DKT. MIGIRO KUBADILI SEKRETARIETI YA CCM?
Posted in
No comments
Sunday, January 12, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
IWAPO
majina ya Asha-Rose Migiro na Mwigulu Nchemba yataingizwa kwenye Baraza
jipya la Mawaziri, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitalazimika kufanya
mabadiliko ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, IMEBAINIKA!!!
Wakati joto hilo la baraza jipya ya mawaziri likizidi kupanda, taarifa nyingine zilizolifikia gazeti hili jana zinaeleza kuwa Kamati Kuu ya Chama hicho tayari imepanga kuanza kukutana kesho, kujadili masuala kadhaa, likiwemo hilo la mawaziri.
Dk. Migiro na Nchemba wanapewa nafasi kubwa ya kuingizwa kwenye baraza jipya la mawaziri, linalotarajiwa kutangazwa wakati wowote mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha Kamati Kuu.
Kwamba kama wakijumuishwa kwenye baraza hilo, watapoteza sifa za kuwa kwenye sekretarieti hiyo kwa sababu kanuni za CCM, haziruhusu Waziri kuwa mjumbe wa Sekretarieti hiyo ya chama.
Ndani ya Sekretarieti hiyo ya Halmashauri Kuu ya CCM, Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mwigulu Nchemba ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho.
Wengine wanaounda Sekretarieti hiyo ya Halmashauri Kuu ya CCM, ni Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Oganaizesheni, Mohammad Seif Khatib pamoja na Katibu wa Fedha na Uchumi, Zakia Meghji.
Taarifa zinaeleza kuwa Dk. Asha-Rose Migiro anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwa Waziri wa ama Wizara ya Mambo ya Nje au Fedha.
Kwamba waziri aliyepo sasa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, anaweza kuhamishwa na kupelekwa Wizara ya Mambo ya Ndani, kutokana na uzoefu wake mkubwa katika masuala ya usalama wa nchi na pia historia yake ya nyuma ambapo aliwahi kuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, endapo ikishindikana kwa Dk. Migiro kupewa Wizara ya Mambo ya Nje, basi atapewa Wizara ya Fedha, kutokana na sifa yake ya kuwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), kwamba itasaidia nchi kukuza uhusiano kimataifa pamoja na kuvutia wahisani kwa ajili ya kuisaidia nchi.
Kwa upande wake, Nchemba anatajwa katika nafasi ya Naibu Waziri wa Fedha na hatua hiyo inatokana na kigezo cha elimu yake ya juu ambapo alisomea masuala ya uchumi.
Wakati hayo yakijiri, MTANZANIA Jumapili imedokezwa kwamba Kamati Kuu ya CCM ambayo inatarajia kukutana kati ya Januari 13-15, pamoja na mambo mengine, itajadili rasimu ya pili ya Katiba Mpya, mawaziri waliong’oka pamoja na kutathimini hali ya siasa nchini.
Alipotafutwa na gazeti hili, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, alithibitisha taarifa hizo, lakini alisema kuwa Kamati Kuu itajadili ajenda moja tu ya kupitisha jina la mgombea ubunge wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mansour Yusuph Himid, ambaye alivuliwa uanachama hivi karibuni.
Katika hatua nyingine, taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa Jumatatu na Jumanne wiki hii, Rais Jakaya Kikwete alikutana na Makamu wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Ikulu, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuanza kupanga safu ya baraza la mawaziri.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa, Rais Jakaya Kikwete anatarajia kutangaza Baraza jipya la Mawaziri kati ya Januari 13 hadi 15, mwaka huu, baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa wiki kadhaa sasa, kutokana na msiba wa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, lakini pia sherehe ya Mapinduzi inayoadhimishwa leo.

Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :