TWANGA PEPETA KUHAMISHIA NGUVU MIKOANI; KUTEMBELEA , MBAMBABAY MKOANI RUVUMA
No comments
Wednesday, March 12, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, akifanya mambo jukwaani katika moja ya maonyesho ya bendi yake.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya The African
Stars, Twanga Pepeta, itakuwa nje ya jiji la Dar es Salaam kwa wiki moja,
kutokana na kuwa na ziara ya kuinadi albamu yao ya Nyumbani ni Nyumbani, katika
mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mbeya kuanzia Machi 26 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehani, alisema kuwa Machi 26
wataanza na shoo katika Ukumbi wa Turbo Hall, uliopo mkoani Njombe, wakati siku
inayofuata watacheza na mashabiki wao Mbamba Bay, katika Ukumbi wa Bay live
Social Hall.
Mwimbaji wa Twanga Pepeta, Kalala Junior, katikati akionyesha umahiri wake wa kucheza na jukwaa katika moja ya maonyesho ya bendi yake.
Alisema Machi 28 bendi
yao itafanya shoo katika Ukumbi wa Serengeti, uliopo mjini Songea, wakati Machi
29 Twanga watatumbuiza City Pub, mjini Mbeya, huku Machi 30, wakifanya shoo
High Class, uliopo mjini Tunduma.
“Hizi ni ziara maalum
kwa ajili ya kwenda kuinadi albamu yetu na bendi yetu kwa ujumla, hivyo naamini
wadau tutakuwa nao bega kwa bega.
“Tunaomba tushirikiane
kwa nguvu mashabiki wetu ambao kwa kiasi kikubwa tumeamua kuwapelekea bendi yao
ili wafurahie burudani za Twanga Pepeta,” alisema.
Kwa kuwa na ziara ya
mikoani, sasa wapenzi wa bendi hiyo watalazimika kusubiri kwa siki moja kabla
ya kuanza tena kuipata burudani ya Twanga Pepeta.
Habari Zingine
- Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu
- Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora
- Guzo mitandaoni: Thamani ya Barua ya Mohammad Ali kwa Mandela
- Wasiwasi DR Congo muhula wa Kabila ukifikia kikomo
- jaydee: hii ndio siri ya kufanya vizuri miaka yote
- Maskini Mr. Nice azushiwa kifo kwenye Social Media
- Jionee jinsi Kuwait walivyoanikiwa kuivuta bahari nchi kavu ili kutengeneza mji mpya
- GK KUIBUKA NA VANESSA MDEE JUMATATU HII
- KWEINGOMA WAAHIDI UHONDO WA NGOMA YA SELO TAMASHA LA HANDENI KWETU 2014
- DIAMOND AWA BALOZI WA "MZIIKI"
- TABORA WAMKATAA NUH MZIWANDA; WASEMA HAWEZI KUWA SHEMEJI YAO
- SHABIKI WA SKYLIGHT BAND AWADATISHA JONIKO FLOWER NA ANETH KUSHABA KWA KUCHEZA MA-STYLE YA BENDI HIYO BILA KUKOSEA!
- RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
- New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao
- Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :