Idris Sultan: Nipo tayari kuigiza nimekufa Hollywood lakini siyo kuwa punga

Posted in
No comments
Tuesday, June 14, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Mshindi wa shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan amefunguka na kuzungumzia mpango wa kuingia rasmi kwenye tasnia ya uigizaji.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Idris alisema mpango wake mkubwa ni kwenda kuigiza Hollywood na siyo hapa nyumbani.
“Nia yangu ni kuingia kwenye tasnia ya filamu,” alieleza Idris Sultan baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kuingia kwenye tasnia ya filamu.
“Target yangu kubwa ni Hollywood, yaani hata nikiambiwa niende sasa hivi nikaigize nimekufa nitaenda fasta ila kasoro kwenda kuigiza kuwa punga Hollywood, hiyo hapana,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Idris amesema tayari ameshasaini madili ya kuwa balozi wa makampuni kadhaa na baada ya mwezi wa ramadhani atayaweka wazi.
Bongo5

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .