MWANDISHI WA BBC ANN WAITHERA AMEFARIKI DUNIA.
No comments
Tuesday, January 28, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Na Reporter Wetu, London
Shirika la habari la BBC limempoteza
mwandishi wa habari Ann Waithera. Ann alikuwa anafanya kazi na BBC katika ofisi
za Nairobi na amekuwa akiugua Saratani ya Ubongo kwa karibu miaka miwili.Ann
aliwahi kuwa ripota wa BBC mjini Addis Ababa Ethiopia.
Kabla ya kujiunga na BBC Ann
alifanya kazi na shirika la habari la Nation Media Group nchini Kenya na
Citizen TV. Ann alikuwa na umri wa miaka 39.Waandishi wenza wa Ann BBC
wameelezea masikitiko yao na jinsi watakavyomkumbuka Ann katika enzi zake alipokuwa anafanya kazi nao.
Razvan Scortea mmoja wa wakuu wa BBC
amesema : "Nimeshtushwa sana na kifo cha Ann. Alikuwa mtu mzuri , mwerevu
mpenda watu na mwenye matumaini kwa kila jambo. Mungu ambariki.'' Mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera
ameelezea kuwa ni jambo la kuhuzunisha sana kumpoteza Ann.
''Nimehuzinika sana. Anne alikuwa
mwandishi mahiri . Kila nilipomtembelea nilivutiwa sana na matumaini ya Ann kupona.
Hata katika mkesha wa krismasi, nilipozungumza na Ann alikuwa mcheshi sana.
Nakumbuka Ann ndiye alikuwa mwandishi wetu wa kwanza mwenye uwezo wa kuripoti
katika lugha zaidi ya moja mjini Addis Ababa Ethiopia,'' alisema Solomon
Mkuu wa idhaa ya kiswahili ya BBC
Ali Saleh naye pia ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha Ann akimkumbuka kama
mwandishi mahiri na mwenye kujitolea kwa kazi zake.'Nakumbuka kufanya naye kazi kabla
ya yeye kwenda Addis Ababa, na kufanya mipango ya kila alichotarajiwa kufanya.
Matumaini mengi ila yamekatizwa mapema mno.''
alisema Elizabeth Blunt aliyekuwa
mwandishi wa BBC mjini Addis Ababa kabla ya Ann kuchukua usukani kutoka kwake. "Anne alikuwa mmoja wa
waandishi mahiri wa BBC nchini Kenya . Kifo kimetupokonya mmoja wa waandishi
wenye talanta kuu Afrika Mashariki.'' Kauli ya David Okwemba mhariri mkuu wa
ofisi ya BBC Nairobi Kenya.
Mhariri mkuu wa idhaa ya Hausa mjini
London Mansur Liman, ametuma rambi rambi kwa familia ya Ann, akiwaombea utulivu
wakati huu mgumu.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :