MACHIFU 120,MRISHO MPOTO NA WEMA SEPETU KUNOGESHA TAMASHA LA MTU KWAO ARUSHA LEO
Posted in
Matukio
No comments
Thursday, May 15, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
chifu Gilbert Isambe akiwa na vazi la kichifu
chifu Gilbert Isambe akiwa anaongea na vyombo vya habari pembeni ni mratibu wa tamasha la Mtu kwao bi Janeth Jonas
Zaidi ya machifu 100 kutoka katika mikoa mbalimbali hapa
nchini wanatarajia kuuthuria katika tamasha la mtu kwao linalotarajiwa kuanza
kutimua vumbi May 15 hadi 20 mwaka huu
katika kiwanja cha kumbu ya sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa Mratibu wa
tamasha hilo ambaye ni mkurenzi wa kampuni ya Utamaduni Traning L.T.D Janeth Jonas alisema kuwa tamasha hilo
litashirikisha machifu 120 kutoka katika mikoa mbalimbali na makabila
mbalimbali ya hapa nchini.
Alibainisha kuwa nia
na dhumuni la kuandaa tamasha hili la mtamaduni wetu ni kuweza kuuenzi utamaduni wa mtanzani ambapo ni
kuanzia mavazi ya makabila mbalimbali,vyakula pamoja na ngoma kutoka katika makabila yote hapa nchini.
“pia katika tamasha hili tumeamua kuwaita machifu mbalimbali
l kutoka katika makabila mbalimbali hapa
nchini na baadhi ya mchifu ambao watauthuria ni pamoja na chifu kutoka oldmoshi
ambaye yeye ameshawasili hapa Arusha kwaajili ya tamasha hili Gerald Mandera ,chifu Gilbert Rugal Isambe kutok a kasulu
na wengine wengi wote watakuwepo”alisema Janeth
Aidha alisema kuwa katika tamasha hili kila mtu atapata
fursa ya kuona ngoma kutoka katika makabila mbalimbali pamoja na kuonja chakula cha kila aina cha
makabila ya hapa nchini pamoja na nje ya nch
Alisema kuwa pia katika tamasha hili zaidi ya vikundi vya
ngoma 100 vitatumbuiza pamoja na wasanii mbalimbali akiwepo msanii wa ngoma za
utamaduni Mrisho mpoto,wema sepetu
,kundi la weusi kutoka Arusha,Jambo Squards ,Dogo janja
pamoja na msanii kutoka nchini Kenya Daniel
ole Sekuo.
Naye
mmoja wa machifu ambaye atauthuria tamasha hilo Chiefu Gerald Mandera kutoka
oldmoshi alisema kuwa waandaaji
wamefanya jambo jema sana kuanda tamasha hili
kwani wao ndo wametambua uwepo wa machifu na wameona umuhimu wao mpaka
wameamua kuwakusanya pamoja katika tamasha kama hili.
Alisema kuwa sasa ivi serekali nayo inawajibu
wa kujipanga vilivyo na kutenga siku maalumu kwa ajili ya kufanya tamasha hili
kama jinsi wenzetu kutoka katika nchi zingine wanavyo azimisha siku hii katika tarehe hizi na mwezi huu kila mwaka.
Aidha alibainisha kuwa kuwakusanya watu
mbalimbali kutoka katika tamaduni mbalimbali pamoja na makabila mbalimbali
itasaidia kwani inaweza kuwezesha hata
nchi kupata vazi la taifa kwani makabila haya yate yanakuja yakiwa yamevaa vazi
la ukabila wao na hii itakuwa fursa pekee ya kuweza kuchagua vazi hasili la mtanzanzia.
“ni
aibu kubwa sana unakuta sisi kama watanzania hadi leo hii atuna vazi
linaloweza kutuwakilisha sisi kama watanzania na ukiangalia wenzetu wa n je ya
nchi wanamav azi yao ya kiutamaduni
ambao ukimuona tu mtu amevaa unajua
katoka katika kabila Fulani,naitanishangaza
sana kuona mtu anauzarau utamaduni wake na anauweka mbele utamaduni wa kigeni “alisema
chifu Gilbert Isambe
Aidha alibainisha kuwa hii ni fursa ya watu
kuja kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo ,akiwasihi wanafunzi wa shule
mbalimbali pamoja na wanavyuo mbalimb ali kuja katika tamasha hili kushuhudia
na kuwaona machifu ambao muda mrefu walikuwa wanawasoma tu kwenye vitabu bila
kuwaona moja kwa moja.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :