BASI LA HOOD LAPATA AJALI MWANGA; AMEKUFA MMOJA MAJERUHI NI 16
No comments
Tuesday, March 11, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Basi
la Hood linalofanya safari zake kutoka Arusha kwenda Mbeya, namba za usajili
T.488 AXV aiana ya Scania imeata ajali mbaya leo, majira ya saa 3 asubuhi na
kusababisha kifo cha Mtu mmoja na kujeruhi wengine 16.
Ajali
hiyo imetokea katika, barabara ya Same - Mwanga, Kijiji cha Kiverenge wilaya ya
Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo taarifa za awali zinasema kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa tairi ya
mbele.
Kamanda
wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
ambapo amesema katika ajali hiyo alifariki Abiria mmoja aliyemtaja kwa jina la
Joshua Likumbia, Raia wa Kenya, ambaye alikuwa akisafiri kuelekea jijini Mbeya.
Kamanda
Boaz amesema majeruhi katika ajali hiyo ambao ni 16, akiwemo dereva wa Basi, Fadhili
Hashim wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Same na Hospitali ya Rufaa mkoani
Kilimanjaro, KCMC.
Kamanda
Boaz ameendelea kufafanua kuwa majeruhi hao nane wamelazwa Same huku wengine 8
wakikimbizwa mjini Moshi katika hospitali ya KCMC kutokana na hali zao kuwa
mbaya ambapo watatu kati yao wakia wamelazwa katika chumba cha wagonjwa
mahututi.
Habari Zingine
- IS yauwa wanajeshi 32 wa Libya
- Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete alivyoongoza mazisi ya mtoto wa Mdau, Issa Muhiddin Michuzi
- UPDATES ZA MSIBA WA MTOTO WA ANKAL: MWILI UMESHAWASILI DAR ES SALAAM, MAZISHI LEO JUMAMOSI SAA 10 ALASIRI MAKABURI YA KISUTU
- Ndege ya KoreanAir yawaka moto muda mfupi baada ya kutoka Korea Airport
- Mabaki ya ndege ya EgyptAir yapatikana
- TUNDAMAN ANUSURIKA KIFO AJALINI HUKO IDETELO
- WATU 100 WAHOFIWA KUTEKETEA KATIKA HEKALU LA WAHINDU, WENGINE 150 WAMEJERUHIWA
- MAFURIKO YAATHIRI DARAJA LA KIKULETWA WILAYANI HAI
- WENGI WAJITOKEZA KWENYE MSIBA WA MPOKI BUKUKU TABATA, JIJINI DAR ES SALAAM
- Jivu la mwili wa Fidel Castro lazikwa Santiago Brazil
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :