MAJAMBAZI YAUA KIBORILONI-MOSHI-MKOANI KILIMANJARO

Posted in
No comments
Tuesday, March 11, 2014 By danielmjema.blogspot.com


Majambazi wavamia duka la jumla na kumuua mfanyabiashara maarufu mkoani Kilimanjaro ameuawa kwa kumpiga risasi mbili Kichwani na tumboni kabla ya kutoweka kusikojulikana.

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 2:15 usiku katika maeneo ya Mnazi kata ya Kiboriloni, wilaya ya moshi, mkoani hapa ambapo watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha inayosadikiwa kuwa ni SMG/SAR walimvamia na kumpiga risasi mfanyabiashara, Respiki Eustarck Shirima.

kwa mujibu wa taarifa zilizothibitisha na Kamanda wa polisi mkoani hapo, Robert Boaz, tukio hilo lilitokea juzi machi 10 mwaka huu na kuongeza kwamba majambazi hao walimpiga risasi mbili kabkla ya kutoweka kusikojulikana.

Boaz amesema mpaka sasa haijafahamika kama kuna mali zilizo chukuliwa na majambazi hao na kwamba uchunguzi unaendela ili kubaini chanzo cha mauaji hayo na kuongeza kuwa Jeshi lake limeanza msako mkali kuwasaka majambazi hao.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .