KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA MCHANA WA LEO
Posted in
Bunge
No comments
Friday, May 23, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta akijibu hoja za
wabunge kabla Bunge halijapitisha Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa
Afrika ya Mashariki kwa Mwaka 2014/2015.
Maofisa
wa wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wakiwa pamoja na
Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakifuatilia kikao cha Bajeti ya Wizara
ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa
Mwaka 2014/2015.
Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta akijadiliana
jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya
Mashariki,Joyce Mapunjo mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara
hiyo kwa Mwaka 2014/2015.
Wabunge wa Afrika Mashariki wakiwasili Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa kuteuliwa Mhe.James Mbatia akifurahia jambo na Mhe.Shyrose Banji Mbunge wa Afrika Bunge la Afrika ya Mashariki.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Joyce Mapunjo
(kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano,Mhe.Samia Suluhu (kushoto) na Mhe.Celina Kombani.
Mbunge
wa Chalinze,Mhe.Ridhiwani Kikwete (kushoto) akijadiliana jambo na
Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki,Mhe. Shyrose Banji
Wanachuo
kutoka Chuo cha Mipango Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja nje ya
viwanja vya Bunge wakati walipofanya ziara ya kimafunzo Bungeni na
kufuatilia Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa
Mwaka 2014/2015.
Wanachuo
kutoka Chuo cha Uuguzi Mirembe Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja nje
ya viwanja vya Bunge wakati waliofanya ziara ya kimafunzo Bungeni na
kufuatilia Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa
Mwaka 2014/2015 .
Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ,Joyce Mapunjo wakiwa
kwenye picha ya pamoja na Maofisa wa wizara yake pamoja na Wabunge wa
Afrika ya Mashariki mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara ya
Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa Mwaka 2014/2015.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :