ZITTO AWEKA PINGAMIZI MAHAKAMANI KUZUIA KIKAO CHA CHADEMA.
Posted in
No comments
Thursday, January 2, 2014
By
danielmjema.blogspot.com

Baada ya kuwepo kwa kila dalili za Mh.Zitto kabwe kutotendewa haki na
Kikao cha Kesho cha kamati Kuu chadema.Zitto ameamua kuweka pingamizi
la kukao hicho,kimahakama inawezekana na inaruhusiwa kuweka pingamizi
ama kikao kisiwepo au wasikujadili kwenye kukao husika.
Slaa na mbowe wamekuwa akionesha dhamila ya wazi ya kutaka kumfukuza Zitto bila kufuata katiba ya Chama.Awali Mwanasheria wa Zitto aliweka bayana kuwa Zitto alivuliwa nyadhifa zake CHADEMA bila kupewa nafasi ya Kuhojiwa,Mashitaka n.k kitu ambacho ni Ukiukwaji Mkubwa wa katiba.
Lakini pia siku za Karibuni Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amenukuliwa na Vyombo vya habari akisema hayupo tayari kuona Zitto anarejeshewa vyeo Ili hali Zitto amekata rufaa Baraza kuu la chama(Chombo cha juu kabisa cha Maamuzi) na akishinda vyeo anarudishiwa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :