UHURU WA KUPENDA NA KUPENDWA UNAVYOATHIRI PENDO HURIA

Posted in
No comments
Friday, March 14, 2014 By danielmjema.blogspot.com



Uhuru wa kupenda au kupendwa ni moja ya haki binadamu ambayo kama zilivyo haki yoyote ile inatakiwa iheshimiwe kwa sababu kila mmoja ana haki ya kuoensha hisia zake katika kile ambacho moyo wake unaouhusudu.

Uhuru huu wakati mwengine hutafsiriwa kutokana na Dini, kabila au utamaduni wa jamii kwa mujibu wa sheria za nchi au eneo husika.

Kuna kitu upendo na kuna kitu uhuru, uhuru kidunia ni uwezo wa kufanya utakacho, utakavyo, utakapo na kwa umtakaye, lakini ifahamike kuwa falsafa inatukumbusha kuwa endapo mtu atakuwa na uhuru wa kufanya kitu vilevile anakuwa na uhuru wa kutokifanya.

Miktadha ni mingi maana katika kupenda kuna kupenda kitu, gari na uturi au kumpenda mtu mfano mapenzi kati ya wazazi na wana wao au ndugu lakini pia kuna mapenzi ya yaliyozoeleka kama muhibu, nyonda, mpenz, laazizi, kichuna, uyuni ambao tunakesha kila siku kuwatungia mashairi na kuwasifu katika nyimbo.

Lakini katika kujivunia uwepo wa mazingira yoyote yale ya haki ya kupenda au kupendwa, Uhuru na pendo zikichanganyika migogoro, balaa uvunjifu wa amani au hata mauaji huwezi kutokea maana uhuru wa kupenda au kupendwa ni tofauti na pendo huria.

Pendo huria mara nyingi hukwaruzana na uhuru wa kupenda, ni vigumu kufanya kitu kwa sababu kuna uhuru wa kupenda au kupendwa, huwezi kumalimisha mtu kumpenda mtu au kupendwa na mtu tu eti kwa sababu kuna uhuru wa kufanya hivyo, kwa kufanya hivyo kutakuwa na kitu kinaitwa Mapenzi elekezi.

Moja ya matukio kama haya yaliwahi kuripotiwa hapa nchini na hata nchi jirani ya Kenya ambapo katika kijiji cha ngamwa mukurweini, kaunti ya Nyeri kati ya familia ya Geofrey Kibuyi na mke wake.

Katika tukio hilo Jane Wamboi ambaye ni mke wa Kibuyi alifikishwa Hospitalini baada ya kudaiawa kunywa sumu.

Jamii nyingi imejikuta ikitumia uhuru huu kuvunja dhana ya pendo huria, tamaduni nyingi ya kiafrika kwa mfano ni wahanga wa pendo elekezi au pendo shuruti, utamsikia baba akimwambia mwanaye sisi kama wazazi wako tumeridhikana mtu Fulani hivyo wewe unachopaswa kufanya ni kufuata na kutii na sio kuhoji.

Katika mfano kama huu mara nyingi wanawake wamekuwa ni wahanga wakubwa sana, hali hii ni tatizo kubwa ambalo limekuwa likizalisha ndoa zisizokuwa na amani ambapo wahanga wakubwa wamekuwa na wanawake na watoto.

Mwisho.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .