HATIMAYE! MWANDISHI WA DW ALIYEPOTEA APATIKANA JIJINI DAR ES SALAAM

No comments
Monday, March 21, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Mwakilishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle visiwani Zanzibar anayeiandikia Gazeti la Mwananchi linalomilikiwa na Kampuni ya Mwananchi Communication, Salma Said, ambaye alikuwa ametoweka kwenye mazingira ya kutatanisha tangu tarehe 18 Machi 2016, amepatikana leo jijini Dar es Salaam. 


Kamanda wa polisi wa Dar Simon Siro amethibitisha kupatikana kwa mwanahabari huyo. BBC imezungumza na Mume wa Salma Said, Bw Ali Salim Khamis, ambaye amesema kwa sasa Salma yumo anatoa maelezo kwa polisi Dar es Salaam.

Timu nzima ya Idhaa ya Kiswahili ya DW inawashukuruni wapenzi na wasomaji wetu wa hapa Facebook na wasilikizaji wetu kwa dua na ushirikiano wenu katika kipindi cha siku zote mbili za kutoweka kwa mwenzetu. Tuna furaha pia kwa familia yake na tunazidi kumuombea afya na siha njema.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .