MB DOG AIMWAGIA SIFA VIDEO YAKE MPYA YA "MBONA UMENUNA"

Posted in
No comments
Wednesday, May 21, 2014 By danielmjema.blogspot.com


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam 

MKALI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amesifia video ya wimbo wake mpya ya Mbona Umenuna akisema imeandaliwa kwa kiwango cha juu na kudhihirisha ubora wake. 


Akizungumza leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema mashabiki wote watakaopata bahati ya kuitazama video hiyo iliyotengenezwa na Abby Kazi, ataamini makali yake. Alisema lengo lake ni kuwapatia mashabiki burudani kami

Alisema lengo lake ni kuwapatia mashabiki burudani kamili, hivyo wadau wote wapate muda wa kuitazama video hiyo iliyoachiwa rasmi mwishoni mwa wiki iliyopita, sambamba na kuingizwa kwenye mitandao ya kijamii, youtube na blogs.

 “Hii ni safari yangu ya kurudi katika makali yangu ya zamani, hivyo naamini wimbo wangu ulipokewa kwa shangwe na sasa nimeachia video. “Mashabiki wote naomba waniunge mkono kwa kuiangalia kazi hii na kusubiri mambo mazuri zaidi kutoka kwangu, maana mipango yangu ni kufanya kazi nzuri zaidi ya Bongo Fleva,” alisema.

Katika video hiyo, msanii huyo anaonyesha ujuzi wa aina yake wa kuimba, huku mdundo ‘beat’ yake ikipigwa kisasa zaidi kulingana na mabadiliko ya kisanii kwa wakali wengi Tanzania.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .