MOSHI CLUB WALIVYOIBUKA MABINGWA KATIKA SERENGETI FIESTA SOCCER BONANZA.

Posted in
No comments
Saturday, August 30, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Mbwiga akijaribu kufanya mambo ya kiufundi uwanjani.
Mbwiga akiongoza timu ya Kitambi noma kupiga jaramba kabla a mchezo wao dhidi ya Mandela Bar.
Kikosi cha timu ya Qx Pub kilikuwa kimesheheni wachezaji nguli akiwemo Shaffih Dauda.
Mbwiga akijaribu kumtoka mchezaji wa tiu ya Oysterbay.
Mchezaji Shaffih Dauda akijaribu kuweka mpira katika himaya yake.
Mbwiga akijiandaa kutoa pasi ya mwisho.
Shaffih akijaribu kufunga kwa kupiga mpira "Kizungu"hapa .
Mbwiga akiwafunga watu tela.
Moja kati ya faulo hatari ikipigwa na Shaffih, kama sio umakini wa walinzi wa Oyster Bay  ali manusura izae goli 
Mzaramo injini ikachemsha ,benchi la ufundi likaamua kumpumzisha.
Kama kawaida alivyo "Unga wa Ngano"kupika kila aina ya vitafunio ,Mbwiga akaingia kwenye kutangaza mechi hiyo.
Ghafla akaachana na shughuli ya kutangaza mechi akageuka Mmachinga akaanza kuuza T-shirt.
Ikafika mapumziko timu zote zikiwa zimetoshana nguvu ya bila kufungana.
Baada ya Injini kupoa Mbiwga tena akaomba kuingia.
Watu wa huduma ya kwanza walikuwa makini kuhakikisha kila aliyepata tatizo anahudumiwa mara moja.
Kikosi cha Mandela Bar kikiwa mapumziko huku kikifanya maandalizi ya mchezo wa fainali dhidi ya Moshi club.
Kikosi cha Moshi club wakijaribu kubadilishana mawazo. 
Clouds fm radio walikuwa live uwanjani hapo.
Kikosi cha Mandela Bar kilichocheza fainali 
Kikosi cha Moshi Club kilichocheza fainali.
Mpira mwingi sana ulipigwa kati ya timu  hizi mbili ambazo zilikuwa mahasimu.
Wadau mbalimbali walikuwepo uwanjani hapo kufuatilia Bonanza hilo.
Mechi ilipigwa hadi kufikia hatua ya matuta.
Mchezaji Mtanange wa Moshi Club ndiye aliyepiga penati ya mwisho iliyoipatia ubingwa wa bonanza hilo klabu yake ya Moshi .
Viongozi wa Moshi Club wakiwa wamembeba juu juu Mtanange.
Wachezaji wa Moshi club wakashangilia kwa style za aina tofauti tofauti ikiwemo ile ye Kidiaba.
Baadaye utaratibu wa kutangaza washindi ukafanyika ,hapa ni Shaffih Dauda na Dixon Busagaga wahusika katika maandalizi ya Bonanza hilo.
Zawadi za kreti tano za bia zikatolewa kwa mshindi wa Pili timu ya Mandela Bar.
Washindi Klabu ya Moshi wao pia wakapata zawadi yao ya kreti 10 za bia.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .