MATUKIO MANNE KABLA YA AJALI NA PICHA YA ARI ALILOPATA NALO AJALI DIRECTOR GEORGE OTIENO "BABA SONIA" TYSON

Posted in ,
No comments
Saturday, May 31, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.30 AMDj Choka ambae kwa sehemu kubwa alikua kwenye safari moja ya Dodoma na Marehemu George Tyson, ameandika kwenye http://djchokamusic.com/ kwamba Marehemu alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.
Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Kwenye gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza. Kwenye hii safari, George Tyson aliambatana na mtangazaji Mboni Masimba wa The Mboni show.
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.12 AM
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.38 AM
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.58 AM
Screen Shot 2014-05-31 at 3.47.07 AM

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .