RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA DARAJA LA GULWE MPWAPWA
Posted in
Matukio
No comments
Saturday, August 30, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza kushoto akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu pamoja na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene, akiweka jiwe la msingi kama ishara ya kuzindua rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa mita 170 litakalo unganisha kati ya Wilaya ya Mpwapwa na Kibakwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglicana Tanzania Jacob Chimeleja, Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu, Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa mita 170.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na Mkandarasi,viongozi wa dini na kitaifa mara baada ya Rais kuzindua rasmi ujenzi wa daraja la Gulwe.
Daraja la Gulwe linalotumika sasa kama linavyoonekana hali iliyopelekea Serikali ya awamu ya nne kupitia Wizara ya Ujenzi kuanza kujenga daraja kubwa na la kisasa la Gulwe litakalokuwa na mita 170 mara baada ya kukamilika kwake.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akipita mbele ya Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa Mita 170.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wapili kutoka kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi ERB Profesa Ninatubu Lema watatu kutoka kulia pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wakifatilia ngoma za asili kabla ya uzinduzi rasmi wa Daraja la Gulwe
Ujenzi wa Makalvati yatakayosaidia Daraja kupitisha maji katika mto Gulwe kama yanavyoonekana. Jumla ya Makalvati tisa yatajengwa katika daraja hilo la mita 170.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ili kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akizungumza na Mbunge wa zamani wa Mpwapwa George Malima Lubeleje kabla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia akiwatambulisha Wakurugenzi, Wenyeviti, Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Ujenzi kabla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Daraja la Gulwe litakalokuwa na mita 170.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :