KILIMANJARO MARATHON 2015 YAZINDULIWA

Posted in
No comments
Friday, November 7, 2014 By danielmjema.blogspot.com


·         Tigo wadhamini wapya Nusu Marathon

Mbio za 13 za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika Moshi tarehe 1 Machi, 2015 zimezinduliwa leo jijini Dar es salaam. 

George Kavishe, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager alisema “Sasa tumeingia mwaka wa 13 wa udhamini wa Kilimanjaro Marathon. Tunafurahi kuona Kilimanjaro Marathon kwa mara nyingine tena ikiwa kivutio kwa makampuni mbalimbali, hii ni uthibitisho wa jinsi mbio hizi zilivyoendelea kuwa kubwa na kivutio chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager tangu zilipoanzishwa.”

“Kilimanjaro Premium Lager ina furaha kuona jinsi ambavyo Kilimanjaro Marathon imepata mvuto na kuleta shauku kubwa kwa washiriki wa hapa nchini na wa kimataifa kwa mara nyingine tena mwaka huu. Udhamini wetu kwa Kilimanjaro Marathon umelenga kuwapa nguvu wanariadha wetu na kuendeleza ari ya ushindi ili kuipeleka riadha ya Tanzania juu zaidi.”

Tangu udhamini wetu wa kwanza kwa Kilimanjaro Marathon mwaka 2003, tumeshuhudia ukuaji wa mbio hizi na tuna furaha kubwa kwa fursa ya kuendelea kuwa sehemu ya mbio hizi na kuweza kuwaletea wanariadha wetu tukio kubwa la kimataifa hapa nyumbani. Tunatarajia kuwa na tukio la kusisimua na tunayofuraha kutangaza kwamba Kilimanjaro Marathon 2015 itakuwa ya kuvutia na yenye msisimko zaidi na tunakaribisha watu wote wajitokeze kushiriki mbio hizi za aina yake tarehe 1 Machi 2015.

Akitangaza udhamini wa Tigo kwa mbio hizo, Meneja Chapa waTigo, William Mpinga alisema udhamini huo ni sehemu ya wajibu wa kampuni hiyo katika maendeleo ya michezo nchini na pia katika kusaidia jitihada za uhifadhi wa Mlima Kilimanjaro, kivutio kikubwa cha utalii Tanzania”

“Tuna furaha sana kuwa sehemu ya mbio hizi za aina yake ambazo zimepata mafanikio makubwa sana katika kuutangaza Mlima Kilimanjaro kama kivutio cha kipekee cha utalii hapa nchini na nje. Kama kampuni ya Kitanzania, tunajivunia mbio hizi kwa kuleta fursa ambayo sio tu uwavutia wanariadha wa kimataifa, lakini pia ni jukwaa muhimu la kuionyesha dunia vipaji vyetu katika riadha,” alisema Mpinga.

Meneja Chapa huyo alisema kwamba mbali na kufurahia mbio za nusu marathon zitakazojulikana kama “Tigo Kili Half Marathon” zinazodhaminiwa naTigo mashabiki na wakazi wa Moshi watapewa fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali za dijitali kutoka Tigo na huduma zitakazoonyeshwa kwenye mbio hizo.

Meneja Utawala wa GAPCO, Jumbe Onjero alisema: "GAPCO, wadhamini wa mbio za Marathon za Walemavu kwa kushirikiana na waandaaji  Wild Frontiers, Deep Blue Media na Executive Solutions tutatoa msaada wa viti vya magurudumu 50 kwa wahitaji mkoani Kilimanjaro ikiwa ni kuonyesha wajibu wetu kwa jamii.”

Kilimanjaro Marathon ilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2003 na imekua na kuwa moja kati ya mbio kubwa zaidi barani Afrika ikiwa na washiriki zaidi ya 6,000 kutoka nchi zaidi ya 40. “Kilimanjaro Marathon imeendelea kuboreshwa kila mwaka, kwenye mbio ya kwanza mwaka 2003 tulikuwa na washiriki 750 tu, lakini kwenye mbio zilizopita tulikuwa na washiriki zaidi ya 6,000 na idadi hii inatarajiwa kuongezeka ukizingatia hizi ndio mbio zenye mvuto zaidi kwa watalii barani Afrika,” alisema John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo.

Mbio hizi zinadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu), Tigo (Nusu Marathon), GAPCO (Mbio yaWalemavu), pamoja na wadhamini wa vituo vya maji kwenye mbio hizo ambao ni Kilimanjaro Water, FNB, CMC Automobiles, Simba Cement, TPC Sugar, KK Security, Kibo Palace, Rwandair na UNFPA.
MWISHO


PRESS RELEASE
5/11/2014
2015 KILIMANJARO MARATHON LAUNCHED
·         Tigo are new Half Marathon sponsors
The 13th edition of the annual Kilimanjaro Marathon scheduled to take place in Moshi on 1 March 2015 was launched in Dar es Salaam today. The Kilimanjaro Premium Lager Brand Manager, George Kavishe said “We have now entered the 13th year of Kilimanjaro Marathon sponsorship. We are proud to see the Kilimanjaro Marathon once again attracting involvement of various corporate sponsors, a demonstration of how big and attractive this event has become under Kilimanjaro Premium Lager since its inception.”

“Kilimanjaro Premium Lager are thrilled to see the tremendous enthusiasm and support for Kilimanjaro Marathon event and our local and international runners once again this year. Our sponsorship of the Kilimanjaro Marathon aims to inject positive energy into our Tanzanian athletes and foster a winning spirit that would take local athletics to the next level.”

Since our first sponsorship to Kilimanjaro Marathon in 2003, we have witnessed the spectacular growth of this event and we are so thrilled for the opportunity to continue being part of it, but more importantly to add to our support to national athletes and help them experience the excitement of an international sporting event at their door step. 

We are looking forward to an exciting event and we are delighted to declare that the 2015 Kilimanjaro Marathon will bring more excitement than ever and we invite everyone to show up on the starting line on 1st March, 2015 for yet another spectacular marathon experience”
Announcing Tigo’s sponsorship towards the annual event, Brand Manager William Mpinga, said this was part of the company’s commitment to the development of sports in the country as well as towards the conservation efforts of Mount Kilimanjaro, the symbol of Tanzania’s tourism attraction prowess.

“We are truly delighted to be part of this great annual marathon race that has achieved so much in creating awareness of the Mount Kilimanjaro as a unique tourist attraction both locally and abroad. As a Tanzanian company, we also take pride in the event for creating a platform that, not only attracts international athletes, but is also a unique opportunity to showcase our local athletic talents to the world,” Mpinga said.
The Brand Manager said apart from enjoying the “TigoKili Half Marathon” sponsored by Tigo, athletic fans and the residents of Moshi town coming to see the race will be accorded to a unique opportunity of experiencing all Tigo digital products and services which will be showcased during the event.

JumbeOnjero, the GAPCO Human Resources and Administration Manager said: “GAPCO, the GAPCO Disabled Marathon sponsor in collaboration with organisers Wild Frontiers, Deep Blue Media and Executive Solutions will be donating 50 wheelchairs to the needy recipients in Moshi as a demonstration of our commitment to the community."

Kilimanjaro Marathon took place for the first time in 2003 and has grown to become one of the biggest races in Africa attracting over 6,000 runners and participants from over 40 countries.

“ Kilimanjaro Marathon has constantly been improving every year, during the inaugural event in 2003, we had 750 athletes, but in last year’s twelfth edition, we had over 6,000, a number is set to increase since this is the best destination marathon in Africa,” said John Addison, Managing Director of Wild Frontiers, organizers of the event.

The event is sponsored by Kilimanjaro Premium Lager (title sponsors), Tigo (Half Marathon), GAPCO (Disabled Marathon), as well as Water Table sponsors; Kilimanjaro Water, FNB, CMC Automobiles, Simba Cement, TPC Sugar, KK Security, Kibo Palace, Rwandaira and UNFPA.

END

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .