Familia ya Conjestina kuwashitaki wanaomzushia kifo

Posted in
No comments
Wednesday, May 25, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Kufuatia uvumi uliosambaa katika mitandao ya kijamii, yakidai kuwa Mwanamasumbwi wa zamani wa Kimataifa kutoka Kenya, Conjestina Achieng amefariki dunia, Familia ya Mwanamichezo huyo imetishia kuwashitaki wahusika wote wa uvumi huo.
Kwa mujibu wa kaka wa Bingwa huyo wa zamani wa dunia, William Ochieng, uvumi huo unasambazwa na watu na maadui wa Mwanamasumbwi huyo. William aliwaambia waandishi wa Habari kuwa Mwanamichezo huyo yuko hai na mzima kabisa japo bado anaendelea kujiuguza na kuongeza kuwa wanashuku kuwa baadhi ya watu wenye nia ya kukwapua kiwanja chake kilichopo Nairobi ndio wanaosambaza uvumi huo.
Alisema uvumi huo umesababisha usumbufu mkubwa katika familia yao huku akiongeza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakiipuuzia upuuzi huo lakini kuanzia sasa watachukua hatua kubwa dhidi ya yeyote yule anayehusika.
Aidha Kaka huyo wa Conjestina ameiomba serikali na watu wote wanaomtakia mema mwanamasumbwi huyo kujitokeza na kuwasaidia ili Mwanamichezo huyo 'Hands of Stone' aweze kupata huduma bora ya matibabu.
Conjestina alifanikiwa kuwa mwanamke wa kwanza Mwafrika kutwaa taji la kimataifa alipomtandika Fiona Tugume wa Uganda katika pambano la kuwania ubingwa wa WIBF Middleweight kabla ya kupoteza pambano kimizengwe dhidi ya Ragosina Natascha wa Russia, ubingwa wa WBC na WBA.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .