Kauli hiyo aliitoa baada ya baadhi ya madiwani kupinga bajeti y ushuru wa mazao kwa madai kuwa inawaumiza wakulima wa mazao mbalimbali .
Akitoa hoja hiyo diwani wa viti maalumu Claudi Muro alisema suala ushuru wa mazao katika masoko mengi limekuwa kero ambapo alitaka kujua serikali ya wilaya ina mpango gain wa kuondoka tatizo hilo?
Alisema ushuru unatoza katika masoko unawaumiza wakulima na kuwanufaisha wazabuni huku halmashauri ikiendelea kupoteza mapato kutokana na wakulima wengi kukwepa ushuru huo
Nae diwani wa kata ya Sanya Mjini Juma Jane alisema ushuru unaotozwa na wazabuni ni kati ya shilingi 2500 hadi 4500 jambo ambalo limekuwa kero kwa wakulima na baadhi yao wamekuwa wakitafuta hata njia za panya ili kukwepa ushuru huo,
Alisema ushuru unatozwa katika halmashauri ya Siha ni mkubwa ikilinganishwa na halmashauri za jirani ambapo halmashauri zote zinazopakana nazo zinatoza ushuru kati ya shilingi 500 hadi shilingi 1000
Akichangia hoja hiyo, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jonathan Nassari aliwataka wataalamu kuliangalia suala hilo kwa kina na kukaa na wazabuni ili kuweza kulitafutia ufumbuzi wa suala hilo
Akizungumzia hali hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo Rashid Kitambulio mbali na kukiri kupokea malalamiko mengi juu ya tozo hizo alisema kuwa ofisi yake ina andaa utaratibu wa kukutana na
wazabuni wote ili kuweza kuliangalia suala hilo kwa upya ikiwa ni juhudi za kuondoa kero hiyo.
Alisema katika maelekezo ya awali mzabuni huyo alielekezwa kukusanya kiwango kisicho zidi asilimiaa 5% kutoka kwa wafanyabishara hao wa mazao ya Chakula na kwamba mkataba huo pia uliwaondoa katika tozo hiyo wakulima wanaorudisha mazao yao kutoka shambani baada ya kuyavuna.
Awali akitoa taarifa ya rasmi ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka fedha 2014/2015 mkurugenzi wa halmashauri Rashidi Kitambulio alisema kuwa wanatazamia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 19.320,034,512 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ruzuku toka serikali kuu na mapato ya ndani
Kitambulio alifafanua kuwa kiasi hicho ni sawa na ongezeko la shilingi bilioni 2,297,943,008 ikilinganishwa fedha zilizoidhinishwa katika bajeti ya shilingi bilioni 17,022,091,594 ya mwaka wa fedha 2012/2013
Alisema katika bajeti hiyo wanakusudia kukusanya shilingi bilioni 1, 935,247,550kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ikiwemo ushuru wa masoko, ushuru wa vituo vya mabasi , ushuru wa mazao na vyanzo vingine vilivyopo katika halmashauri hiyo.
“Ndugu wa baraza la madiwani tunatazamia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 12,421,114,116 kwa ajili ya mishahara, miradi ya maendeleo shilingi bilioni 4,535,083,755, na matumizi ya kawaida shilingi bilioni 1,856,866,786,”alisema
“Na katika kuendeleza vijana na wanawake kupitia asilimia tano kwa kila kundi rasmu hiyo ya bajeti tumetenga kiasi cha shilingi milioni 168,782,675 kutokana na mapato ya ndani nah ii ikiwa ni asilimia kumi ya mapato yote ya ndani na pia tumetenga kiasi cha shilingi milioni 337,565,510”alisisitiza Kitambulio
Hata hivyo wajumbe wa baraza hilo la madiwani walipisha rasimu ya bajeti ya mapato na matumizi kwa ajili ya halmashauri hiyo ya shilingi jumla ya shilingi bilioni 19.320,034,512

Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :