Showing posts with label Biashara. Show all posts
Showing posts with label Biashara. Show all posts

Tigo yakabidhi Kompyuta na Printa kwa Jeshi la Polisi Mwanza, Tanzania

Tigo yakabidhi Kompyuta na Printa kwa Jeshi la Polisi Mwanza, Tanzania

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi,akizungumza na Mkurugenzi wa Kanda ya ziwa wa mtandao wa tigo Ali Maswanya(kushoto) jijini Mwanza jana,baada ya kupokea kompyuta na printa wakati wa hafla ya makabidhiano ,kulia ni Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mwanza ACP Augustino Senga akishuhudia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi,akipokea kompyuta na printa kutoka kwa Mkurugenzi wa Kanda ya ziwa wa mtandao wa tigo Ali Maswanya(kushoto), wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana,kulia ni Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mwanza ACP Augustino Senga akishuhudia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi,akizungumza na Mkurugenzi wa Kanda ya ziwa wa mtandao wa tigo Ali Maswanya(kushoto) jijini Mwanza jana,baada ya kupokea kompyuta na printa wakati wa hafla ya makabidhiano ,kulia ni Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mwanza ACP Augustino Senga akishuhudia.

Microsoft kuinunua Linkedin kwa Dola Bilioni 26.2

Microsoft kuinunua Linkedin kwa Dola Bilioni 26.2

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Kampuni ya Microsoft imetangaza kuwa inaununua mtandao wa kijamii wa LinkedIn kwa dola bilioni 26.2. Mtandao huo hadi sasa una watumiaji milioni 433 na hutumiwa zaidi kwa masuala ya kazi. Manunuzi hayo ni ya fedha taslimu.


Kwa Microsoft, LinkedIn itaipa fursa kubwa katika biashara ya mitandao ya kijamii hasa yenye maudhui ya masuala ya kazi na biashara. Mtandao huo hutumiwa zaidi na waajiri na waajiriwa na hivyo kampuni hiyo imepata sehemu ya kuuza zaidi bidhaa zake.
Mtandao wa LinkedIn upo katika zaidi ya nchi 200 duniani huku ikiwa na watumiaji hai zaidi ya milioni 105 kila mwezi na waliojiunga wakiwa milioni 433.

BODI YA FILAMU NCHINI KENYA YAISHINIKIZA Coca Cola KUFUTA TANGAZO

BODI YA FILAMU NCHINI KENYA YAISHINIKIZA Coca Cola KUFUTA TANGAZO

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Kampuni ya vinywaji vya Coca Cola imelazimika kulifanyia mabadiliko tangazo lake la biashara linalofahamika kama "Taste the feeling" kufuatia kuingiliwa kati na bodi inayodhibiti filamu nchini Kenya.

Bodi hiyo ambayo awali imelaumiwa kwa kukiuka mipaka yake, ilitangaza leo asubuhi kuwa Coca Cola italifanyia mabadiliko tangazo hilo kwa misingi ya kimaadili.

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya filamu ya bodi hiyo nchi Kenya Ezekiel Mutua, alisema kuwa tangazo hilo lilikosolewa na umma kutokana na picha za kubusiana ambazo zinatajwa kuwa za kukiuka maadili ya kijamii.

Mutua amesema kuwa baada ya kufanya mkutano na meneja wa Coca Cola nchini Kenya Nicholas Mruthu kampuni hiyo imekubali kuleta tangazo lingine lisilo na picha kama hizo.


Bodi hiyo pia imeonya makampuni ikiyataka yaheshimu maadili ya familia kutokana na kile yanayojumuisha kwenye matangazo ya biashara na muda ambao matangazo hayo yanapeperushwa .

KUTOKA KIJIWENI: ILI UFANIKIWE ACHA KUFANYA HAYA

KUTOKA KIJIWENI: ILI UFANIKIWE ACHA KUFANYA HAYA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
1. Acha tabia ya kuahirisha mambo.
  Kama kuna jambo au kitu unachotakiwa kukifanya leoleo ni vizuri ukafanya kuliko kukiacha na kutegemea utafanya kesho. Wakati wa kubadili maisha yako upo sasa na wala si kesho kama unavyofikiri. Hiyo kesho unayoisubiri haitafika na wala hakuna kesho kama unavyofikiri. Ni mara ngapi umesema utafanya kitu hiki kesho na hukufanya? Hii ni moja ya tabia inayokuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa unayoyataka. Unataka kuwa tajiri achana na tabia hii kwanza.

2. Acha tabia ya kufikiria sana makosa uliyoyafanya.
Wengi wanakuwa wanashindwa kusonga mbele kutokana na kufikiria sana makosa waliyoyafanya siku za nyuma. Kama kuna sehemu ulikosea, hiyo imeshapita chukua hatua sasa za kusonga mbele. Acha kuumia na kung’ang’ania kufikiri pale ulipokosea, hiyo haitakusaidia sana zaidi ya kukurudisha nyuma. Kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara kukosea ni sehemu ya maisha ya binadamu, kitu cha msingi jifunze kutokana na hayo makosa.

3. Acha tabia ya kuongelea sana ndoto zako.
Watu wengi sana ni waongeaji juu ya ndoto zao lakini sio watendaji. Kama ni kuongea umeongea sana juu ya ndoto zako, umefika sasa wakati wa kufanya mambo yako kwa vitendo. Jifunze kuchukua hatua dhidi ya ndoto zako kila siku, hata kama ni kwa kidogo kidogo utasogea, mwisho utajikuta unafanikisha kile unachokitaka. Hii ni tabia ambayo imekuwa ikiwakwamisha wengi kutokana na kuongea sana. Unataka mabadiliko achana na tabia hii.

4. Acha tabia ya kutokujiwekea akiba.
Hii ni tabia ambayo ukiiendeleza katika maisha yako kutojiwekea kipato itakuwa ni ngumu sana kwako kufanikiwa. Unaposhindwa kujiwekea kipato katika pesa unayoipata kitakachokutokea katika maisha yako, utashindwa kumudu kupata pesa ya kuendeshea miradi yako na mwisho wa siku utakuwa ni mtu wa kulalamika tu. Kama unataka kuwa tajiri na kuwa huru kifedha anza kujifunza kujiwekea akiba, hii itakusaidia sana kusonga mbele katika mambo yako mengi.

5. Acha kutumia pesa zako hovyo.
Watu wengi huwa ni watumiaji vibaya wa pesa zao hasa pale wanapozipata. Unapotumia pesa zako hovyo hiyo hupelekea kuweza kukosa pesa ambayo ungeweza kuipata kama akiba yako ya baadae. Mtumizi mabaya ya pesa, ni moja ya tabia kama tabia zingine, lakini ambayo inakukwamisha kwa kiasi kikubwa kufikia ndoto na malengo yako makubwa uliyojiwekea. Ili uweze kusonga mbele na kuachana na majuto uliyonayo jifunze kutunza pesa zako vizuri, utafanikiwa.

6. Acha tabia ya kuwa na madeni mengi.
Unapokuwa na madeni mengi hiyo itakusababishia badala ya kuendelea mbele utakuwa unarudi nyuma. Acha kulimbikiza madeni ambayo kwako yanakuwa mzigo kwako. Kabla hujakopa chukua hatua muhimu ya kujiuliza je, kuna ulazima wa kukopa hiyo pesa? Madeni ni kitu ambacho kimekuwa kinawarudisha wengi nyuma bila kujua, kutokana na kuwa na elimu ndogo inayohusiana na madeni. Unataka kuwa na mafanikio, iache tabia hii mara moja.

7. Acha tabia ya kusubiri sana kutekeleza ndoto zako.
Hakuna muda sahihi ambao upo wa kuanza kutekeleza ndoto zako kama unavyofikiri. Muda wa mafanikio na kufanya ndoto zako kuwa za kweli ni sasa na wala si kesho. Acha kuwa na tabia au fikra za kufikiri kuwa mipango yako mingi utaiyafanya siku nyingine, hakuna kitu kama hicho. Hii ni tabia ambayo umekuwa nayo na inakukwamisha. Unataka kutoka hapo ulipo anza kutekeleza mipango na malengo yako iliyojiwekea mara moja.

Kama una nia ya kweli kutaka kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yako, anza kujiandaa kubadilika wewe kwanza ikiwa ni pamoja na kubadili hizo tabia ulizonazo zinakukwamisha sana. Kwa kadiri, utakavyoweza kumudu kubadili tabia zako kwa kiasi kikubwa, ndivyo utakavyo jikuta maisha yako yanakuwa na mafanikio makubwa kuliko unavyofikiri. Kumbuka hili, mafanikio yanajengwa na tabia tulizonazo. (Ahsante JF)

TANZANIA: RC DAR ES SALAAM, SAID MECK SADIKI AZINDUA DUKA LA HUAWEI JIJINI DAR ES SALAAM

TANZANIA: RC DAR ES SALAAM, SAID MECK SADIKI AZINDUA DUKA LA HUAWEI JIJINI DAR ES SALAAM

No comments
By danielmjema.blogspot.com
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu , Samora jijini Dar es Salaam.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani juu duka la kuwapatia wananchi bidhaa zenye viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda sambasamba na mabadiliko ya teknolojia hivyo kuwapatia wateja wao simu za mkononi za kisasa,jijini Dar es Salaam.
  
Na Mwandishi Wetu,
Kampuni ya simu kutoka nchini China ya Huawei, imezidi kutanua wigo wa huduma kwa kuzindua maduka mawili ya simu moja likiwa jengo la JMall na duka la pili lenye Kituo cha huduma ya matengenezo ya simu za mkononi likiwa jengo la NHC karibu na TTCL mtaa wa Samora..

 Hii ikiwa ni baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei jijini Dar es Salaam na pia kuhakikisha kuwa vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.kwa ukaribu zaidi jijini la Dar es Salaam.

Maduka hayo ya Huawei yana mahali husika panapo ruhusu wateja wake kuangalia na kujaribu simu na vifaa vingine vya Huawei. Maduka hayo pia yanatoa nafasi nzuri kwa wateja kupata huduma bora na kuzoea bidhaa za Huawei na hata kwa kujaribu baadhi ya vifaa vyetu vya mtandao vyenye uwezo wa 3G/4G LTE Smartphone.

Maisha ya wateja wetu yana badilika kila siku na matarajio yao ni kuona ubora na ukuaji wa huduma katika kiwago cha juu zaidi. Kama wadau wakubwa Huawei imekuwa ikijitahidi katika kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja na pia kuahidi kuwaonyesha wateja thamani ya pesa yao. 

“Dar es salaam kama kitovu katika ukuaji wa uchumi, tunaamini maduka yetu ya simu na pia kituo cha matengenezo ya simu za mkononi yataongeza ufanisi na kusaidia ufikiaji wa huduma za mawasiliano kwa ukaribu Zaidi. Maduka yetu yamejikita katika ubora wa kutoa bidhaa kwa wateja wa rejareja na kuwapa wauzaji uwezo wa kupata vifaa halisi, bora na pekee”.

Maduka mapya ya Huawei, mbali na uuzaji wa Simu za mkonon , Pia  yatatoa huduma baada ya mauzo wataalam wa mauzo wataweza watatoa msaada wa  kifundi na utumiaji na matengenezo
Katika kusherekea ufunguzi huu wa maduka ya Huawei na kituo cha huduma za simu, Huawei inatoa punguzo la bei kuanzia tarehe 25 mpka tarehe 29 mwezi huu ikiwa pamoja na promosheni za simu zao P8 na G8. Manunuzi ya simu hizi mbili za P8 na G8 yataambatana na zawadi kama selfie stiki, spika za Bluetooth na tisheti.

Huawei Tanzania imejipanga kuhakikisha ina weza kuwafikia wateja wake wote Tanzania kote katika ubora na huduma zenye ufanisi Zaidi.

Maduka yetu yatakuwa yanatoa huduma itakayo fanya manunuzi yako yawe ya kihistoria, pia tupo kwenye msimu wa kuhakikisha uwepo wetu unajulikana Tanzania kwa ujumla kwa kuanza na Dar es salaam” aliongeza meneja wa Huawei nchini.

Maduka hayo yatatoa huduma siku zote za wiki saa 2 asubuhi hadi saa kumi na moja jioni jumatatu hadi Ijumaa na jumamosi yatakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa saba mchana. Maduka ya Huawei yatakuwa kwa ajili ya kuboresha utumiaji sahihi wa  teknolojia  katika njia sahihi zaidi, Wateja Wote mnakaribishwa 

Kuhusu Huawei
Huawei ni vinara wa teknolojia na mawasiliano hususani katika kutimiza matakwa ya wateja wao, katika kuhakikisha wanawapa wateja wao kile kilicho bora katika viwango vya juu, umuhimu wa mawasiliano na vifaa vya mawasiliano vinatumika katika nnchi Zaidi ya 170 na mikoa yake, Huawei ilishika nafasi ya 228 ulimwenguni kwa mwaka kutokana na mapato yake mwaka 2014 kati ya makampuni 500.

Mapato ya kampuni yamefikia kiasi cha dolla za kimarekani bilioni 46.5. Huawei imeshika nafasi ya 3 kwenye usambazaji wa simu kwa mwaka 2015 kwa kusambaza zaidi ya simu milioni 100 duniani kote, Kampuni ya Huawei ipo katika kuhakikisha inatoa ushirikiano katika kukuza na kuboresha vifaa vya mawasiliano  duniani kote.

Kampuni ya Huawei inajihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti kwa njia ya modemu na vifaa vya matumizi ya nyumbani. Huawei imeimarisha mahusiania ya biashara na makampuni kama Tigo, Vodacom, Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom.

Hotuba ya Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Peter Philip
Uongozi wa Huawei
Wadau mbalimbali wa Huawei
Waandishi wa Habari
Mabibi na Mabwana
------------------------------------------------------------------------------------------------------

Nina furaha kubwa kuwa miongoni mwenu leo pamoja na timu nzima ya Huawei. Katika dunia ambayo teknolojia ya mawasiliano inabadilika kwa kasi kushiriki  katika mabadiliko hayo ya maendeleo ni upendeleo mkubwa.

Mabibi na Mabwana, Christine Qiang mwana Uchumi wa Benki ya Dunia alisema” Wigo wa simu za mkononi unakuwa kwa kasi, ukiwa ni njia moja kuu ya kutanua fursa za kiuchumi na huduma za msingi kwa mamilioni ya watu” Kuunganishwa kupitia Intaneti au simu za mkononi kunaleta taarifa za masoko, huduma za kifedha na huduma za kiafya sehemu za mbali zisizofikika kiurahisi na ina saidia kubadilisha maisha ya watu kwa namna za kipekee.

Mabibi na Mabwana Ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza Huawei Tanzania kwa hatua hii nzuri katika kuendeleza sekta ya mawasiliano na teknolojia nchini Tanzania.

Sekta ya mawasiliano na teknolojia nchini Tanzania inakua kwa kasi na kuwa moja ya nguzo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Maendeleo haya ya kasi katika mawasiliano na teknolojia yamepelekea wawekezaji Wengi kuwekeza katika sekta hii nchini kwetu. Kwa sasa sekta hii inakua kwa kasi ya asilimia kumi na tano na asilimia ishirini kwa mwaka, kiwango ambacho kinaonyesha kua cha juu katika ukanda wa afrika mashariki.

Nchi Zaidi ya thelathini duniani hutengeneza simu za mkononi, hata hivyo ubora umekua alama ya utofautishaji katika makampuni haya ya simu. Kampuni ya Huawei imethibitisha mara kwa mara uwezo wao katika kuridhisha wateja wao kwa kuwapatia bidhaa zenye viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda sambasamba na mabadiliko ya teknolojia ivyo kuwapatia wateja wao simu za mkononi za kisasa.

Mabibi na Mabwana

Duka hili jipya na huduma matengenezo ya simu za mkononi la Huawei haliashirii ongezeko katika utajiri au mauzo yao ila inaashiria kutambua mahitaji ya wateja wao na fursa ya kupata bidhaa zenye uhakika na zilizo bora.

Nina Imani kuwa Huawei itaendelea kuwatosheleza wateja wake. Nchi ya Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi katika sekta ya teknolojia ivyo natumai na naamini Huawei watatumia fursa hiyo kuongoza soko la simu za mkononi nchini Tanzania.

Mabibi na Mabwana, Kwa mara nyingine nishukuru sana Uongozi mzima na menejimenti ya Huawei kwa kunishirikisha katika tukio hili tunapo fungua rasmi duka la Huawei na huduma za simu hapa J Mall.

Nina uhakika kila mteja atakae pita katika malango haya ya Huawei atapata kumbukumbu njema na mguso wa teknolojia ya uhakika.

Asanteni sana.

TANZANIA: WAFANYABIASHARA WA SUKARI WAPAMBANA NA RAIS MAGUFULI

TANZANIA: WAFANYABIASHARA WA SUKARI WAPAMBANA NA RAIS MAGUFULI

No comments
By danielmjema.blogspot.com

SASA ni wazi kwamba wafanyabiashara wa sukari nchini wameamua kuanzisha vita na Rais John Magufuli, kwa kuamua kuficha bidhaa hiyo na hivyo kuadimika katika soko na kupanda bei. Hatua hiyo ya wafanyabiashara imekuja baada ya Rais Magufuli kutangaza utaratibu mpya hivi karibuni wa kutaka uagizwaji wa sukari kutoka nje ufanywe na wazalishaji wa bidhaa hiyo hatua ambayo inakata mrija wao wa ulaji.

Jana Bodi ya Sukari ililazimika kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kile walichokibaini baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa bidhaa hiyo imeadimika. Akitoa tamko kwa niaba ya Bodi ya Sukari na wazalishaji bidhaa hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero, Ami Mpungwe, alisema tangu Rais Magufuli alipotangaza utaratibu mpya wa kuwatumia wazalishaji kuagiza sukari wamebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameanza kufanya mipango ya kuhujumu taratibu hizo.

Alisema wafanyabiashara hao wameamua kuficha bidhaa hiyo ili kuwaaminisha wananchi kwamba sababu kubwa ya kuadimika kwa sukari inachangiwa na uamuzi huo wa rais. Kabla ya uamuzi huo haujafikiwa na Rais Magufuli, wafanyabiashara wengi wa bidhaa hiyo walikuwa hawalipi kodi hali iliyochangia kufanya biashara hiyo kiholela huku wakipata faida nyingi na kuinyima mapato Serikali.

Hili linathibitishwa na kauli iliyotolewa na Mpungwe jana ambaye aliwanyooshea vidole waziwazi wafanyabiashara hao kwamba walikuwa wakinufaika na uingizaji holela wa sukari bila kulipia kodi na kwamba hata wanachokifanya sasa cha kupandisha bei ya sukari ni mbinu chafu ili kudhoofisha juhudi za Serikali za kuendeleza viwanda vya ndani kwa nia ya kujinufaisha wao binafsi.

“Wameanzisha kampeni za kuwatia hofu wananchi wakiwaonyesha sukari imeadimika kutokana na agizo lililotolewa na Serikali la kudhibiti uingizaji sukari nchini,” alisema Mpungwe. “Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuficha maghalani na kuendesha propaganda kwamba bei ya sukari imepanda na wapo waliopandisha kwa ghafla bei ya sukari kwa madai kwamba kuna upungufu viwandani na wengine wakiwalaghai watu kwamba bei wanayonunulia viwandani imepanda,” alisema Mpungwe na kusisitiza kuwa wanaofanya hujuma hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumzia utaratibu huu mpya alisema unafanyika kwa kuzingatia ulipaji kodi kwa sukari ya nje inayoingizwa nchini lakini pia umelenga kulinda viwanda vya sukari kwa kuimarisha soko la ndani.
Mwenyekiti huyo wa Bodi ya sukari nchini, alisema wazalishaji nchini wanatambua kwamba viwanda vyote vya wasambazaji vinauza sukari kati ya shilingi 1,700 na 1,800 kwa kilo na hakuna kilichopandisha bei tangu tamko la Rais lilipotoka.

“Hali ya uzalishaji sukari msimu huu 2015/2016 ni nzuri na msimu utafungwa Aprili kupisha matayarisho ya msimu mpya 2016/2017 Mei na Juni 2016 kama ilivyo taratibu kwa kila mwaka na viwanda vina akiba ya tani 32,000 za sukari inayoendelea kuuzwa,” alisema na kuongeza:

“Kiwanda cha sukari cha TPC kilichopo Moshi na kile cha Kagera vinaendelea kuzalisha sukari hadi Aprili 2016 na Serikali imeshatangaza utaratibu wa uagizaji wa sukari ambao utahakikisha sukari inayoruhusiwa kuingizwa nchini na kiasi kinachohitajika kuziba mahitaji ya wakati viwanda vinapokuwa vimefunga uzalishaji.”

Aliongeza kuwa kutokana na utaratibu huu mpya wa kuweka uwazi katika usimamizi wa bidhaa ya sukari, utasaidia kwa kiwango kikubwa kudhibiti sukari ya magendo na kuhakikisha inayoingia ni ile iliyoruhusiwa kwa kulipiwa kodi.

Mwenyekiti huyo alisema Bodi ya sukari na wazalishaji wanawahakikishia Watanzania kwamba hali ya upatikanaji wa sukari nchini ni nzuri na wao kwa kushirikiana na vyombo husika vya Serikali watahakikisha wanaendelea kuwa na sukari ya kutosha kwa muda wote.

KAULI YA RAIS MAGUFULI

Hivi karibuni Rais Magufuli alitoa kauli ya kupiga marufuku uingizwaji wa sukari kutoka mataifa ya kigeni ili kuvilinda viwanda vya sukari nchini ambavyo vimeathiriwa na uingizaji wa sukari ya bei rahisi kutoka nje.Rais huyo alisema Taifa haliwezi kufikia malengo yake ya kuimarisha viwanda vya ndani iwapo viwanda vya sukari nchini havitalindwa na kuwezeshwa dhidi ya uingizaji huo.

Rais Magufuli alielezea kuwepo kwa viwanda nchini ambavyo hununua miwa kutoka kwa wakulima wadogo wadogo na viwanda hivyo huzalisha sukari, lakini pia ajira ni chanzo cha mapato ya Serikali. Alisema ingawa ipo hifadhi ya kutosha ya sukari lakini wapo watu serikalini wanaotoa vibali vya kuingiza sukari kutoka nje.

Aliwaelezea watu hao kama ni sehemu ya kukandamiza juhudi za Serikali hali iliyosababisha kuchukua hatua ya kuzuia utolewaji wa vibali kuruhusu uingizaji wa sukari, hadi itakapotokea mahitaji maalumu. Alisema wapo baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu ambao wamekuwa wakiingiza sukari nchini iliyoisha muda wake wa matumizi na haifai kutumiwa na binadamu.

Mahitaji ya sukari nchini ni tani 420,000 ambako tani 170,000 zinatumiwa kwa mahitaji ya nyumbani na nyingine iliyobaki hutumiwa viwandani. Alisema viwanda vya hapa nchini vimekuwa vikizalisha tani 300,000 hali inayosababisha kuwepo kwa upungufu wa tani 290,000 kila mwaka kwa matumizi ya nyumbani na yale ya viwandani.

Chanzo: Mtanzania
Mwandishi: Shabani Matutu

TANZANIA: Bayport na Viwanja

TANZANIA: Bayport na Viwanja

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya wa mikopo ya viwanja vinavyotolewa na taasisi yao katika maeneo sita ambayo ni Kilwa, Bagamoyo, Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Morogoro. Kulia kwake ni Zahra Moore kutoka kwenye kampuni yao ya BlackWood na Mwanasheria wao Ntiiba Muganga. Picha na Story kwa Hisani ya Bayport Financial Services.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, imezindua miradi sita mipya ya mikopo ya viwanja katika maeneo ya Kibaha, Bagamoyo, Chalinze, Temeke, Kilwa na Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa utoaji huduma bora za viwanja baada ya ule wa Vikuruti kuungwa mkono Watanzania wengi.

Kuzinduliwa kwa huduma hizo mpya za viwanja huku wakiongozwa na Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Bertha Minga, kunatanua wigo wa urahisishaji wa maisha ya Watanzania, hususan katika suala la ardhi linalozidi kupanda thamani siku hadi siku, jambo linalohitaji juhudi za taasisi kama Bayport za kuwasaidia wananchi wake kupata maeneo ya makazi kwa utaratibu rahisi na nafuu.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bi Bertha Minga, aliyesimama akizungumza katika uzinduzi wa hudumaya viwanja inayotolewa na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, leo mchana katika Ukumbi wa Ramada Encore, Posta, jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwanasheria wa Kampuni ya BlackWood, Ntiiba Muganga na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa BlackWood Zahra Moore.

Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo mipya ya viwanja, Mkurugenzi Mkuu Bayport Financial Services, John Mbaha, alisema huduma zao zitakuwa na njia rahisi kwa ajili ya

fastjet yapunguza safari za Kilimanjaro - Nairobi

fastjet yapunguza safari za Kilimanjaro - Nairobi

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com


Dar es Salaam, Februari 17, 2016 - Fastjet imepunguza mtiririko wa safari zake  kwenye njia ya Kilimanjaro Tanzania na Nairobi Kenya kuanzia Jumatatu Februari 15, 2016.
Fastjet ambao awali walikuwa wanatoa safari za kila siku kwenye njia hii hivi sasa watakuwa wanafanya  safari kutoka Uwanja Ndege wa  Kimataifa wa Jomo Kenyatta hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mara mbili kwa wiki  siku za Ijumaa na Jumapili tu.




Mabadiliko ya  mtiririko wa safari utazifanya ndege za fastjet kuondoka Nairobi kila Ijumaa na Jumapili saa 5.40 na kutua Kilimanajaro saa 6.40 na safari ya kurudi ndege itaondoka Kilimanjaro saa 7.10 na kutua Nairobi saa 8.10.

Kupunguzwa kwa safari hizo kumetokana na kuwepo kwa mahitaji kidogo miongoni mwa wateja nyakati za wiki kutoka masoko yote mawili ya Kilimanjaro na Nairobi na hivyo kufanya safari za ndege za kila siku kutokuwa nzuri kibiashara  kwenye siku hizo.
Shirika hilo limesema kuwa lengo lake ni kurejesha safari hizo kwenye njia ya Kilimanjaro –Nairobi pindi tu wateja wake watakapohitaji.


Safari za kila siku za  kutoka Dar es Salaam na Kilimanjaro hadi Nairobi zilianza Januari 11, 2016. Mahitaji ya abiria kwa safari za ndege kwenye njia kubwa ya kibiashara kati ya majiji ya Dar es Salaam na Nairobi   ambayo kwa pamoja  yana idadi ya watu zaidi ya milioni nane yamekuwa ni ya kuridhisha na fastjet iko kwenye mawazo kuwa  ndege moja ni lazima iongezeke kwenye safari kati ya majiji haya miwili katika siku za usoni.

Matokeo ya safari za fastjet kwenda Nairobi kutoka Dar es Salaam yamekuwa ni makubwa ambako kunaelezwa na ukweli kuwa nauli zinazotolewa na mashirika ya ushindani kati ya  nchi hizo mbili zimeshuka kwa  kiwango cha hadi asilimia 40 tangu fastjet waanze safari zake.


Nauli za fastjet kwa kiwango kikubwa zipo chini kuliko zile zinazotozwa na mashirika mengine  kwa safari za moja kwa moja kati ya Nairobi/Dar es Salaam  ambapo nauli zinaanzia dola 80 kwa safari moja.

Nauli hizo hazijumuishi kodi ya serikali ambayo ni dola 49 kuondokea Tanzania na dola 40 kuondokea Kenya na hivyo fastjet kupendekeza wateja wake kufanya maandalizi mapema ili kutumia fursa hiyo ya tozo la nauli nafuu.

Hata hivyo fastjet inasisitiza kuwa  kupunguza safari kwenye njia kati ya Nairobi na Kilimanjaro kunafungua fursa ya kuongeza uwezo kwenye njia za kikanda zilizopo na hali kadhalika uwezekano wa kuzindua  njia nyingine mpya ya kikanda katika siku za karibuni.

JARIDA LA EUROMONEY LA UINGEREZA LATOA TUZO YA UFANISI KWA BENKI YA NMB TANZANIA

JARIDA LA EUROMONEY LA UINGEREZA LATOA TUZO YA UFANISI KWA BENKI YA NMB TANZANIA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto), akiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Tuzo ya Ufanisi wa kibenki nchini Tanzania iliyotolewa na Shirika la Euromoney la Uingereza  kwa benki hiyo ijulikanayo Euromoney 2015 Award for Excellence. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa benki hiyo, Joseline Kamuhanda.
 Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa benki hiyo, Joseline Kamuhanda (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

BENKI ya NMB imetajwa kuwa Benki bora Tanzania kwa mwaka 2015, na kujinyakulia tuzo ikiwa ni kwa miaka mitatu mfurulizo.

Tuzo hiyo ilitolewa jijini London nchini Uingereza na Jarida la Euromoney linalojihusisha na masuala ya fedha.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker alisema Jarida ilo huandaa hafla ya kuyatambua Zaidi ya Makundi 20 ya bidhaa za taasisi za kifedha, ili kutazama benki bora.

Alisema Tuzo hiyo huzitambua pia taasisi za kifedha duniani kote ambazo zimepata mafanikio ya hali ya juu katika shughuli zake, hasa kwa kuonesha ubunifu na kupata mafanikio ya kifedha kila mwaka.

Alifafanua kuwa kazi ya kutafuta washindi, ufanywa na  Jopo la wataalam kutoka mataifa mbalimbali na wenye utaalamu mbalimbali, ambao hupitia taarifa zinazowasilishwa na taasisi zote za kifedha duniani na kutangaza washindi.

"Katika miezi 12, benki ya NMB imeanzisha huduma mbali mbali za kibenki na hivyo kuendelea kuwafikia wateja wa huduma za kibenki kuanzia kuweka akiba, kutoa na kuchukua fedha mijini na vijijini"alisema

Bussemaker alitoa shukrani kwa wateja wa Benki hiyo, wafanyakazi na washika dau wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio hayo.

Aliongeza kuwa tuzo hiyo inaongeza kwenye hazina ya tuzo ambazo benki imezipata katika miezi 12 huku akizitaja baadhi kuwa ni benki bora ya mwaka kutoka jarida la Banker, Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wakiipa NMB tuzo ya mlipakodi anaefuata sharia katika taasisi za kifedha nchini. 

KONGAMANO LA KWANZA LA WANAWAKE WAFANYABIASHARA SOKONI TANZANIA LAFANYIKA JIJINI DAR LEO.

KONGAMANO LA KWANZA LA WANAWAKE WAFANYABIASHARA SOKONI TANZANIA LAFANYIKA JIJINI DAR LEO.

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Equality for  Growth (EfG), JaneMagigita akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Dar es salaam leo.
Ofisa Programu Dawati la Uangalizi wa Serikali wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hussein Sengu (kulia) akitoa mada katika Kongamano la siku mbili la Wanawake Wafanyabiashara Sokoni Tanzania lililofanyika Dar es Salaam leo. Kongamano hilo lililowahusisha wanawake kutoka mikoa tisa ya Tanzania Bara limeandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Japhet Makongo akizungumza na Wanawake wafanyabiashara waliohudhuria Kongamano hilo.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Sarah Mambea na Brenda Kharono.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo, kutoka kulia Mussa Mlawa,Susan Sitta na Munaa Abdalah.
Wafanyabiashara wanawake Masokoni wakiwa kwenye Kongano hilo.


Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (Repoa), Samwel Wangwe amewataka watanzania kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo hususani wanawake kwani wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa.

Akizunguza Dar es Salaam leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la kwanza la wanawake wafanyabiashara sokoni Tanzania, Wangwe alisema ni muhimu kuhakikisha wafanyabiashara hao wanawezeshwa na kuwajali katika uzalishaji na uendeshaji wa biashara zao.

Alisema kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi duniani katika sekta ya wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo kutoa changamoto kubwa katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya kisera.

"Wafanyabishara wadogo ni wengi sana hivyo wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa kutokana na uwepo wa asilimia 43 ya wajasiriamali wanawake Tanzania," alisema Wangwe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, alisema  lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wanawake wafanyabiashara walio sokoni kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa lengo la kuwajengea mshikamano na kujadili masuala muhimu yanayowahusu katika biashara zao.

Alisema kongamano hilo limehusisha wanawake 200 kutoka katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mtwara, Lindi, Mara, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, na mkoani Tanga katika Wilaya ya Lushoto huku wakiongozwa na kauli mbiu isemayo 'Sauti ya Mwanamke Sokoni'.

Alisema kauli hiyo inalenga kumkomboa mwanamke mfanyabiashara kwa kumjengea uwezo kutambua yeye ni nani na nafasi yake kama raia katika kuendesha shughuli biashara za shughuli za soko. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712-727062)

VODACOM NA TIGO WAUNGANA KUTOA HUDUMA BORA ZA KIFEDHA

VODACOM NA TIGO WAUNGANA KUTOA HUDUMA BORA ZA KIFEDHA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutia saini makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na kampuni yake kupitia huduma ya M-Pesa na Tigo kupitia huduma yake ya Tigopesa. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez.
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutia saini makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na kampuni yake kupitia huduma ya Tigopesa na Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa. Anaeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto, aliyekaa) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kulia, aliyekaa), wakitia saini mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na makampuni yao kupitia huduma ya M-Pesa na Tigopesa. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Vodacom Tanzania, Ngayama Matongo na kulia ni Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (wa pili toka kushoto) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, wakibadilishana nakala za mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na makampuni yao kupitia huduma ya M-Pesa na Tigopesa, wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Vodacom Tanzania, Ngayama Matongo na kulia ni Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga.

AIRTEL YAKABIDHI MAGARI MATATU KWA WATEJA WAO

AIRTEL YAKABIDHI MAGARI MATATU KWA WATEJA WAO

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akishangiliwa na wafanyabiashara wenzake sokoni hapo, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota 
IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana.

  
Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akikabidhi mfano wa ufunguo wa  gari kwa mshindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi, Grace Pascal Kalengela  wakati wa  kumkabidhi  gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika katika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni mume wa mshindi huyo, Daudi Mayunga na (kulia) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akiwa mwenye furaha, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783 
DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange.
Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akiwa mwenye furaha, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange.

VODACOM: WATANZANIA WANAENDELEA KUNUFAIKA NA HUDUMA NA GHARAMA NAFUU ZA MAWASILIANO.

VODACOM: WATANZANIA WANAENDELEA KUNUFAIKA NA HUDUMA NA GHARAMA NAFUU ZA MAWASILIANO.

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mkurugenzi Mtendaji waVodacom Tanzania Rene Meza, akiongea na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini hotuba aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (hayupo pichani) juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifuatilia kwa makini hotuba aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wao Rene Meza (hayupo pichani) kwa waandishi wa habari juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini hotuba aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (hayupo pichani) juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia akijibu waswali ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Rene Meza kuongelea juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni jijini Dar es Salaam jana. 

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .