UPDATES ZA MSIBA WA MTOTO WA ANKAL: MWILI UMESHAWASILI DAR ES SALAAM, MAZISHI LEO JUMAMOSI SAA 10 ALASIRI MAKABURI YA KISUTU
Posted in
Kifo
No comments
Saturday, May 14, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Assalaam Aleikhum,
Updates za familia ya 'Ankal' Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin (18), aliyefariki Jumapili Mei 8, 2016 huko Durban, Afrika Kusini:
Mwili wa Marehemu umeshawsili nchini jana Ijumaa Mei 13, 2016 majira ya saa tisa mchana kwa ndege ya shirika la Emirates kupitia Dubai (kwa kukosekana kwa ndege za moja kwa moja kuja nchini kutoka Durban). Mwili wa kijana wetu umepokelewa na ndugu, jamaa, majirani na marafiki katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere eneo la Cargo la Swissport, Jijini Dar es salaam.
Mazishi yamepangwa kufanyika leo Jumamosi saa 10 alasiri katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Taratibu za kuandaa mazishi zitaanza saa 4 asubuhi leo Jumamosi, nyumbani kwa mama wa marehemu kota za Wazo Hill, Tegeta, ulipo msiba.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Maggid baada ya kuwasili Dar es salaam jana Ijumaa
Michuzi akiwa na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kuwasili na mwili wa marehemu katika msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es salaam, ambako unahifadhiwa hadi baadae leo kabla ya kupelekwa Wazo Hill saa nne kwa dua na baadaye kurudi hapo msikitini kuswaliwa na hatimaye kupelekwa makaburi ya Kisutu kwa mazishi saa 10 Alasiri.
Michuzi akiwa na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kuwasili katika msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es salaam
Michuzi akiwa msibani Wazo Hill na wanahabari wenzie usiku huu. Kutoka kushoto ni Faraja Mugwabati, Maggid Mjengwa na Sufiani Mafoto.
NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement cha Wazo Hill, mbele mkono wako wa kulia kuna Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona Bar yenye uzio wa rangi ya njano ambao umeandikwa "Twiga Cement", hapo pana bango linaloelekeza njia karibu na kituo cha Bajaji nje. Unaingia upande huo wa kulia mita 250 mbele unakata tena kulia, mita 70 mbele utakuta maturubai, ndipo msibani.
Innalillah wa inna ilayhi raajiun
-AMIN.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :