Showing posts with label Matukio. Show all posts
Showing posts with label Matukio. Show all posts

Guzo mitandaoni: Thamani ya Barua ya Mohammad Ali kwa Mandela

Guzo mitandaoni: Thamani ya Barua ya Mohammad Ali kwa Mandela

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Barua iliyowekwa sahihi na mwanamasumbwi Mohammad Ali na kuandikiwa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, akitoa rambu ramba zake kufuatia kuawa kwa mtu aliyekuwa akipinga ubaguizi wa rangi imeuzwa kwa pauni 7,200.
Muuzaji wa barua hiyo Andrew Aldridge alisema, "ni vyema kuwa Mohammad Ali alikuwa mwanamichezo bora zaidi hukui naye Nelson Mandela akiwa mtu mashuhuri zaidi katika karne iliyopita.
Barua hiyo ilipiwa chapa cha msaidizi wa meneja wa hoteli ya Elangeni iliyo mjini Durban ambapo Ali alikuwa akiishi wakati huo. Barua hiyo iliyouzwa kwa mnunuzi kutoka nchini Marekani ilitarajiwa kuuzwa kwa kati ya dola 6,000 na 8,000.
Muhammad Ali alikuwa nchini Afrika Kisini kwa kipindi kifupi mwezi Aprili mwaka 1993 baada ya kuwasili muda mfupi baada ya kuuliwa kwa Chris Hani tarehe 10 mwezi Aprili.
Hani alikuwq kamanda wa kundi la Umkhonto We Sizwe, kundi lililojihami la ANC. Alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya ubaguzi wa rangi na aliuaw mkereketwa mmoja nje ya nyumba yake eneo la Boksburg.
BBC

Wasiwasi DR Congo muhula wa Kabila ukifikia kikomo

Wasiwasi DR Congo muhula wa Kabila ukifikia kikomo

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mzozo wa kisiasa unaendelea kutokota nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku muhula wa Rais Joseph Kabila ukifikia kikomo leo, kwa mujibu wa katiba. Mazungumzo ya kutafuta suluhu kati ya serikali na upinzani yaliahirishwa wiki iliyopita baada ya kukosekana kwa mwafaka. 
Mazungumzo hayo yanayoongozwa na maaskofu wa kanisa Katoliki yanatarajiwa kurejelewa Desemba 21. Kuna wasiwasi kwamba huenda kukatokea maandamano Jumatatu wafuasi wa upinzani wakipinga kuendelea kusalia madarakani kwa Bw Kabila.
Upinzani unamlaumu Rais Kabila ukisema ndiye aliyechangia mzozo wa sasa kwa kujaribu kukwamilia madaraka. Watu zaidi ya 50 waliuawa kwenye maandamano ya upinzani mwezi Septemba. Maafisa 3 wa polisi pia waliuawa kwenye maandamano hayo.
Rais Kabila amesema ataendelea kusalia madarakani kwani uchaguzi mkuu haukufanyika ilivyotarajiwa mwezi Novemba na hivyo basi hakuna mrithi aliyechaguliwa.
Wanajeshi na maafisa wa polisi wameweka vizuizi kwenye mji mkuu Kinshasa, kukiwa na wasiwasi wa kutokea tena kwa maandamano na ghasia.Serikali iliagiza kampuni za mawasiliano kufungia mitandao ya kijamii na imeahidi kukabiliana vikali na waandamanaji.
Waziri wa mawasiliano Lambert Mende ameambia BBC: "Kabila atasalia madarakani hadi rais mpya achaguliwe. Hakuna jambo jingine litakalofanyika. Mtu akijaribu kuvuruga amani hapa mjini, atakumbana na polisi kama inavyofanyika maeneo mengine duniani."
Uchaguzi uliahirishwa hadi 2018, hatua ambayo upinzani unasema ni jaribio la Bw Kabila la kutaka kusalia madarakani. Kwa mujibu wa katiba, muhula wa pili wa Rais Kabila, aliyeingia madarakani baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka 2001, unafaa kumalizika tarehe 19 na kuwe na rais mpya 20 Desemba. 
Mwaka uliopita, watu 12 waliuawa katika maandamano ya upinzani. Tangu kujinyakulia uhuru zaidi ya miaka 55, hakuna kiongozi aliyewahi kumkabidhi mrithi wake madaraka kwa njia ya amani.

BBC

jaydee: hii ndio siri ya kufanya vizuri miaka yote

jaydee: hii ndio siri ya kufanya vizuri miaka yote

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na remix ya wimbo ‘Together’  akiwa ameshirikiana na mpenzi wake Spicy, amedai siri ya yeye kukaa kwenye game kwa muda mrefu inatokana na kujichanganya kwa kufanya kolabo ya wasanii tofauti tofauti pamoja na kukubali mawazo mapya kutoka kwa watu wake wa karibu.
“Muziki namna ambavyo naufanya mimi kila siku nabadilisha watu wakufanya nao kazi, sifanyi kazi na watu wale wale kila siku pia napokea mawazo kutoka kwa watu wengine tofauti,” alisema Jay Dee. “Kwa sababu naamini kila mtu ana mchango wake awe ni msanii mchanga au mkubwa. 
Lakini ukisema unafanya kazi na watu wale wale kila siku utakuta muziki wako unafanana, na hiyo ndiyo sababu ambayo inafanya muziki wangu uweze kubadilika kutokana na mazingira,” Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kusubiria kazi mpya akiwa na Spicy.

Maskini Mr. Nice azushiwa kifo kwenye Social Media

Maskini Mr. Nice azushiwa kifo kwenye Social Media

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mfalme wa Takeu Style, Lucas Mkenda, Mr. Nice amesikitishwa na watu ambao wamemzushia kifo katika mtandao wa kijamii. Mtandao mmoja wa kijamii uliandika taarifa za uongo kwamba muimbaji huyo amefariki akiwa nchini Tanzania.
Mr Nice ambaye yupo nchini Kenya amesema alishangaa kuona watu wakimpigiwa simu kwa nyingi na kuulizwa kuhusu afya yake na alivyofuatilia akagundua kuna mtandao umeandika taarifa za uongo kwamba amefariki.
Kupitia facebook, Mr Nice aliamua kuandika taarifa hii:
East africa vibes nawashukuruni sana kwa kunizushia kifo sina la kuwajibu ,,ila mungu awalipe kadri ya vile mnavyostaili kwa hiki mlichonizushia leo ….mungu ni wetu sote na hasikilizi amri za binadamu so atakaponihitaji ataniita kwa mapenzi yake but si nyie east african vibes mnaoweza kuniua wala yeyote yule chini ya hili jua
…kama nyie hamuioni thamani yangu hilo ni juu yenu kwani huku niliko mimi ni kama lulu na maisha yanaendelea tena kwa kiwango cha juu kabisa ..hii si mara ya kwanza kunizushia kifo na mambo mengine ya ajabu ajabu ila all in all mi nipo na bado mtaniona sana nikiendelea kuwepo ….im total dissapointed kwakweli …mungu awape stahiki yenu ..THANKS SANA EATV 13/12/2016

Jionee jinsi Kuwait walivyoanikiwa kuivuta bahari nchi kavu ili kutengeneza mji mpya

Jionee jinsi Kuwait walivyoanikiwa kuivuta bahari nchi kavu ili kutengeneza mji mpya

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mwaka 1986 Khalid Yousef Al Marzouq alikuwa na wazo la kujenga mji katika jangwa, Al Marzouq alikufa lakini mwanae Fawaz ameifuata ndoto ya baba yake ambayo imezaa matunda na ujenzi huo ulianza 2003 baada ya kuchelewa kutokana na vita ya ghuba.
Eneo hilo ambalo liko mpakani mwa Kuwait na Saudi Arabia halikuonekana kama ni eneo sahihi la kutengeneza mji mpya lakini Mji huo wa ajabu umejengwa kwenye jangwa kwa kuivuta bahari nchi kavu kwa mfumo unaoitwa ingenious system of tidal gates, mfumo ambao umeileta bahari mile 6 nchi kavu. Mji huo unaweza kuchukua nyumba 250,000.
33CC10FE00000578-3550045-A_unique_system_of_tidal_gates_have_been_used_to_convert_the_two-a-91_1462895964135 33CC13ED00000578-3550045-The_new_city_pictured_is_only_a_few_miles_from_the_border_with_S-a-88_1462895964132 33CC14BD00000578-3550045-Few_yachtsmen_would_currently_consider_passing_through_the_Strai-a-97_1462895964143
DCIM100MEDIADJI_0170.JPG
DCIM100MEDIADJI_0232.JPG
33CC15D200000578-3550045-The_new_sea_city_is_a_vast_engineering_undertaking_which_has_cos-a-84_1462895964127 33CC15E200000578-3550045-The_entire_area_was_formerly_a_non_descript_salt_marsh_and_it_to-a-89_1462895964133 33CC15F600000578-3550045-This_satellite_image_shows_how_a_network_of_inlets_which_will_be-a-83_1462895964124
33CC18BE00000578-3550045-The_city_is_being_named_after_Sheikh_Sabah_Al_Ahmad_right_the_86-a-98_1462896063315
Fawaz Khalid Al Marzouq (kushoto) ambaye ameitimiza ndoto ya baba yake na kulia ni Kiongozi wa Kuwait Sheikh Sabah Al Ahmad  ambaye mji huo umepewa jina lake.  
33CC17FF00000578-3550045-Development_will_take_place_in_10_phases_and_over_25_years_so_do-a-94_1462895964139 33CC18B400000578-3550045-The_area_has_been_carved_out_of_the_desert_Temperatures_during_t-a-96_1462895964142 33CC157F00000578-3550045-Billions_of_dollars_have_been_invested_into_the_project_but_it_i-a-92_1462895964136 33CC148900000578-3550045-A_key_element_of_the_project_is_a_yachting_marina_and_retail_cen-a-85_1462895964128 33CC174800000578-3550045-Wish_you_were_here_A_picture_postcard_from_Sheikh_Sabah_Al_Ahmad-a-95_1462895964141
DCIM100MEDIADJI_0013.JPG
340997F400000578-3550045-image-a-117_1462963343766

Mungu Mkubwa! Tizama Mama mwenye miaka 70 aliyepata Mtoto

Mungu Mkubwa! Tizama Mama mwenye miaka 70 aliyepata Mtoto

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

3401C30C00000578-3582592-image-a-1_1462882141093 34094D4A00000578-3584606-image-a-21_1462964860004 34094D3400000578-3584606-image-a-20_1462964845995 340949C100000578-3584606-image-a-19_1462964842643 3409347700000578-3584606-image-a-22_1462964861793
340932A500000578-3584606-image-a-18_1462964832901
ULIKOSA SHOW YA KAYUMBA AKIFANYA VITU VYAKE CLUB BILICANAS? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI

UNESCO, SERIKALI WATIA SAINI MRADI WA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU

UNESCO, SERIKALI WATIA SAINI MRADI WA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
DSC_0023
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (wa pili kulia), Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (kushoto), Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia), Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja na mkalimani wa Balozi wa China wakifurahi jambo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani) akiwasili kwenye chumba cha mikutano Wizara ya Elimu kwa ajili ya hafla fupi ya kutiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Modewji blog team

SERIKALI na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jana wametiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini. Akizungumza baada ya kutiwa saini kwa mkataba huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema mradi huo ni mkombozi mkubwa katika maandalizi ya kufundisha kwa kutumia Tehama nchini.

Alisema mpango huo wenye kuwezesha walimu kujifunza Tehama unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China ambao ndio wamepitisha fedha zao UNESCO. Katika utiaji saini huo ambapo Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing alikuwepo, katika jumla ya uhai wa mradi ambao ni miaka miwili , miundombinu ya ufundishaji masomo ya sayansi na hesabu katika vyuo vya walimu vya Monduli na Tabora itaboreshwa.

Katika mradi huo walimu watafundishwa elimu ya Tehama, namna ya kufundisha na kujifunza. Katibu mkuu Mchome alisema kwamba vyuo hivyo viwili vitawezeshwa kuwa na mtandao ambao utaunganishwa na vyuo vingine vinane vya masomo ya sayansi na hesabu kwa ajili ya kubadilishana taaluma.

Pia vyuo hivyo vitawezeshwa kuandaa programu zenye kuelezea mfumo wa utoaji huduma za Tehama kwa ajili ya walimu wa masomo ya sayansi na hesabu.

DSC_0037
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akisalimina kwa furaha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (kulia) na kushoto ni Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (aliyeipa mgongo kamera).

Profesa Mchome alisema ili taifa liweze kusonga mbele katika mpango wake wa kufundisha kwa kutumia Tehama ni vyema kuandaa walimu na fedha za China kupitia Unesco zitasaidia maandalizi hayo.

“Tunaamini tukiwekeza katika vifaa vya kupromoti Tehama, walimu wakifundishwa na kuandaliwa vyema, wataenda kusaidia kufundisha na kuwezesha matumizi ya Tehama katika shule zao.” Alisema Profesa Mchome.
Alisema japo zipo program ndogo nyingine , program waliyotia saini jana ilikuwa kubwa na yenye tija itakayoimarisha ubora wa elimu kwa kuwapa wanafunzi elimu ya kujitegemea, elimu yenye kuwakwamua kiujuzi na kuutumia ujuzi huo kwa maendeleo yao na taifa.

Tanzania ni miongoni mwa mataifa barani Afrika ambayo mapema wametambua thamani ya kufundisha kwa njia ya Tehama ili kuboresha elimu na mfumo wa elimu. Taasisi zitakazohusika na mradi huo ni pamoja na Chuo Kikuu Huria (OUT) na Taasisi ya Elimu nchini(TIE) kwa kuratibiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

DSC_0074
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) pamoja na Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (kushoto) kabla ya kutiliana saini mkataba huo.

DSC_0080
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo kabla ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome na Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi. Waliosimama wakishuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Joel Nanauka wa UNESCO, Afisa tawala msaidizi wa UNESCO, Rahma Islem, Afisa mipango wa utamaduni wa UNESCO, Rehema Sudi, Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing, Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja na Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha.
DSC_0084
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome wakitiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China. Wanaoshuhudia tukio hilo waliosimama ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. LU Youqing (wa pili kushoto), Ofisa anayeshughulikia masuala ya elimu kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar (wa pili kulia), Afisa mipango wa utamaduni wa UNESCO, Rehema Sudi (kushoto), Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha na Kulia aliyeketi ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
DSC_0086
Zoezi la kusaini mkataba likiendelea.
DSC_0089
Wakifurahi kwa pamoja mara baada ya zoezi la kutia saini kukamilika.
DSC_0090
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome wakibadilishana hati za mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. LU Youqing(wa pili kushoto) pamoja na Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia).
DSC_0091
DSC_0103
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo baada ya kutiliana saini mkataba huo.
DSC_0068
Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia) akizungumza jambo na Afisa wa ubalozi wa China (katikati) na Kushoto ni Afisa Utawala msaidizi wa UNESCO, Rahma Islem.

Happy Birthday MO

Happy Birthday MO

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
DSC01228-Edit
MODEWJI BLOG TEAM : Thanking you for being a great boss just isn't enough for your special day! Thank you for inspiring us to be our best! Happy birthday, boss!
And below is a small gift from us!
IMG_9643  
Please join us to wish him a Happy Birthday by follow him on his twitter @moodewji and instagram @moodewji

Miaka 90 ya Rais Ali Hassan Mwinyi

Miaka 90 ya Rais Ali Hassan Mwinyi

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Leo, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi anatimiza miaka 90.
Tulipata fursa ya pekee kuketi naye akatueleza mambo machache kuhusu maisha yake
UNGANA NASI

Hatimaye wakazi wa kijiji cha Amani Tabora usiku wa leo watalala bila kero ya kunguni!

Hatimaye wakazi wa kijiji cha Amani Tabora usiku wa leo watalala bila kero ya kunguni!

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Kijji cha Amani kinavyoonekana
Taasisi ya Better Living Aid kupitia kampuni ya Royal Nsyepa General Supplies ambayo mkurugenzi wake ni Bw Mgalula Fundikira za jijini Dar es Salaam leo imepeleka mtaalamu wa upulizaji madawa ya kuuwa wadudu kama kunguni na wengineo katika kijiji cha Amani kilichopo km 6 nje ya mji wa Tabora. Hatua hiyo ya Better Living Aid ilifuatia ombi toka kwa wakazi wa kijiji hicho chenye wakazi wapatao 70 ambao baadhi yao ni wazee na wenye uathirika wa gonjwa sugu la ukoma, pamoja na changamoto ya kunguni pia wakazi wa hao wametoa maombi kwa taasisi hiyo nawasamaria wema wengine wajengewe vyoo zaidi kwani kwa sasa wana vyoo viwili tu vilivyo kwenye hali ya kutumika, huku vingine vikiwa vimejaa na haviwezi kunyonyeka. Akiongea na mtandao huu mwenyekiti wa kijiji hicho Bw George Lusambilo alisema"kwa kweli tunaishukuru sana taasisi hii kwa kutuletea msaada huu, kwani tumekuwa tukilala kwa taabu sana, naona kuanzia leo tutalala kwa raha kama watu wengine" pia aliongeza "Ila tu jamani msituchoke, bado tunakumbushia ombi la kujengewa vyoo zaidi kwani idadi yetu na ukilinganisha na vyoo tulivyonavyo kwa kweli ni changamoto, lakini pia tunaomba tupate hata ka zahanati kadogo ili mganga na muuguzi wapate mahala maalum pa kutuhudumia hasa sisi wagonjwa wa ukoma"

Naye afisa ustawi wa jamii mkoa Bw Charles Makoye alisema "kwa niaba ya serikali naishukuru sana tasisi hii ya Better Living Aid kwa jitihada zao za kuboresha maisha ya wakazi wa hapa kijijni na napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kusaidia kijiji hiki kwani ustawi wa jamii si suala la serikali peke yake bali ni la jamii nzima inayotuzunguka kwani hawa wazee wametoka huko huko katika jamii zetu.

Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid ametoa wito kwa makampuni na watu binafsi kuiunga mkono taasisi hiyo katika jitihada zake za kuwajengea vyoo na zahanati wakazi wa kijiji hicho. Vile vile ameeleza dhamira ya taasisi hiyo kutafuta wafadhili ili kujenga zahanati katika kijiji cha Masweya, wilayani Ikungi mkoa wa Singida alisema "Nilipata kufika kijijini Masweya mapema mwaka huu ambako nilipata kujua kwamba wakazi wa hapo hulazimika kutembea km 30 na ushee kwenda kjiji cha Mtunduru kupata huduma za matibabu. Hivyo Better Living Aid itafanya kila liwezekanalo kijiji hicho kipate zahanati japo mdogo ya kuweza kuhudumia wagonjwa wa Malaria nk pia zahanati iweze kutoa huduma kwa wazazi, kitu mambacho kwa sasa hakipo kjijini Masweya. 

Shukurani za dhati ziwaendee Mh Munde Tambwe (viti maalum Tabora), Mh Aden Rageh (Mbunge Tabora mjini) Bibi Joha Masawe, Bi Mtagwa Fundikira, Bibi Jamila Kaimika, Bibi Celina Koka na wanachama wote wa kundi la Better Living Aid Tunashukuru kwa msaada wa hali na mali iliyowezesha kijiji cha Amani kufanyiwa fumigation bila kumsahau mtaalamu Bw Selemani Muhogo wa kampuni ya SILVER ENTERTRADE LIMITED aliyepulizia dawa hiyo.

Baadhi ya magodoro ya wakazi hao yakiwa yametayarishwa kwa kupuliziwa dawa

Bw Muhogo akiandaa mashine ya kupulizia dawa
Hpa akianza kunyunyiza dawa kwenye magodoro

Job DONE

Baadhi ya vyoo vya hapo kijijini


Mzee Hamisi Husseni akisubiri vifaa vyake vitiwe dawa
Badhi ya mizigo ya wakazi wa kijiji hicho
Afisa ustawi wa jamii Bw Charles Makoye akiongea na mkazi wa kijini hapo.

Bibi Theresia Joseph akiwa nje ya chumba chake akisubiri huduma ya kupuliziwa dawa ya kuuwa  kunguni na wadudu wengine.
Rundo la mahindi likiwa limotolewa nje kupisha upulizaji dawa ya kuua kunguni nani ya chumba yalimokuwa yamehifadhiwa.
Baadhi ya panya waliokutwa ndani ya chumba cha mkazi mmoja wa kjijini hapo leo.
Blogger wa Aloyson.com akiwa na Mzee Hamisi Husseni
Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid Mkala Fundikira kushoto akiwa na mwenyekiti wa kijiji cha Amani Bw George Lusambilo baada ya zoezi la upulizaji dawa ya kuuwa wadudu kunguni waliokuwa wakwasumbua mno wakazi wa kijiji hicho cha wazee wasiojiweza na waathieika wa ugonjwa wa ukoma.

Baada ya ya kupuliziwa dawa baadhi ya kunguni wanaonekana wakiwa wamekufa.
Blogger Juma Kapipi wa JHabari blog akiongea na mhanga wa kunguni baada ya kumhoji
Baadhi ya nguo zikichomwa moto baada ya kukutwa na kunguni wengi kupita  kiasi.
Habari na picha kwa hisani ya TBN Central zone!

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .