NEY WA MITEGO ANAJIVUNIA MAFANIKIO YA "KULA UJANA'
Posted in
Muziki
No comments
Saturday, May 31, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa Hip Hop, Emmanuel Elbariki maarufu kama Ney wa
Mitego, amesema wimbo wake wa ‘Nakula Ujana’ unampa raha kutokana na kupokewa
kwa shangwe na mashabiki wa kizazi kipya nchini.
Msanii Ney wa Mitego pichani.
Ney wa Mitego aliyasema hayo katika mazungumzo ya kuelezea namna gani amejiwekea mikakati ya kulinda hadhi na uwezo wake kisanaa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya uzinduzi wa huduma mpya
ya Kampuni ya Simu za Mikononi ya Airtel Tanzania, inayojulikana kama switch
on, katika Hoteli Kilimanjaro Kempisk, inayotoa urahisi wa wateja wao kupata
huduma ya internet kwa urahisi.
Alisema kuwa wimbo wake huo wa Nakula Ujana umetokea kupendwa na wengi, hasa anapokuwa katika maonyesho mbalimbali, hivyo kuonyesha kuwa maendeleo yake kisanaa yamekuwa mazuri kupita kiasi.
“Nawashukuru wadau wangu wote kwakuwa wanapenda kazi zangu,
hasa huu wimbo wa Nakula Ujana, ambao mimi mwenye unanipa raha.
“Naamini kila kitu kitakuwa kizuri zaidi kwa kuwapatia raha
mashabiki wangu wakati wowote, kwakuwa bado nitaendelea kupambana ili kufanya
vizuri zaidi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini,” alisema.
Katika uzinduzi huo wa huduma ya Airtel, watu mbalimbali
walialikwa, sambamba na msanii Barnabas na Vanessa Mdee nao kuwa miongoni mwa
wasanii waliokutana kwa pamoja katika tukio la aina yake.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :