HAYA NDIO MAONI ALIYOYATOA MAKAMU WA RAIS DKT BILAL KWA TUME YA KATIBA LEO
Posted in
No comments
Wednesday, January 23, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya,
Jaji Joseph Sinde Warioba, wakati tume hiyo ilipofika Ofisini kwake
Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuchukua maoni yake binafsi
ikiwa ni sehemu ya kuchangia maoni ya katiba mpya.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza wakati akitoa maoni yake kwa Viongozi wa Tume ya katiba
mpya, iliyofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo ikiwa ni
sehemu ya jukumu la tume hiyo la kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa
maoni ya Katiba mpya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati akitoa maoni yake.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya,
Jaji Augustino Ramadhan, wakati Tume hito ikiondoka Ikulu baada ya
kupokea maoni ya Mhe. Makamu leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa tume ya Kukusanya
maoni ya Katiba Mpya, baada ya mazungumzo yao ya kupokea maoni
yaliyofanyika leo Januari 23, 2013, Ikulu jijini Dar es Salaam.
*******************************************
*MHESHIMIWA
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ATOA MAONI YAKE KWA
TUME YA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA MPYA JANUARI 23, 2013, IKULU JIJINI
DAR ES SALAAM
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
amekutana na ujumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya iliyokuwa
chini ya Mwenyekiti wake Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde
Warioba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu
Agostino Ramadhan. Mheshimiwa Makamu wa Rais amepata fursa ya kukutana
na Tume hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Tume ya Katiba Jaji Warioba kabla ya kumruhusu Mheshimiwa Makamu Wa
Rais kutoa maoni yake, alimuelezea namna tume hiyo inavyofanya kazi na
namna zoezi zima la kukusanya maoni ya mtu mmoja mmoja lilivyofanyika na
kisha akaeleza kuwa, tume hiyo inaendelea na zoezi hilo kwa kukutana na
makundi maalum sambamba na mtu mmoja mmoja kufuatia umuhimu wa hoja
ambazo tume inakutana nazo na hivyo kuhitaji ufafanuzi.
Katika
muktadha huo, Jaji Warioba sambamba na kumpa fursa ya kuchangia maoni
yake mengine anayopenda alimtaka Mheshimiwa Makamu wa Rais kujikita
zaidi katika suala la Muungano kufuatia yeye kuwa na uzoefu wa kiuongozi
katika serikali zote mbili yaani ya Muungano sambamba na ile ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Akizungumzia
suala la Muungano Makamu wa Rais Dkt. Bilal ameieleza Tume kuwa yeye ni
muumini wa Muungano wa serikali mbili na kwamba haoni sababu ya
kubadili mfumo uliopo kwa kuwa umeipatia tija nchi yetu na kuipambanua
kama nchi yenye muungano wa mfano katika dunia.
Pia
alifafanua kuwa mfumo wa serikali mbili umesaidia kujenga na kudumisha
udugu, amani na utulivu baina ya wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani
kwa kipindi cha miaka 49 sasa.
Tanzania
imechangia kitu kikubwa katika historia, kudumisha Muungano wa mfumo wa
serikali mbili kati ya nchi mbili, kubwa na ndogo, jambo ambalo kwa
nchi nyingine za Afrika wameshindwa. Kumekuwepo na nchi nyingi ambazo
ziliungana na kushindwa kudumu kama tulivyo sisi. Hatuna haja ya
kujifunza mfumo mpya wakati tulionao umeweza kudumu, « alisema.
Katika
ujumbe wa tume uliofika kuchukua maoni ya Mheshimiwa Makamu wa Rais ni
pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Profesa wa Sheria
Palamagamba Kabudi, Ndugu Simai Said, Ndugu Assa Rashid, Ndugu Sasmir
Kyuki, Ndugu Salum Athuman, Ndugu Juma Mzalau na Mratibu wa Tume hiyo
Ndugu Ramadhan Kailima.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :