ALPHONCE FELIX WA TANZANIA AJITOA MADOLA

No comments
Saturday, July 26, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Mwanariadha wa Tanzania Alphonce Felix Simbu amelazimika kujitoa katika mashindano ya Commonwealth Games yanayoendelea mjini Glasgow Scotland baada ya vipimo kuonyesha kwamba ana jeraha katika mguu wake.
Alphonce Felix alikuwa akisumbuliwa na jeraha hilo tangu akiwa mazoezini Ethiopia hadi kupelekea yeye kushindwa kushiriki mashindano ya taifa, alisisitizza kwamba anaumwa lakini RT hawakuwa wasikivu!

Alfonce Felix alikuwa awakilishe Tanzania katika mbio za mita 10,000 na 5000.

Hivyo sasa Tanzania imepata pigo jingine katika siku ya pili ya mashindano ya Jumuiya ya Madola.

Uingereza inaongoza kwa kuwa na medali 17 ikifuatiwa na Australia ikiwa na medali 15 huku mwenyeji Scotland ikishikilia nafasi ya tatu. 

Kwa upande wan chi za kiafrika Afrika Kusini, Nigeria na Ghana zimefanikiwa kupata medali kadhaa. Gidabuday Blog inatoa pole kwa mwanariadha huyo mpole na mwenye bidii !..

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .