ALIYETAKA KUMTAPELI DKT. SLAA KESI YAKE YAPIGWA KALENDA
Posted in
Sheria
No comments
Friday, May 2, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi wetu, Hai
Usikilizwaji
wa kesi ya jaribio la kumtapeli katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, umekwama baada ya hakimu anayeisikiliza
kupata udhuru.
Jaji mkuu
mstaafu,Barnabas Samatta, Mbunge wa Arusha mjini,Godbless Lema na wakili wa
Chadema, Profesa Abdalah Safari ni miongoni mwa mashahidi 12 watakaotoa
ushahidi katika kesi hiyo.
Kesi hiyo
inayovuta hisia za wakazi wa miji ya Arusha na Moshi, ilikuwa imepangwa kuanza
kusikilizwa Ijumaa iliyopita mbele ya hakimu mkazi wa wilaya ya Hai, Denis
Mpelembwa.Hata hivyo
kesi hiyo iliahirishwa baada ya Hakimu kuwa nje ya ofisi kikazi.
Inadaiwa
kati kati ya Aprili na Mei, 2012, mshitakiwa Abedi adamu Abeid (23),
alijitambulisha kwa Dk. Slaa, Lema na Profesa Safari kuwa yeye ni mkuu wa
Takukuru wilaya ya Ulanga, Abel Kibaso.
Katika
kipindi hicho pia, mtuhumiwa aliwapigia simu viongozi hao akijitambulisha ni
Jaji mstaafu Samatta akitaka wampe pesa ili washinde katika kesi namba 47/2012
iliyokuwa mahakama ya Rufaa.
Rufaa
hiyo ilifunguliwa na Lema dhidi ya Mussa Hamisi na wenzake akipinga
hukumu ya mahakama kuu Arusha ya kumvua Ubunge wa Arusha mjini.
Hata hivyo
Lema alishinda Rufaa hiyo na kurudishiwa Ubunge wake.waendesha
mashitaka kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (takukuru) wanadai
mtuhumiwa alijifanya ni Jaji mkuu mstaafu Samatta wakati akijua siyo Jaji
Samatta kwa lengo tu la kujipatia fedha kinyume cha sheria.
Mshitakiwa
amekanusha mashitaka hayo na sasa kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Mei 21 baada
ya kukwama kusikilizwa Ijumaa iliyopita.
Mwisho
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :