Italia walivyoitandika Ubelgiji 2-0

Posted in
No comments
Tuesday, June 14, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Bado michuano ya Euro 2016 inaendelea kama kawaida, usiku wa June 13 ilikuwa zamu ya Italia na Ubelgiji kushuka dimbani kucheza mchezo wao wa kwanza wa Euro 2016.Italia walionekana kuwa imara zaidi ya Ubelgiji baada ya kutumia vyema nafasi zao mbili.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa unapewa nafasi ya kuwa ni mgumu kwa kila timu kupata matokeo, Italia walifanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0 na kuacha kikosi chaUbelgiji kikiwemo na nyota wake kama Eden Hazard wa Chelsea kutoka uwanjani vichwa chini. 
Msimamo wa Kundi E baada ya matokeo ya mechi za leo
Magoli ya Italia yalifungwa na Emmanuele Giaccherini  dakika ya 32 na Graziano Pelledakika ya 90, Ubelgiji wamepoteza mchezo lakini kwa dakika zote 90 walikuwa wanaongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 55 kwa 45 dhidi ya Italia.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .