RAIS KENYATTA NA MUSEVENI WASHINDWA KUFIKIA MWAFAKA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KATI YA KENYA NA UGANDA

No comments
Monday, March 21, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Rais Uhuru Muigai Kenyatta wa Kenya na mwenzake Yoweri Kaguta Museni wa Uganda sasa watalazimika kukutana tena wiki mbili zijazo, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu uwezekano wa kupitisha bomba la mafuta kati ya nchi hizo mbili, jijini Kampala.

Mazungumzo ya awali yaliyofanyika leo katika Ikulu ya Nairobi, haikuzaa matunda baada ya pande mbili ikiongozwa na viongozi hao, kushindwa kufikia mwafaka.

Kwa mujibu wa Taarifa, iliyotolewa na mawaziri wa Nishati wa nchi hizo mbili, mara baada ya kuvunjika kwa kikao cha kujadili swala hilo, kikao hicho kilijikita katika mazungumzo ya kupunguza gharama za ujenzi pamoja na njia mwafaka wa kusafirisha Oili chafu.


Kumekuwa na madai kwamba Uganda imekuwa katika njia panda kuhusu ni njia ipi kati ya Mombasa na Ile ya Tanga nchini Tanzania inataka kutumia kwa ajili ya kusafirisha mafuta yake. Wakati Uganda ikiwa katika hali ya kutokuwa na maamuzi, Kenya kwa upande wake imekuwa ikijitahidi kushinikiza ujenzi wa pamoja wa bomba ya kusafirisha mafuta kati yake na Uganda, huku ikisisitiza umuhimu wa kupunguza gharama za ujenzi huo.

Mkutano wa utakaofanyika wiki mbili zijazo Jijini Kampala, unatarajiwa kuwapa maafisa wa Nishati kutoka nchi zote mbili muda mzuri wa kujipanga kwa lengo la kuongea lugha moja kuhusu namna nzuri ya utekelezaji wa mpango wa  ujenzi wa njia ya kupitisha bomba la mafuta kutoka  Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Lamu.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .