NJAA INAUA WATOTO SOMALILAND
Posted in
afrika mashariki
No comments
Monday, March 28, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Baa la njaa limesababisha vifo vya watoto na mifugo kufuatia ukame wa miaka miwili Somaliland. Maafisa
wa serikali iliyojitangaza huru ya Somaliland wameiambia kituo cha BBC kuwa hofu
imeanza kutanda baada ya mvua kukosa kunyesha kwa mwaka wa pili
mfululizo katika maeneo ya Magharibi wa jimbo hilo lililojitenga kutoka
kwa jamhuri ya Somalia.
Ali Hamud Djibril amesema kuwa watoto kadhaa wameaga dunia huku maelfu ya mifugo ikifa kufuatia ukame huo uliodumu kwa misimu mwili. Eneo hilo la Magharibi lilikuwa limewapokea wakimbizi kutoka Ethiopia lakini hali imezidi kuzorota Somaliland.
Umoja wa mataifa unasema kuwa maelfu kwa mamia ya watu wanahitaji msaada wa dharura Somaliland na mashariki mwa Somalia.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :