Nahreel afunguka kuhusu Beat ya 'Arosto'
Posted in
Burudani
No comments
Tuesday, June 14, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Baada ya taarifa kusambaa kuwa beat ya wimbo wa G-Nako ‘Arosto’ ilikuwa ya mtayarishaji wa muziki Bongo Fleva, Nahreel na ilipotea baada ya kusahau external yake kwenye studio za Switch Records, mwenyewe amesema kuwa hana uhakika kama ilikuwa yake au lah.
Hadi muda huu inafamika kuwa beat ya wimbo huo imetayarishwa na Luffa kutoka studio za Switch Records zinazomilikiwa na Quick Rocka. Nahreel aliwahi kufanya kazi kwenye studio hizo kabla ya kuanzisha The Industry.
Akiongea na Bongo5, Nahreel amesema kuwa hataki kuthibitisha hilo kama beat ya ‘Arosto’ ilikuwa yake au lah kwa sababu hana uhakika.
“Kusema ukweli kwa sasa siwezi kuthibitisha hilo ile external niliyoiacha pale Switch ilikuwa na beat nyingi sana kama 600. Nimekuwa nikitengeneza beat nyingi sana mpaka niende nikahakiki ndiyo nitajua. Kusema ukweli external yangu iko pale, nikisema hivyo nitakuwa natengeneza kitu ambacho siyo kizuri,” alisema Nahreel.
Hata hivyo Nahreel ameongeza kuwa beat hiyo haiwezi kuwa ya kwake kama ingekuwa hivyo angeifahamu mapema.
Habari Zingine
- New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao
- Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi
- Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu
- Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora
- RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :