HARAMBEE STARS PIGA HAO! WAKENYA TWENDE KAZI!

Posted in
No comments
Monday, March 21, 2016 By danielmjema.blogspot.com


Kesho kuanzia majira ya saa moja jioni, kwenye uwanja wa Estadio Natinal 24 de Satembro, mjini Bissau, timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, watakuwa kibaruani, katika mchezo wa raundi ya kwanza, dhidi ya Guinea Bissau, kusaka tiketi ya kushiriki mashidano ya AFCON 2017.




Mchezo huu ni muhimu sana kwa Harambee Stars mpya iliyojaa sura mpya ya wachezaji chipukizi, Stars mpya iliyochini ya uongozi mpya wa FKF ya 'kijana' Nick Mwendwa, ni Stars iliyochini ya Kocha mpya Mzalendo, Stanley Okumbi.

Hivyo basi, huu ni muda wa kuonesha 'Ukenya' wetu, ni muda wa kusahau tofauti zetu zinazotokana na timu zetu, ni muda wa kusahai masahibu yetu kwenye msimu huu wa ligi, ni kweli kwamba kinachoendelea hivi sasa kinaumiza sana. hasa kwa mashabiki wa timu kubwa kama vile Gor Mahia.

Siasa, ukabila na udini tuweke kando, sote tujitokeze kuisapoti timu yetu, wenye uwezo wa kwenda Bissau twendeni kwa wingi tukaishangalie timu yetu, kwa sababu kilichobaki ni sapoti ya mashabiki, Guinea Bissau lazima afungwe!

Kwa kutizama rekodi ya mechi tuliyokutana nao, ni dhahiri kwamba, Guinea Bissau watataka kulipiza kisasi cha kichapo 2-1 tulichowapa, mara ya mwisho tulipokutana nao mwaka 2011, kwenye mechi ya kutafuta tiketi ya kufuzu AFCON 2012.
 
Kocha mkuu wa Stars, Stanley Okumbi ambaye huu ndio mtihani wake wa kwanza tangu ateuliwe kuchukua nafasi ya Bobby Williamson, tayari ameshaonesha kuwa na imani na vijana wake akitamba kuwanyoa Guinea Bissau.

Wakenya tunapswa kuelewa kuwa matokeo ya kazi ya Okumbi na vijana wake dimbani, unategemea kwa kiasi kikubwa utulivu na sapoti yetu ‘mchezaji namba 12’ hivyo shime tujitokeze kwa wingi kuwaunga mkono.

Katika kikosi chake kinachosafiri kwenda Guinea Bissau, kucheza mechi hiyo ya raundi ya kwanza kundi E, alichotangaza juzi, Kocha Okumbi, amewaacha wachezaji watatu kutoka Gor Mahia ambao ni Harun Shakava, Collins Okoth and Francis Kahata.

Timothy Otieno wa Posta Rangers, Kipa Bonface Oluoch na Musa Mohammed (Gor Mahia), wameungana pamoja na Patillah Omoto na Michael Ovellah Ochieng wa Kariobangi Sharks huku Ayub Timbe wa Lierse SK, akikosekana.

Nahodha Victor Wanyama (Southampton) pamoja na mastaa wengine wataungana na timu mjini Bissau lakini wakati huo Paul Were akishindwa kutokea katika raundi hii ya kwanza kutokana na sababu mbalimbali.


Kikosi kamili.

Makipa: Arnold Origi (Lillestrom, Norway), Boniface Oluoch (Gor Mahia)

Difenda: Dennis Odhiambo (Thika United), Musa Mohammed (Gor Mahia), Omar Mbongi (Ulinzi Stars), David Owino (Zesco United), James Situma (Tusker FC), Brian Mandela (Maritzburg United)
Viungo: Victor Wanyama (Southampton FC), Johannah Omollo (Antwerp), Patillah Omotto (Kariobangi Sharks), Johannah Erick (Mathare United), Clifton Miheso (AFC Leopards), Anthony Kimani, David Kingatua (Bandari FC), Anthony Akumu (Zesco United).

Mastrika: Michael Olunga (IF Djugardens), Timothy Otieno (Posta Rangers), Jesse Were (Zesco United), Ovella Ochieng (Kariobangi Sharks) 

Kikosi cha Harambee Stars kiliondoka nchini juzi (Jumapili, Machi 20) majira ya saa sita usiku ambapo jana iliunganisha ndege ya moja kwa moja hadi Bissau.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .