Showing posts with label Burudani. Show all posts
Showing posts with label Burudani. Show all posts

RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY

RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY


​

Rapper maarufu wa nchini Cameroon, Atanga Schneider Ngomah maarufu kama Ngoma, ameachia video ya wimbo wake mpya, All Les Day. All Les Day ina maana ya ‘Kila Siku.’ Ukitayarishwa na producer wake wa miaka mingi, Dijay Karl, huu ni wimbo wenye mahadhi ya Hip hop na Trap iliyonakishwa na mitindo asili ya uchanaji katika viunga vya mitaa maarufu ya Cameroon.
Pia ina vionjo vya mtindo wa Jwe’te ambao ni mchanganyiko wa muziki wa asili wa kabila la Ngemba ambavyo vinasikika kwa mara ya kwanza kwenye wimbo. Amesema vionjo hivyo vitasikika zaidi kwenye nyimbo zake zijazo.  Pamoja na kutumia Pidgin English (Kiingereza kizungumzwacho Cameroon), Ngoma ametumia Kifaransa pamoja na kabila na Ngemba kwenye wimbo huu. Video yake imeongozwa na Shamak Allharamaji.
Ngoma si mgeni kwenye masikio na macho ya mashabiki wa muziki wa Tanzania. Mwaka jana akiwa na wimbo wake maarufu, Mangosi, alifanya ziara ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika vituo vya redio na TV vikiwemo Clouds TV, East Africa Radio, EFM, Times FM na Magic FM.
Katika ziara yake hiyo, Ngoma alifanikiwa kurekodi collabo na Ray Vanny katika studio za Surprise Music chini ya producer Rash Doni, huku mdundo na ukamilishaji wa wimbo ukifanywa na Dijay Karl. Amepanga kuachia wimbo huo mapema mwakani wakati wa shamrashamra za Kombe la Mataifa ya Afrika.  Pia Ngoma amesema baada ya kuachia video takriban nne, ataachia album yake inayosubiriwa kwa hamu, G.O.AT. (Greatest of All Time).

New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao

New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Wimbo mpya wa msanii Lady JayDee, unaitwa “Sawa na Wao”. Staa huyo ambaye hivi karibuni alitangaza ujio wake mpya, alioupa jina la Naamka tena kwa kutoa wimbo wa 'Ndi Ndi Ndi' amesema wazo la wimbo ‘Sawa na Wao’ ambao ameuachia hivi karibuni alilipata kutokana na maisha ya watu wake wa karibu ambao amekuwa akiishi nao katika maisha ya kila siku.

Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi

Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Muimbaji wa Marekani na mshindi wa tuzo za Grammy, Madonna, yupo nchini Kenya alikoenda kutembelea makazi duni ya Kibera yaliyopo jijini Nairobi.


Muimbaji huyo ni muasisi wa taasisi ya Raising Malawi na balozi mwema wa Child Welfare nchini Kenya. Madonna anayekadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni 800 ametumia muda wake kuzungumza na wakazi wa makazi hayo ya Kibera. Ameshare picha kadhaa za kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa kwenye makazi hayo maarufu.
“Hugging Mama Sopfie. This Amazing Woman lives in a 10 by 10 dwelling in Kibera with her 14 children-2 adopted. Her husband killed in a political uprising. She’s starting her own business with the help of @shofco. God Bless Her,” ameandika Madonna kwenye picha moja.

Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu

Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Staa wa Bongo fleva, Timbulo amepinga taarifa zilizoenea kuwa amerudi kwenye kazi ya ualimu ambayo siku zote amekuwa akisema ndiyo kazi bora kwake.


Akiongea na Bongo5, Timbulo amesema kuwa ‘sijawahi kusema nimerudi kwenye kazi ya ualimu hayo yote ni maneno ambayo yamekuwa yanatembea mtaani.’
“Siku zote nimekuwa nikisema kuwa kazi ya ualimu ni kazi yenye respect kubwa mimi nasema tofauti na kazi hii ninayoifanya ambayo respect yake ni ndogo sana,” alisema Timbulo.
“Huku unakuwa maarufu lakini ukienda kwa watu wenye heshima bado wanakuona ni mtu mhuni tu. Lakini nimekuwa nikisema kuna siku nitarudi huko,” aliongeza.

Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora

Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mamia ya vijana walijitokeza katika usaili wa mashindano ya Maisha Plus mwishoni mwa wiki ili kufanya usaili wa mashindano hayo kwa msimu wa tano.
677A0281
677A0696 
Mashindano hayo yalifanyika katika kijiji cha Makumbusho Kijitonyama jijini Dar es salaam ambapo vijana waliojitokeza waliulizwa maswali mbalimbali ikiwemo mtazamo wao juu ya mwenendo wa kiuchumi ndani na nje ya Tanzania, afya, kilimo, ufugaji na mengine.
Vijana waliofanyiwa usaili walitoka mkoa wa Dar es salaam pamoja na mikoa ya jirani ikiwemo Pwani.
"Maswali yetu huwa hayana utaratibu, wala sio maswali ambayo mshiriki anaweza kujiandaa. Mengi huwa yanakusudia kupima uelewa wa mshiriki juu ya maswala mbalimbali ya kidunia na namna anavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali." Alisema Masoud Kipanya, Jaji na mwanzilishi wa mashindano ya Maisha Plus.
677A0614
Akitaja vigezo vya kushiriki Maisha Plus, Kaka Bonda, miongoni mwa majaji na waanzilishi wa Maisha Plus alisema, "Tunachukua washiriki wenye umri wa miaka 18 hadi 26, walio na elimu na ambao hawajasoma kabisa, wawe raia kutoka nchi za Afrika Mashariki"
677A0389
677A0646
677A0422
Maisha Plus kwa mwaka huu wa 2016 inatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi tano ambazo ni Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania ambapo mshindi atafadhiliwa wazo la biashara lenye thamani ya fedha ya kitanzania Milioni 30. Kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka huu ni 'Vijana Ndio Ngazi'.
677A0857
677A0262
677A0763
Usaili unaendelea katika mikoa mingine na nchi nyingine nje ya Tanzania. Vijana wametakiwa kusikiliza matangazo ya ratiba kupitia redio mbalimbali katika nchi shiriki, runinga ya Azam Two, mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na tovuti maalum ya mashindano hayo ya www.maishaplus.tv.

Diamond yuko mbioni kufanya ngoma na Psquare

Diamond yuko mbioni kufanya ngoma na Psquare

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com


Mkali wa muziki wa Bongoflava na Afro Pop, Diamond Platnum ‘Simba’ ameanza kunguruma katika mitandao ya kijamii kuashirikia kujipanga kuachia ngoma yake mpya ambayo amewashirikisha wasanii wa kundi la P Square kutoka nchini Nigeria.


Muimbaji huyo hajaweka wazi ni lini kazi hiyo inatoka lakini kuna kila dalili kuwa kazi hiyo inaweza kutoka muda wowote.
Kupitia instagram, Diamond ameandika:
My People!!!!!!!!! Subscribe to my Youtube Channel now so that you can be the first one to watch the HIT from SIMBA ft P-SQUARE!!!! (Najua unakiu kias gani….haya Jiunge na Channel yangu ya YOUTUBE sasa ili uwe mtu wa kwanza kushuhudia Mshine yangu Mpya Nilowashirikisha P-SQUARE! ) Cc @peterpsquare @rudeboypsquare #SimbaKaseMa
Kitendo cha Diamond kupost picha hiyo na kuandika maneno hayo kumeibua hisia mbalimbali zenye furaha kwa mashabiki wake ambo wengi wameonyesha kuwa na furaha na wakitabiri kuwa huenda ikawa kazi kubwa kutokana na jinsi wanavyomuamini msanii wao na kusema kuwa hajawahi kuwaangusha. Haya ni maoni ya mashabiki kuhusu kazi hiyo.


baba_kai10karibu
Sana na tunaisubili kwa hamu sana wewe huwaga hukosei fundi na wala huwaga hutungi bifu na fulani ili ikupe kiki. weldone Chibu DANGOTE

miraji2441

Kabla ata haijatoka viuws 2mil we Simba umeshndkanaaaaaa aiseeeeeee

Shubi_ruby@shadilicious2015

Bado haijatolewa ndio maana kasema subscribe now, ili akiitoa utaweza kujua ipo ukaangalia. Na ukiweka notifications on basi utapata hapo hapo sekunde hiyo na kubonyeza kuiangalia kwa raha zako

cathbertkweka_depay

Simba akiunguruma msituni wanyama wote kmyaaaa @diamondplatnumz
mbarakamsalum
Very good simba keep fighting and moving fowrd.

Wema Sepetu: Kurudiana na Diamond? hapana

Wema Sepetu: Kurudiana na Diamond? hapana

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Vunja ukimya! Tetesi zinazogonga vichwa vya mashabiki wa mastaa wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ zimepata ufumbuzi baada ya mlimbwende huyo kuanika ukweli wa ‘ubuyu’ huo.

KABLA YA MAHOJIANO
Kabla ya Wema kufunguka mambo mazito juu ya Diamond, uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, sababu hasa za mashabiki wa wawili hao kuhisi penzi lao limefufuka chini kwa chini ni baada ya Wema kuanza kuwahimiza watu kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, wampigie kura Diamond ambaye anawania Tuzo za BET kwenye kipengele cha Best International Act: Africa, zitakazofanyika nchini Marekani hivi karibuni.
wema na Mond
JIUNGE NA WEMA
Wikienda: Mashabiki wako wapo kwenye sintofahamu ya tetesi za wewe kurudiana na Diamond. Je, ukweli ni upi?
Wema: (kicheko cha kukata na shoka hadi machozi) hivi kwa nini kila ninapokutana na mtu lazima aniulize kuhusu mimi kurudiana na Nasibu (Diamond)?
Wikienda: Sasa hapo ndiyo ujue lisemwalo lipo na kama halipo laja, hebu eleza hili likoje?
Wema: Kwanza kabisa mimi sasa hivi nimekua. Utoto nimeuweka kando, sihitaji tena bifu zisizokuwa na maana na hata ukiangalia ni kitu gani tulichogombania, hakuna hivyo kuna wakati unafika lazima mtu ubadilike kabisa tena kwa kipindi kama hiki cha mwezi mtukufu.
Wikienda: Kuna mtu yeyote alikushauri kuanza kuposti watu wajitoe kumpigia kura Diamond?
Wema: Hakuna, mimi niliongozwa na hisia zangu kwa sababu hata hivyo sipendi kupelekeshwa na hisia za watu au watu wanasema nini, inatakiwa ifike kipindi nifanye vile moyo na akili yangu inavyotaka.
Wikienda: Unajua kuna kitu kinaitwa timu, yaani kati yako na Diamond. Vipi kwa upande wako hawajakujia juu kuhusu kuwataka mashabiki wampigie kura Diamond kwa sababu mara nyingi timu zenu huwa zinatukanana?
diamond-na-wema
Wema: Kwanza hilo ndilo nataka kuliweka wazi, sasa hivi sitaki kuendesha maisha yangu kupitia timu kwa sababu mwisho wa siku mimi nina maisha yangu na wao wana maisha yao, yaani mpaka vitu vingine vinakera kwa sababu mtu unatakiwa kufanya kitu kinachotoka ndani ya moyo wako siyo kusikiliza watu wanataka nini.
Wikienda: Kwa hiyo unaona timu ndizo zinachochea ugomvi wenu?
Wema: Kabisa kwa sababu inatokea wakati anatukanwa Diamond, mtoto wake (Tiffah) na mkewe (Zari) kiukweli naomba kusema wazi mimi sipendi na mara nyingi naonekana kama mimi nimewatuma. Aisee sipendi kabisa hali hiyo na ninaomba timu zipunguze kutukana watu siyo vizuri.

Wikienda: Unafikiri timu imekusababishia matatizo?

Wema: Siyo kwangu tu hata kwa Diamond. Hatuishi maisha ya kwetu, tunafuatisha timu. Labda niseme kwamba mimi ni shabiki namba moja wa nyimbo za Diamond lakini kiukweli hata ukitaka kuimba wimbo unajificha yaani maisha hayo sitaki tena kwa sababu hata nje ya uhusiano wa kimapenzi tuliokuwa nao huko nyuma  mimi ni shabiki mkubwa wa nyimbo zake, sasa kwa nini nibane hisia za kitu nikipendacho?

Wikienda: Kwa hiyo kinyongo ulichokuwa nacho nyuma sasa hivi huna tena?
Wema: Yaani mimi nimesafisha nia kabisa, sina tatizo na yeye kwa sababu najua inawezekana hata yeye anatamani kuniuliza kitu inashindikana au anahitaji kufanya kazi na mimi inakuwa ngumu kitu ambacho ni mambo ya kizamani kabisa.
wema & Dai
Wikienda: Mara ya mwisho kuwasiliana na Diamond ni lini?
Wema: Niliwasiliana na Diamond tena kwa kumtumia meseji kipindi f’lani mama yake alikuwa anaumwa. Kiukweli kama mapenzi yalikwisha zamani sana. Yeye akaendelea na maisha mengine na mimi hivyohivyo.

Wikienda: Ukipata nafasi ya kukutana naye ili mfanye kitu kwa ajili ya mashabiki wenu inawezekana?
Wema: Kama nilivyosema awali, kwa upande wangu mimi sina tatizo lakini najua kabisa kuna vitu Diamond anavifanya vibaya kwangu ili kunizibia sehemu f’lanif’lakini sasa hiyo inanionesha nini kwa Diamond? Amekuwa kimuziki lakini siyo yeye mwenyewe, kuna kipindi namuonea huruma sana kwa mambo yake, natamani hata nimwite tukae chini na kumwambia kuwa yeye ni wa kimataifa hivyo mambo ya Kiswahili hayana nafasi tena kwake.
Wikienda: Kwa hiyo mtu akiwakutanisha mzungumze upo tayari?
Wema: Bila tatizo lolote, mambo ya matashititi hayahitajiki kwa sasa na hayana nafasi kwani imefika kipindi watu tumekua na maisha yanaendelea kwa sababu siwezi kumfikiria tena kimapenzi.
Katika mahojiano hayo, Wema alidai kwamba kuna mambo mengi ambayo Diamond amekuwa akimfanyia umafia hivyo tetesi kuwa amerudiana naye hazina ukweli wowote na kwamba haitatokea.
wema-na-diamond
DIAMOND ATAFUTWA
Jitihada za kumpata Diamond ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, kutumiwa ujumbe bila kujibu na kufuatwa ofisini ambako hakuwepo hivyo jitihada zinaendelea.
TUJIKUMBUSHE
Wema na Diamond ni wapenzi waliokuwa gumzo miaka miwili iliyopita kutokana na kuachana na kurudiana hivyo mashabiki wao wamekuwa wakiamini ipo siku watarudiana.

GPL

Mambo 9 ya Ray C baada ya kuchukuliwa na Polisi

Mambo 9 ya Ray C baada ya kuchukuliwa na Polisi

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Usiku wa June 16 kuamkia June 17 kuna video ya mwimbaji wa Bongofleva Ray Cilisambaa mitandaoni na kila mmoja kuzungumza habari tofauti kuhusu clip video hiyo, wapo waliosema Ray C kapata kichaa na mambo mengine mengi tu, nakusogezea mambo 9 ya kufahamu kuhusu Ray C baada ya kusambaa kwa video clip na yeye kuchuliwa na Polisi.
1- Polisi wamesema hawakumkamata Ray C bali walimpeleka hospitali kupatiwa matibabu
2- Ray C amepimwa hospitali wala hana kichaa ni mzima ana akili timamu.
3- Mkurugenzi wa uzalishaji na utafiti Clouds Media Ruge Mutahaba amethibitisha kuwa June 17 Ray amepelekwa Rehab Bagamoyo.
4- Rehab aliyopelekwa Ray C ni Bagamoyo mkoa wa Pwani, Rehab ambayo aliwahi kuishi Chid Benz wiki tano zilizopita.

Mengine zaidi ingia...

Ommy Dimpoz afagilia Ndoa ya Mwana FA

Ommy Dimpoz afagilia Ndoa ya Mwana FA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Ndoa ya Mwana FA haikuwa ya kifahari lakini ilikuwa bora, yenye furaha na iliyochangamka kuliko nyingi alizowahi kuhudhuria Ommy Dimpoz. Akizungumza kwenye documentary yangu maalum niliyoipa jina ‘Bado Nipo Nipo ilivyogeuka kuwa historia kwa Mwana FA’, Ommy amedai kujifunza mengi kupitia ndoa ya swahiba wake huyo.


FA alifunga ndoa June 5, 2016 na mchumba wake wa miaka mingi ambaye tayari pamoja wana mtoto wa kike aitwaye Maleeka. “Watu wengi wanaogopa kuoa kwasababu ya kufikiria gharama, naweza kusema kwamba ndoa ya Mwana FA haikuwa ndoa yenye mambo ya kifahari lakini ilikuwa moja ya ndoa nzuri kabisa nilizowahi kuhudhuria,” anasema Ommy.
“Haikuwa na mambo mengi kwa maana ya magharama, tumetoka msikitini tumeenda moja kwa moja nyumbani kwake. Baada ya hapo nyumbani kulikuwa tu na kasherehe kadogo tumekusanyika washkaji, kama house party. Ukiangalia kwasababu ilikuwa ndoa ya staa ikawa kubwa,” ameongeza.
Ommy pia amedai kuwa FA alikuwa amepanga kuifanya ndoa itakayohusisha watu wachache sana na ya faragha. “Mwenyewe alitaka kwamba harusi iwe ni ya watu wasiozidi kumi,” anasema.
“Hakutaka watu watu wajue kabisa. Tulikubaliana kwamba hakutakuwa na picha hata moja. Kwahiyo mimi nilikuwa nahisi naenda kwenye harusi ambayo sitapost chochote. Lakini nafika msikitini naona watu wako busy wanaorekodi Snapchat… nikaona hapa hamna siri na mimi nikaanza kurekodi hapo hapo nikaanza kuzirusha.” “Baada ya hapo unajua tena ndoa jambo la heri, sio jambo la siri.”

Bongo5

Ibaki Story imeandikwa na mwandishi wa Moyo Mashine ya Ben Pol? Haya ni majibu ya Rich Mavoko

Ibaki Story imeandikwa na mwandishi wa Moyo Mashine ya Ben Pol? Haya ni majibu ya Rich Mavoko

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
So mtaani kuna tetesi kuwa hit mpya ya Rich Mavoko imeandikwa na mwandishi wa wimbo wa Ben Pol ‘Moyo Mashine’, Lollypop. Mavoko amezijibu tetesi hizo kupitia 255 ya XXL kupitia Clouds FM na kudai kuwa ni kweli mwandishi huyo amehusika lakini si kama inavyosemwa na si kweli kwamba amekausha kutoa credits.

Mayweather atumia $37m kununua ndege binafsi ya pili

Mayweather atumia $37m kununua ndege binafsi ya pili

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Aliyekuwa bingwa wa ngumi kwa uzito wa kati Floyd Myweather amenunua ndege binafsi nyingine iliyomgharimu zaidi ya dola milioni 37.
Mtu wa karibu wa Mayweather ameiambia TMZ, “It’s a 12 passenger Gulfstream III with gold cup holders, gold sink, gold accents throughout. It has all white leather seats and a fully stocked kitchen. He now has two jets.
“Air Mayweather 1 and 2,” aliongeza.
Mayweather amekuwa akitumia fedha nyingi kununua vitu vya gharama tangu alipotangaza kustaafu ngumi mwaka jana.

Happy Birthday Lady Jaydee: Yafahamu maisha yake ya utoto hadi kuja kuwa staa

Happy Birthday Lady Jaydee: Yafahamu maisha yake ya utoto hadi kuja kuwa staa

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Lady Jaydee alizaliwa tarehe kama ya leo. Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, tunakupa fursa ya kumfahamu zaidi muimbaji huyo nguli kuanzia enzi zake za utoto hadi amekuja kuwa muimbaji mahiri barani Afrika akiwa na album sita hadi sasa.
May mwaka jana nilikutana naye kwa mara ya kwanza na kumfanyia interview ndefu.“Sisi kwetu tumezaliwa watoto kumi,” alisema Jaydee. “Lakini bahati mbaya watatu wamefariki na tumebakia saba. Familia yetu ni familia ya dini, tumezaliwa kwenye maadili ya kisabato, tumekulia kanisani na nidhamu.”
“Nilikuwa naimba kwaya kanisani, nilishiriki pia kwenye vikundi vya Pathfinder kanisani kwetu tangu nina miaka saba yaani nilikuwa naweza nikasimama mbele ya kanisa nikaongoza watu, nikaimbisha watu wakaimba. Unajua ukiwa mdogo huwezi ukajua kama ni kipaji, mimi nikawa naona ni kitu tu ambacho napenda, kwahiyo nikawa nafanya tu for fun.”
Jaydee anasema alikuwa ni mtoto msikivu na aliyekuwa akifuata kile alichokuwa akielekezwa na wakubwa zake. “Muda mwingi nilikuwa nautumia kanisani zaidi, kwahiyo ilikuwa ni shule, kanisani,” anakumbuka.
Anasema tangu alipojitambua, muziki kilikuwa ni kitu alichopenda kuja kukifanya kama kazi yake. “Nilikuwa napenda kuwaangalia watu ambao wanaimba na kujiweka kwenye viatu vyao na kujifikiria vipi mimi nikiwa kama yule, sikuwa najiona mtu mwingine zaidi ya mwanamuziki.”

Lady Jaydee alizaliwa mkoani Shinyanga hadi darasa la nne kabla ya kuhamia jijini Dar es Salaam. Akiwa Dar es Salaam, pamoja na kuwa na ndoto ya kuja kuwa mwanamuziki, alijikuta katika wakati mmoja akifanya kazi kama mtangazaji wa redio.
“Saa zingine nilikuwa najaribu kutangaza TV kwahiyo nakaa kwenye kioo najiangalia najaribu kuona kama naweza kuwa presenter. Kwahivyo nikasema ngoja nikajaribu kuomba labda kwenye redio pia nione kama ntaweza, lakini mwenyewe binafsi siamini kama ni mtangazaji. Ila nafikiri nilikuwa naenda kwasababu napenda muziki na naona ndio sehemu ambayo naweza nikakutana na watu ambao tunaweza tukafanya masuala hayo ya muziki na vitu kama hivyo.”
“Nilifanya ile kazi lakini sio kwamba nilikuwa naipenda sana kwasababu sio passion yangu. Baadaye nilipoweza kufanya muziki nikaona siwezi kuendelea na kitu ambacho hakipo kwenye moyo wangu, nikaona nifanye muziki na niache kutangaza.”
Wimbo wa kwanza Lady Jaydee kurekodi uliitwa ‘Sema Unachotaka’ aliourekodi kwenye studio za Master J baada ya kushinda shindano lililoandaliwa na Radio One Stereo. Wimbo huo uliwekwa kwenye album iitwayo Asubuhi iliyokuwa na nyimbo za wasanii wengine pia. 
Album yake ya kwanza ilikuwa ni Machozi iliyokuwa na nyimbo nyingi za huzuni na kuumizwa japo anasema hiyo haikuashiria kuwa hayo ndio yalikuwa maisha yake. Kabla ya kuwa na jina, Jaydee alikuwa akirap na Dr. Dre ambaye hadi leo ni role model wake, alikuwa mmoja wasanii aliokuwa akiwasikiliza sana. Ndoto yake hadi leo ni kuja kurekodi na producer huyo.
“Siku zote tu nimekuwa nikiwish tu kwamba labda kama angeweza kunitengenezea hata wimbo mmoja,” anasema Jaydee. Maisha ya umaarufu yamekuwa na changamoto nyingi kwake ikiwemo kujizuia kufanya mambo anayoyapenda ambayo kama asingekuwa staa angeyafurahia kuyafanya. 
“Watu wanashindwa kuelewa kwamba mimi ni Jaydee sawa lakini mimi ni Judith na ni binadamu wa kawaida.” anasisitiza. “Naweza kukasirika, naweza kucheka, naweza kulia, naumia kama mtu mwingine anavyoumia. Lakini wao wanavyochukulia ni kwamba unavyokuwa pale wanapokuwa wameshakufahamu, hutakiwi vitu vingine kufanya kwahiyo unakuwa saa zingine hauko huru sana. 
Labda mtu amekuja amekuchokoza inabidi umwache tu hauwezi kumrudishia wakati katika hali ya kawaida mtu yeyote anaweza kufight back. Na mimi ni mgomvi sana na huwa sipendi kuonewa, saa zingine unaweza kukuta mtu akakufanyia kitu lakini ukakaa tu kimya, huyo sio mimi lakini inabidi tu nifanye hivyo.” Happy Birthday Lady Jaydee.

Professor Jay atembelea ‘WCB’ ya Diamond, afurahishwa na uwekezaji uliofanywa

Professor Jay atembelea ‘WCB’ ya Diamond, afurahishwa na uwekezaji uliofanywa

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Rais wa WCB, Diamond Platnumz akiwa na Mbunge wa Mikumi, Professor Jay
Mbunge wa Mikumi ambaye ni msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Joseph Haule ‘Professor Jay’ Jumatatu hii alitembelea ofisi za WCB na kujionea uwekezaji uliofanywa na rais wa label hiyo Diamond Platunmz.


Babu Tale akiwa na Professor Jay
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Professor Jay amemsifia Diamond kwa uwekezaji aliyoufanya.
“Kikubwa kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza Diamond kwa kuwa na mawazo mapana zaidi kwa sababu kiukweli kwa wasanii wengi wa Tanzania na Waafrika wengi tunaweza tukawa na kipaji lakini mazingira yetu ya kazi yanakuwa magumu,” alisema Professor.
Professor Jay akiwa na Dogo Janja
Aliongeza, “Kwa mfano pale kwa Daimond jana nimeenda nimekuta kuna studio hapo hapo, pamoja na kurecord lakini pia anachumba ambacho amekitengeneza cha kutengeneza photoshoot. Lakini pia ana sehemu ya kufanya editing ya kazi zake na ana watu special ambao amewaajiri kwa ajili ya kazi hizo, hii ni hatua kubwa sana kwa msanii,”
Professor Jay na Raymond

Mo Music: Sihitaji Menejimenti kwa sasa

Mo Music: Sihitaji Menejimenti kwa sasa

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Baada ya kuachana na menejimenti yake, Mo Music amesema kwa sasa anataka kujisimamia mwenyewe kwanza bila menejimenti.


Hivi karibuni Mo Music alivunja mkataba na menejimenti yake iliyokuwa ikisimamia kazi zake kwa madai kuwa wameenda nje ya mkataba wao huku uongozi huo ukidai kuwa yeye ndiye aliyezingua kwenye mkataba wao.
Akiongea na Bongo5, Mo Music amesema kuwa ‘kwa sasa nataka kujisimamia mwenyewe sitaki menejimenti.’
“Mimi nimeona bora nijisimamie kwa muda kwanza, kwa sababu niweke mambo yangu sawa hata kama nikiamua kuchukua menejimenti nijue ipi inanifaa zaidi sitaki kukurupuka. Menejimenti nazozihesabu kama kubwa nne zimenifuata lakini kuna nyingine zinataka zianze kuja,” alisema.
Aidha Mo Music ameongeza kuwa atakuwa makini kuangalia menejimenti nzuri yenye uzoefu na muziki ili yasijitokeze kama yaliyotokea kwenye menejimenti yake ya mwanzo.

Nahreel afunguka kuhusu Beat ya 'Arosto'

Nahreel afunguka kuhusu Beat ya 'Arosto'

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Baada ya taarifa kusambaa kuwa beat ya wimbo wa G-Nako ‘Arosto’ ilikuwa ya mtayarishaji wa muziki Bongo Fleva, Nahreel na ilipotea baada ya kusahau external yake kwenye studio za Switch Records, mwenyewe amesema kuwa hana uhakika kama ilikuwa yake au lah.

Hadi muda huu inafamika kuwa beat ya wimbo huo imetayarishwa na Luffa kutoka studio za Switch Records zinazomilikiwa na Quick Rocka. Nahreel aliwahi kufanya kazi kwenye studio hizo kabla ya kuanzisha The Industry.
Akiongea na Bongo5, Nahreel amesema kuwa hataki kuthibitisha hilo kama beat ya ‘Arosto’ ilikuwa yake au lah kwa sababu hana uhakika.
“Kusema ukweli kwa sasa siwezi kuthibitisha hilo ile external niliyoiacha pale Switch ilikuwa na beat nyingi sana kama 600. Nimekuwa nikitengeneza beat nyingi sana mpaka niende nikahakiki ndiyo nitajua. Kusema ukweli external yangu iko pale, nikisema hivyo nitakuwa natengeneza kitu ambacho siyo kizuri,” alisema Nahreel.
Hata hivyo Nahreel ameongeza kuwa beat hiyo haiwezi kuwa ya kwake kama ingekuwa hivyo angeifahamu mapema.

Linah: Ninatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama za Darassa

Linah: Ninatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama za Darassa

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Linah amesema anatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama za rapa mkali kutoka Bongo, Darassa. Muimbaji huyo amesema kwa jinsi ambavyo amewahi kukaa na Darassa na kumsikia akiongea kwa muda mfupi, alibaini kuwa anaweza kuwa baba mzuri.

“Ni mtu ambaye ana sifa zote za kuweza kuwa mwanaume ambaye namtaka. Namchukulia kama kaka yangu yaani sijawahi kumfeel kimapenzi lakini nimekaa naye kwa muda mfupi, nimemuona ni mtu fulani mwenye busara. Ni mwanaume ambaye nikimuona nasema ‘this guy, I wish ningekuwa nina hisia za kimapenzi naye. Katika wasanii wote I wish my boyfriend angekuwa hivi,” Linah ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.
Ameongeza kuwa Darassa anajua kuwa anakumbali na rapper huyo pia anamkubali Linah na ukaribu wao ni wa kama kaka na dada tu.

Msikilize Ben Pol kuhusu hatua ya WCB kumsaini Rich Mavoko

Msikilize Ben Pol kuhusu hatua ya WCB kumsaini Rich Mavoko

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mkali wa wimbo ‘Moyo Mashine’, Ben Pol amefunguka na kuzungumzia hatua ya Diamond Platnumz kumsani msanii mkubwa kama Rich Mavoko katika label yake WCB.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Ben Pol amesema hatua ya Diamond kuamua kumsaini Rich Mavoko katika label ya WCB, itafungua njia kwa wasanii wengine kuwa na moyo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.
“Ni vizuri sisi kwa sisi tukaaminiana na kufanya kolabo kwenye kazi,” alisema Ben Pol. “Diamond ni mpiganaji na Mavoko ni mtu ambaye ana kipaji na mjanja mjanja, kwahiyo muungano wao unaweza kuleta mapinduzi makubwa katika muziki.”
Pia muimbaji huyo amewataka wale wasanii wenye uwezo wa kuwasaidia wenzao wasisite, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuupeleka muziki wa Tanzania mbele zaidi.

Idris Sultan: Nipo tayari kuigiza nimekufa Hollywood lakini siyo kuwa punga

Idris Sultan: Nipo tayari kuigiza nimekufa Hollywood lakini siyo kuwa punga

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mshindi wa shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan amefunguka na kuzungumzia mpango wa kuingia rasmi kwenye tasnia ya uigizaji.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Idris alisema mpango wake mkubwa ni kwenda kuigiza Hollywood na siyo hapa nyumbani.
“Nia yangu ni kuingia kwenye tasnia ya filamu,” alieleza Idris Sultan baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kuingia kwenye tasnia ya filamu.
“Target yangu kubwa ni Hollywood, yaani hata nikiambiwa niende sasa hivi nikaigize nimekufa nitaenda fasta ila kasoro kwenda kuigiza kuwa punga Hollywood, hiyo hapana,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Idris amesema tayari ameshasaini madili ya kuwa balozi wa makampuni kadhaa na baada ya mwezi wa ramadhani atayaweka wazi.
Bongo5

Audio: Yamoto Band ft Ruby~ ‘Suu’

Audio: Yamoto Band ft Ruby~ ‘Suu’

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Baada ya kuwepo kwa story ambayo inamuhusisha kiongozi wa Bendi ya Yamoto Band, Aslay Isihaka 'Aslay' kutoka kimapenzi na mwanadada Ruby, Bendi ya Yamoto imeachia wimbo mpya waliomshirikisha Ruby, inaitwa 'Suu' kazi ikiwa imefanyika chini ya Producer Shirko.
Bonyeza HAPA kudownload na au kusikiliza 

Lady Jay Dee asema haya kuhusu Wasanii kuogopa kufanya naye 'Collabo'

Lady Jay Dee asema haya kuhusu Wasanii kuogopa kufanya naye 'Collabo'

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Kumekuwepo na imani kuwa wasanii wengi wanaogopa kumshirikisha Lady Jaydee kwasababu wanaamini Clouds FM haitoishia tu kutoucheza wimbo huo bali hata zingine zijazo. Clouds FM na Lady Jaydee wana tofauti ambazo hadi sasa hazijamalizika.


Muimbaji huyo wa Ndindindi amefanikiwa kuelezea suala hilo kupitia kituo cha redio cha Nyemo FM cha mjini Dodoma alikoenda kwaajili ya show yake iliyofana ya Naamka Tena Concert.
“Inawezekana pia lakini hawawezi kusema labda moja kwa moja,” Jide alimjibu mtangazaji wa redio hiyo, Winston Makangale.
“Lakini pia sio vizuri umwongelee mtu ambaye hujui mawazo yake yanafikiria nini au pengine unaweza ukaongea hivyo halafu ikawa sio hivyo ukawa umemsingizia,” aliongeza.
“Kwahiyo nafikiri hilo tuwaachie wao kila mmoja atakuwa anajua kwa nafsi yake kama anaweza au hawezi na sababu zipi zinazopelekea aweze na sababu zipi zinazopelekea asiweze. Lakini la msingi kila mmoja afanye muziki wake kwa nafasi yake na watu waweze kuburudika.”
“Mimi sina tatizo na mtu yeyote ambaye atakuwa yupo tayari kufanya kazi na mimi,” Jaydee alijibu baada ya mtangazaji kusema anatamani kusikia collabo yake na Diamond. “Bado hatujakutana na wala hatujawahi kukaa kuzungumzia kuhusiana na collabo.”

Msikilize Lady Jay Dee

Bongo 5

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .