Giggy Money: Nimekoma 'kuwashobokea' Wanaume wa mitandaoni
Posted in
afrika mashariki
,
Burudani
No comments
Saturday, May 14, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
STAA wa Bongo fleva ambaye jana ameachi wimbo wake unaoitwa ‘Supu’ amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hataki tena wanaume wa mitandaoni na kudai kuwa wanaume hao wamempa somo.
Giggy Money akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo amesema kuwa msanii Hemedy Phd pamoja na Rich Mavoko ndiyo wasanii ambao walimtokea kupitia njia ya mtandao na kitu walichomfanya kimemfanya asitamani tena wanaume kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa sasa sitaki kabisa wanaume kwenye mitandao ya kijamii kwani niliwahi kuwa nao wawili ambao walinitokea kwa njia ya mtandao ambao ni Hemedy Phd pamoja na Rich Mavoko ila kwa walichonitenda sitaki tena wanaume wa mitandao ya kijamii,” alisema Giggy Money.
Mbali na hilo Giggy Money amesema kuwa anatamani kufanya kazi na msanii Vanessa Mdee na Shaa kwani ni wasanii ambao wanajielewa na wanajitambua hivyo anatamani sana kuja kufanya nao kazi.
eatv.tv
x
Habari Zingine
- Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi
- Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu
- Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
- RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
- New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :