Mlipuko waua watu watano Nigeria
Posted in
Kifo
No comments
Tuesday, July 1, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Takriban watu watano wameripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea sokoni Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa gari lililokuwa limebeba mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.
Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kuandaa shambulio hilo.Watu walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa gari lililokuwa limebeba mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.
Tukio hili linakuja huku ripoti ya hivi karibuni ya jeshi la Nigeria ikisema kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi la wapiganaji la Boko Haram.
Mwandishi wa BBC Habiba Adamu toka mji mkuu wa Nigeria Abuja aliyetembeela eneo hilo anasema kuna utata wa idadi ya waliouawa katika shambulio hilo kwani wakati wengine wakisema waliouawa ni watano wengine wanasema huenda idadi ya waliouawa ikawa ni zaidi ya hiyo iliyotolewa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :