By
danielmjema.blogspot.com
|
Mkurugenzi wa Idara ya Oparesheni ya Benki ya Azania, Togolani
Mramba (wa pili kushoto), akimkabidhi zawadi mmoja wa wateja wakuu wa
Benki hiyo mkoani Kilimanjaro, Mfanyabiashara wa Nafaka, Izina Rashid
Msangi, ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa Benki hiyo kutoa mkono wa
shukrani kwa wateja wake na kuwatakia heri katika sikukuu ya Krismasi
na Mwaka Mpya, wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa Benki hiyo, wakiongozwa
na Meneja wa Azania Tawi la Moshi, Bi. Hajira
Mmambe. |
|
Timu ya Wafanyakazi wa Benki ya Azania ikipita mitaani
kuwazawadia wateja wao na kuwapa mkono wa Heri ya Krismasi na Mwaka
Mpya. |
|
Ilikuwa ni msako wa mtaa kwa mtaa, ofisi hadi ofisi,
kuhakikisha wateja wote wanapata sababu ya kuendelea kuamini Benki
hiyo na kudumisha udugu wa kibiashara. |
|
Mkurugenzi wa Oparesheni wa Benki ya Azania makao makuu,
Togolani Mramba (wa kwanza kulia) akiwa na timu ya wataalamu kutoka
tawi la Moshi, katika ofisi ya Mfanyabiashara wa Mafuta katika Stendi
ya Mboya, Manispaa ya Moshi, Thomas Siara Mushi
(Musisha). |
|
Bw. Mramba (aliyevaa koti) akimpa mkono wa shukrani na wa
kumtakia heri ya Krismasi na Mwaka Mpya, Mfanyabiasha wa Mafuta katika
stendi ndogo ya Mboya, Thomas Siara Mushi
(Musisha). |
|
Meneja wa Benki ya Azania Tawi la Moshi, Bi. Hajira Mmambe,
akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Five Star Hardware, Bw.
Frank Lesilian, ikiwa ni
utaratibu wa kawaida wa Benki hiyo kutoa mkono wa shukrani kwa wateja
wake na kuwatakia heri katika sikukuu ya Krismasi na Mwaka
Mpya. |
|
Ni muda wa kufurahia ushirikiano mzuri katika
Biashara na kupongezana. |
|
Uongozi wa Benki ya Azania Tawi la Moshi, ukiongozwa na
Mkurugenzi wa Oparesheni makao makuu, Togolani Mramba ukikabidhi
zawadi kwa Mkurugenzi wa Ibra line Company, Ibrahim Shayo kama sehemu
ya mkono wa Krismasi na heri ya Mwaka mpya. |
|
Hapa kikosi hicho kikakutana na Mkuregenzi Mtendaji wa Dema
Construction, Dismas Massawe (aliyeshika mfuko) akikatiza mitaani na
kumzawadia akiwa ni mmoja wa wateja wakubwa wa benki ya Azania Tawi la
Moshi. |
|
Heka heka za kuwasaka Wateja wakuu wa Benki hiyo mjini Moshi
ziliendelea, ambapo safari hii, Kikosi kizima kikiongozwa na
Mkurugenzi wa Oparesheni, Togolani Mramba (wa kwanza kushoto),
kilibisha hodi katika Ofisi za Mkurugenzi wa Kilimani Pharmacy, Arthur
Kiwia na kumpa zawadi yake. |
|
Safari ikaishia kwa Mmiliki wa Salsalnero Hotel, Benjamin
Mengi (ambaye ni mdogo wake na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dkt.
Reginald Mengi) |
|
Meneja wa Benki ya Azania Tawi la Moshi, Bi. Hajira Mmambe
(kulia) akifurahia jambo na Mzee Mengi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya
Kaskazini |
0 MAOINI :