RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
Posted in
Burudani
No comments
Saturday, May 5, 2018
By
danielmjema.blogspot.com
RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
Rapper maarufu wa nchini Cameroon, Atanga Schneider Ngomah maarufu kama Ngoma, ameachia video ya wimbo wake mpya, All Les Day. All Les Day ina maana ya ‘Kila Siku.’ Ukitayarishwa na producer wake wa miaka mingi, Dijay Karl, huu ni wimbo wenye mahadhi ya Hip hop na Trap iliyonakishwa na mitindo asili ya uchanaji katika viunga vya mitaa maarufu ya Cameroon.
Pia ina vionjo vya mtindo wa Jwe’te ambao ni mchanganyiko wa muziki wa asili wa kabila la Ngemba ambavyo vinasikika kwa mara ya kwanza kwenye wimbo. Amesema vionjo hivyo vitasikika zaidi kwenye nyimbo zake zijazo. Pamoja na kutumia Pidgin English (Kiingereza kizungumzwacho Cameroon), Ngoma ametumia Kifaransa pamoja na kabila na Ngemba kwenye wimbo huu. Video yake imeongozwa na Shamak Allharamaji.
Ngoma si mgeni kwenye masikio na macho ya mashabiki wa muziki wa Tanzania. Mwaka jana akiwa na wimbo wake maarufu, Mangosi, alifanya ziara ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika vituo vya redio na TV vikiwemo Clouds TV, East Africa Radio, EFM, Times FM na Magic FM.
Katika ziara yake hiyo, Ngoma alifanikiwa kurekodi collabo na Ray Vanny katika studio za Surprise Music chini ya producer Rash Doni, huku mdundo na ukamilishaji wa wimbo ukifanywa na Dijay Karl. Amepanga kuachia wimbo huo mapema mwakani wakati wa shamrashamra za Kombe la Mataifa ya Afrika. Pia Ngoma amesema baada ya kuachia video takriban nne, ataachia album yake inayosubiriwa kwa hamu, G.O.AT. (Greatest of All Time).
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :