HAFLA FUPI YA UZINDUZI WA KAMATI YA NDOA YA MDAU PAULO GEORGE MAILE ILIYOFANYIKA FEBRUARI 8, KATIKA HOTELI YA KILIMANJARO CRANES, MJINI MOSHI MKOANI KILIMANJARO

Posted in
No comments
Tuesday, March 11, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Kamati ikatambulishwa Rasmi
Wanakamati ya harusi ya mdau wa kijiwe chetu Blog, Paulo George Maile wakiongozwa na Mwenyekiti, Tito Haule (katikati) muda mfupi baada ya kuteuliwa katika hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Cranes iliyoko mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
mmoja wa rafiki wa Familia ya ndugu Paulo Maile nao walifika, aliyekaa kulia kwake ni mke wake kipenzi
Bibi Harusi mtarajiwa, Mrs. Maile (kulia) akiwa na ndugu jamaa na marafiki katika hafla ya uzinduzi wa kamati ya harusi yao.
MC-Tito akiongoza zoezi la mchango
Mwakilishi wa Familia ya Muoaji ndugu Paulo George Maile katika hafla hiyo
Mhhhh nini tena?....zoezi linaendelea
Mimi kama ndugu wa karibu nitamsindikiza ndugu yetu Paulo Maile kwa Laki tatu, moja na nusu keshi na nyingine ahadi...hahahaha ndio mambo hayo
Mnuso kidogo hapo basi mambo yakakaa sawa

Mambo ya Vyuku

Bwana Paulo George Maile akipata Vyuku baada ya kuridhika na kamati itakayomsindikiza kufanikisha lengo lake

Gambe kila meza...

Sehemu ya ndugu jamaa na marafiki waliojitokeza katika hafla fupi ya uzinduzi wa Kamati ya Harusi ya bwana Paulo George Maile ambaye ni mdau mkubwa wa blog ya Kijiwe chetu...hongera kaka

Nasi tulikuwepo

Bwana Paulo Maile (kushoto) katika meza moja na baadhi ya marafiki zake kutoka mkoani Arusha na Simanjiro, Mererani-Manyara

Laki moja leo nyingine ahadi...chezea

George Gadiel Kadori, Rajabu Msangi na Mdogo wao katika hafla ya kumsindikiza kaka yao, bwana Paulo Maile

Hapa ni mwendo wa Keshi tu, fedha zipo matumizi kichwa kinauma!!

Tulitokelezea...hatari

Mwanakamati Zakayo David Salmini (aliyesimama) ambaye alichaguliwa kushika nafasi ya kaimu mtunza hazina akihakikisha mahesabu yanakwenda sawa

Marafiki zake kutoka Simanjiro, Mererani na Arusha wakitoa michango yao hapa ni mwendo wa milioni tu!

Kamati ikiendelea na uhakiki

Mtunza Hazina msaidizi, Zakayo David Salmini (kushoto) akipata gambe huku mahesabu yakienda sawa

Toa gambe weka gambe ni mwendo wa vinywaji tu


Vyakula vya kila aina vilikuwepo

Mhudumu akiwahudumia wageni, ndugu jamaa na marafiki walioshiriki uzinduzi wa kamati ya Harusi ya Bwana Paulo George Maile.


Mwanakamati Kassim Msaba, akichangia fedha taslimu Milioni Moja kumsindikiza bwana Paulo Maile

Bwana Paulo Maile akiwataja marafiki zake waliofika katika hafla hiyo kutoa michango yao

Mmasaai, Filia ambaye ni rafiki wa karibu wa bwana Paulo Maile, alitoa fedha taslimu shilingi milioni moja, katikati ni bwana Maile na MC-Tito Sambay.

Vinywaji viliwafuata huko huko walikokaa

Masaai ambaye naye ni rafiki wa karibu wa bwana harusi mtarajiwa, bwana Moses Makeseni


Marafiki waliendelea kutoa michango yao

Mathius Lyatoo (kulia) alitoa keshi shilingi milioni moja, kushoto kwake ni bwana Maile

Mathius na Maile wakikumbatiana kwa furaha

Zakayo David Salmini alitoa  shilingi milioni mbili keshi

Bwana harusi una shilingi ngapi?.....mimi kama mhusika wa shughuli nimejipanga, nina shilingi milioni tatu keshi

Nimetoa jamani mmeziona?????



MC- wa shughuli Tito Sambay naye alichangia kwa kutoa shilingi elfu hamsini, keshi shilingi elfu ishirini na ahadi elfu thelethini

Mwenyekiti wa Kamati Tito Haule alichangia shilingi Laki mbili Keshi
Hii ndio kamati yetu

Kamati hiyooooooooooooooo
MC Tito akiteta jambo na wanakamati
Shemeji wa Bwana Harusi mtarajiwa, ndugu Glory Gadiel Kadori (aliyevaa blusi nyuesi katikati) akiwa na Rafiki yake katika hafla hiyo
Wengine walitumia muda wao kusoma habari magazetini chezea
Ukumbi ulifurika vinywaji kila kona, ndugu jamaa na marafiki.   





























Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .