BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YATOKEA MAGARI YAKIPISHA MSAFARA WA RAIS KIKWETE MAENEO YA BOMA WILAYA YA HAI MKOANI KILIMANJARO JIONI HII; WATU 40 WANUSURIKA KUFA

Posted in
No comments
Wednesday, April 23, 2014 By danielmjema.blogspot.com




Hai.





ZAIDI ya abiria 40 waliokuwa katika basi la Urio linalofanya safari zake kati ya mikoa ya Arusha na Lushoto-Tanga wamejeruhiwa vibaya baada ya basi hilo kupinduka wakati likijaribu kukwepa basi jingine katika makutano ya barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA.





Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio walisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10 jioni jirani kabisa na kituo cha mafuta kilichopo kando ya barabara ya Moshi-Arusha wakati magari hayo yakijiandaa kuanza safari mara baada ya kuzuiliwa kwa muda kupisha msafara wa Rais Kikwete.





Taarifa kutoka eneo la tukio zimesema basi hilo lilipinduka wakati likijaribu kupishana na magari yaliyokuwa yakitokea Arusha ambayo yalianza safari bila ya kuwa na mpangilio hali iliyosababisha kutokea kwa ajali hiyo.





Ajali hiyo imetokea ikiwa ni muda mchache msafara wa raisi Jakaya Kikwete kupita katika eneo hilo ukielekea uwanaja wa ndege wa KIA , ukitokea wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro ambako Amefanya ziara ya siku mbili.





Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema baada ya msafara wa rais kupita magari yaliyokuwa yamesimamishwa kwa muda mrefu yaliondoka bila ya kuwa na mpangilio maalum hali iliyosababisha kutokee kwa ajali hiyo.





Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz hakuweza kupataikana mara moja kuzungumzia ajali hiyo kutokana na ugeni wa rais huku simu yake ikiita mara kadhaa bila ya kupokelewa .






picha ya chini na juu ni baadhi ya majeruhi walikuwa kwenye  basi hilo aina ya Urio lililopata ajali leo jioni katika eneo la Kia wilayani Hai  mkoani Kilimanjaro
 wananchi wawakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliotokea leo jioni katika eneo la kia ambapo inasemekana watu zaidi ya 31 wamejeruliwa

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .