MKUTANO WA NNE WA WADAU WA NSSF WAENDELEA KWA SIKU YA TATU JIJINI ARUSHA LEO

Posted in
No comments
Thursday, May 15, 2014 By danielmjema.blogspot.com


 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akiwasilisha mada yake iliyohusu Umuhimu wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii kwa Sekta zisizo rasmi wakati wa Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF unaoendelea,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 Bi. Faustina Nti kutoka nchini Ghana akiwasilisha Mada yake yenye kueleza uzoefu wa utoaji wa Huduma katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii katika nchi ya Ghana.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na Wadau kwenye Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF unaofanyika,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 Bw. Morris Mbetsa akiwasilisha mada yake iliyohusu umuhimu wa Kuongeza Kasi ya Uvumbuzi na Ubunifu katika Mashirika wakati wa Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF unaoendelea,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 Mwenyekiti Mpya wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA),Juma Ally Muhimbi akichangia mada kwenye Mkutano wa nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF unaofanyika,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akielekeza jambo wa Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Bi Eunice Chiume wakati wa Mkutano huo unaendelea kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC,Jijini Arusha.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .