Showing posts with label Jamii. Show all posts
Showing posts with label Jamii. Show all posts

Jamii Media na Kongamano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ICT

Jamii Media na Kongamano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ICT

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam (kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jamii Media, Asha Abinallah na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam. 


Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania inayoendesha mitandao ya JamiiForums na FikraPevu kwa kushirikiana na CIPESA(The Collaboration on International ICT Policy in East and Southern Africa) iliyo na makao makuu yake nchini Uganda imefanya Kongamano la kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini hasa wanaohusika moja kwa moja katika kulinda faragha za wateja wao ili kujadili masuala mbalimbali ya Huduma za Habari na Mawasiliano katika jukumu lao kuwa kiunganishi kati ya mteja na huduma watoazo pamoja na namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia huduma hizo.

Kabla ya kufanyika kwa Kongamano hilo siku ya Jumatano tarehe 12 Julai, Jamii Media ilifanya mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 10 hadi 11 Julai kwa vijana mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati na wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Mafunzo hayo yalilenga kujenga uelewa kuhusu sera zinazohusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Usalama wa Data Mtandaoni, Hali ya Uhuru Mitandaoni na Mambo yanayoathiri uhuru Mitandaoni nchini Tanzania.

Katika Kongamano hilo, Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Dawson Msongaleli kutoka kitengo cha Makosa ya Mtandaoni alifanya pia Uwasilishaji kuhusu Sheria ya Makosa Mtandaoni na kueleza kuwa Usiri na Usalama wa taarifa za watumiaji wa mtandao ni vitu viwili vinavyokanganya na kwamba inafika wakati ili kutekeleza kimoja inabidi misingi ya kingine ivunjwe.

Aidha, alibainisha kuwa kukosekana kwa kanuni za usimamizi wa Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) ni changamoto kubwa kwani inapelekea tafsri ya Sheria hiyo kubadilika kulingana na mazingira na mtu anayetafsiri kitu ambacho kinaathiri kazi yao kama watekelezaji wa Sheria na kuahidi kuwa mamlaka zinashughulikia chamgamoto hiyo.

Mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo alisema hili ni Kongamano la kwanza la aina hii kufanyika tangu kuanzishwa kwa JamiiForums miaka 11 iliyopita na limekuwa na matokeo chanya baada ya wadau kujadili kwa kina masuala mbalimbali yahusuyo usalama wa watumiaji. 
 
Aliongeza kuwa wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za kusimamia huduma nzima ya matumizi ya mitandao lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa huduma hizo.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kampuni yake itaendelea kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo wamiliki wa blogu na watumiaji wa kawaida wa mitandaonya kijamii ili kuhakikisha wanakuwa na matumizi mazuri ya huduma hiyo ili kupunguza mkanganyiko kwao na kuwapa fursa adhimu ya kunufaika na uwepo wa mitandao hiyo.

Mwisho


ONYO: UKIVUNJA AHADI YA NDOA NI UBAKAJI

ONYO: UKIVUNJA AHADI YA NDOA NI UBAKAJI

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Polisi nchini India wamemkamata mwanamume mmoja raia wa Scotland kwa madai ya ubakaji baada ya kuvunja ahadi ya ndoa na mwanamke aliyeshiriki ngono naye. Mtu huyo alituhumiwa kwa kosa hilo baada ya aliyekuwa mpenziwe kumshataki kuwa amevunja ahadi ya kufunga ndoa.

Mwanamme huyo alikuwa akifanya kazi kwenye ukumbi wa mazoezi mjini Delhi na inaarifiwa kuwa alikuwa katika uhusiano na mwanadada huyo kwa muda wa miezi 5. Baada ya mwanamme huyo kuvunja uhusiano kati yao, mwanadada huyo alimshtaki.

Anasema kuwa aliitikia kushiriki mapenzi naye kwani mwanamme huyo alimwarifu kuwa angemwoa. Mwanamume huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka kumi gerezani iwapo atapatikana na hatia na mahakama ya nchi hiyo.

India iko katika njia panda kuhusiana na mabadiliko ya maadili na mtazamo dhidi ya kushiriki mapenzi nje ya ndoa. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kesi kadha zinazokabiliana na kuvunjwa kwa ahadi ya ndoa na kuibua swali iwapo ni kosa la ubakaji ukishiriki ngono na mwanamke kisha uvunje ahadi ya kumuoa.

SEREKALI YAOBWA KUPITIA UPYA SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 1971 KWANI INAWAATHIRI WATOTO WENGI

SEREKALI YAOBWA KUPITIA UPYA SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 1971 KWANI INAWAATHIRI WATOTO WENGI

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com


mwenyekiti wa baraza la watoto wilaya ya Arusha Hassani Omary akizungumza wakati wa kongamano la  watoto ,walimu ,wazazi lililoandaliwa na shirikala intiative for youth (INFOY) kongamano lililofanyika ndani ya shule ya msingi ya uhuru jijini hapa



 baadhi ya wanafunzi ,wazazi na walimu waliouthuria katika kongamano hilo

mmoja wa mwanafunzi aliyeuthuria akieleza mathara ya mimba za utotoni
Na Woinde shizza, Arusha

Serekali  imetakiwa kuangalia upya sheria ya  mtoto ya mwaka 1971 kwani ndio  imebainika kuwa ndio chanzo kimoja wapo kinachoruhusu na kungangia ndoa za utotoni pamoja na mimba za utotoni.
Akizungumza wakati  katika wa kongamano lililoandaliwa na shirika laintiative for youth (INFOY  )  mwenyekiti wa baraza la watoto wilaya ya Arusha Hassani Omary alisema kuwa ni wajibu wa serekali kuangalia upya sherika hii kwani sheria hii imekuwa ikiwaadhiri watoto wengi hapa nchini.

Alisema kuwa sheria hii imekuwa ikiruhusu watoto hata wenye umri chini
ya miaka 18 kuolewa  iwapo tu wazazi wake watakapo kubali kitu ambacho
kinawaathiri watoto wengi katika masomo yao kwani wamekuwa
wanakatishwa masomo yao  na  iwapo akitokea mtu mmoja kupeleka lala
miko lake katika vyombo vya sheria amekuwa akishindwa kutokana na
sheria hii inaruhusu mtoto huyo ata awe mdogo kuolewa mradi tu familia
yake iwe imeafiki.

Aidha aliongeza  kuwa  mbali na sheria hii pia serekali ikinatakiwa
kutilia  mkazo sana katika mila mbalimbali na desturi zetu kwani mila
zingine zimekuwa zikichangia pia kwa kiasia kikubwa watoto wadogo
haswa wakike kukosa haki zao za msingi kwa kuwalazimisha kuolewa iwapo
tu viongozi wa mila zao wakitaka huku akitolea mfano kwa kwa kabala la
kimasai ambalo linaishi hapa Arusha na kudai kuwa wamekuwa wakisimamia
na kulazimisha watoto wao kuolewa pindi tu pale atakapo kuwa amevunja
ungo tu au pale atakapo uonekana amekuwa kidogo.

 Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa  kulinda  na kutetea haya ya
sheria ya mtoto Laurent Sabuni alisema kuwa ni wajibu wa serekali
kutaangalia kwa makini sheria hii kwani imekuwa ikiweaathiri watoto
kwa kiasi kikubwa  kwa kuwakosesha haki zao .

Alisema kuwa  kumekuwepo na matatizo  ya watoto wadogo kupata mimba za
utotoni kutokana na pale wanapopeleka mashitaka katika vyombo vya
sheria  ,sheria hii imekuwa ikiwatetea wahalifu  hali ambayo imekuwa
ikiwapelekea watoto kukata hata tamaa ya kwenda kushitaki katika
vyombo vya sheria.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii  manispaa ya Arusha Saum Kweka
alisema kuwa  katika kipindi hichi ni wajibu wakila mzazi kuhakikisha
anamlinda mtoto wake anampa elimu mtoto wake kuhusiana na mimba za
utoton.
 
Alisema kuwa kumekuwepo na watoto wengi wanapewa mimba wakiwa wadago
lakini kutokana na kutopata ushauri kutoelimishwa kutokaa karibu na
wazazi wao hivyo ni wajibu wa kila mzazi kuahakikisha anamuelimisha
mtoto wake kuhusiana na mazingira yanayomzunguka.


Aidha saum alisema kuwa ni wajibu wa kila mzazi kutambua kuwa
kumuozesha mtoto mdogo ni hatari na pia ni ukiukwaji wa sheria ,pia ni
kumkosesha haki za msingi mtoto hivyo ni wajibu wa kila mzazi kupiga
vita vikali  ndoa za utotoni pamoja na mimba za utotoni huku akigusia
kwa kusema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni tokomeza mimba na ndoa za
utotoni sote kwa pamoja tunaweza.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA UKUMBI WA CHAKULA ULIOFADHILIWA NA TANAPA

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA UKUMBI WA CHAKULA ULIOFADHILIWA NA TANAPA

Posted in ,
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Rombo mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari Olele iliyopo kata ya Olele kwa ajili ya kukabidhi Mradi wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa , Tanzania (TANAPA).
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakifurahia nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanafunzi wa shule ya  sekondari ya Olele wakati alipofika kwa ajili ya uzinduizi na makabidhiano rasmi ya ukumbi wa chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
RC ,Gamana iongozi wengine wakiskiliza nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na kwaya ya shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Kutokana na hali ya mvua iliyokuwepo wakati wa makabidhiano ya ukumbi wa chakula,mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama alilazimika kubadili meza kuu na wao wakaa eneo ambalo pia lilikuwa na mvua huku akisema ni vyema mvua ikawanyeshea wote pamoja na wananchi.
Jengo la Ukumbi wa Chakula lililojengwa kwa ufadhili wa Shirika la  Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Meneja Ujirani Mwema kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ahmed Mbugi akitoa taarifa kuhusiana na ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari Olele.
Baadhi ya wananchi katika kata ya Olele. 
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania,TANAPA,Ibrahim Musa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mradi wa ujirani mwema wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
RC,Gama na DC,Kipuyo wakilowa kutokana na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Wanafunzi katika shule ya sekondari Olele wakifuatilia hotuba ya viongozi waliofika shuleni hapo kwa ajili ya makabidhiano ya ukumbi wa chakula uliojengwa na TANAPA.
Mkuu wa wilaya ya Rombo ,Lembris Kipuyo akizungumza katika hafla hiyo.
Wakazi wa kata ya Olele.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akihutubia wananchi waliofika katika hafla fupi ya makabidhiano ya ukumbi wa chakula uliojengwa katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro ,Leonidas Gama akikagua jengo hilo.
Na Dixon Busagaga wa Globu aya Jamii Kanda ya Kaskazini.

NASSARI ASHIRIKI UJENZI WA CHANZO CHA MAJI KIJIJI CHA KARANGAI KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

NASSARI ASHIRIKI UJENZI WA CHANZO CHA MAJI KIJIJI CHA KARANGAI KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

Posted in ,
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar aiwa amepanda kwenye Lori lililokuwalikibeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji kwa ajili ya kumwagilia katika kijiji cha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akishirikiana na wananchi katika kijiji cha Karangai kuweka mawe katika chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Mbunge Nassar akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo hilo.
Mbunge Joshua Nassar akizungumza na mmoja a wanakiji cha Karangai huku akiwa amembea mtoto muda mfupi baada ya kumaliza hatua za awali za uwekaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Mbunge Joshua Nassar akizungumza na baadhi ya kina mama ambao mingoni mwao wanajishughulisha na shughuli za kilimo alipotembelea kijiji cha Karangai kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya umagiliaji katika kijiji hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

KONGAMANO LA KWANZA LA WANAWAKE WAFANYABIASHARA SOKONI TANZANIA LAFANYIKA JIJINI DAR LEO.

KONGAMANO LA KWANZA LA WANAWAKE WAFANYABIASHARA SOKONI TANZANIA LAFANYIKA JIJINI DAR LEO.

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Equality for  Growth (EfG), JaneMagigita akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Dar es salaam leo.
Ofisa Programu Dawati la Uangalizi wa Serikali wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hussein Sengu (kulia) akitoa mada katika Kongamano la siku mbili la Wanawake Wafanyabiashara Sokoni Tanzania lililofanyika Dar es Salaam leo. Kongamano hilo lililowahusisha wanawake kutoka mikoa tisa ya Tanzania Bara limeandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Japhet Makongo akizungumza na Wanawake wafanyabiashara waliohudhuria Kongamano hilo.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Sarah Mambea na Brenda Kharono.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo, kutoka kulia Mussa Mlawa,Susan Sitta na Munaa Abdalah.
Wafanyabiashara wanawake Masokoni wakiwa kwenye Kongano hilo.


Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (Repoa), Samwel Wangwe amewataka watanzania kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo hususani wanawake kwani wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa.

Akizunguza Dar es Salaam leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la kwanza la wanawake wafanyabiashara sokoni Tanzania, Wangwe alisema ni muhimu kuhakikisha wafanyabiashara hao wanawezeshwa na kuwajali katika uzalishaji na uendeshaji wa biashara zao.

Alisema kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi duniani katika sekta ya wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo kutoa changamoto kubwa katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya kisera.

"Wafanyabishara wadogo ni wengi sana hivyo wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa kutokana na uwepo wa asilimia 43 ya wajasiriamali wanawake Tanzania," alisema Wangwe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, alisema  lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wanawake wafanyabiashara walio sokoni kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa lengo la kuwajengea mshikamano na kujadili masuala muhimu yanayowahusu katika biashara zao.

Alisema kongamano hilo limehusisha wanawake 200 kutoka katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mtwara, Lindi, Mara, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, na mkoani Tanga katika Wilaya ya Lushoto huku wakiongozwa na kauli mbiu isemayo 'Sauti ya Mwanamke Sokoni'.

Alisema kauli hiyo inalenga kumkomboa mwanamke mfanyabiashara kwa kumjengea uwezo kutambua yeye ni nani na nafasi yake kama raia katika kuendesha shughuli biashara za shughuli za soko. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712-727062)

Makampuni, Wachimbaji madini watakiwa kuzingatia Sheria za Mazingira

Makampuni, Wachimbaji madini watakiwa kuzingatia Sheria za Mazingira

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

 Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta (Mb) aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani, akimsikiliza  Mhandisi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Ephraim Mushi wakati alipotembelea banda la Wizara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea  katika viwanja vya Tangamano jijini  Tanga.
 Wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali jijini Tanga, wakiangalia madini ya ujenzi wakati walipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea  katika viwanja vya Tangamano jijiji Tanga.
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Mhe. Stephen Masele, akiongea jambo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Innocent Makomba (kulia) akiwaeleza akiwaonesha wananchi waliofika katika Banda la Wizara ya Nishati na Madini madini ya ujenzi  aina  Uranga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Dunian yanayoendelea katika Viwanja vya Tangamano Jijijini Tanga.
Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta (Mb) aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani, akisalimiana na wananchi na watumishi wa sekta mbalimbali baada ya kuwasili katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga kufungua maonesho ya Siku ya Mazingira .

Na Asteria Muhozya, Tanga.

Kampuni za uchimbaji madini, utafutaji mafuta na gesi wakiwemo wachimbaji wadogo nchini, wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za uhifadhi wa mazingira wakati wanapotekeleza shughuli zao, ili kuwezesha rasilimali zinazopatikana  ardhini ziweze kuwa endelevu  kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Rai hiyo imetolewa na   na Mhandisi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ephraim Mushi wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani yanayoendelea kufanyika  katika viwanja vya Tangamano  Jijini, Tanga.
Mhandisi Mushi ameeleza kuwa, kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu duniani hususan katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania    ni muhimu mahitaji yao yakaenda sambamba na rasilimali zilizopo.

“Nafahamu uelewa wa makampuni ya uchimbaji madini na utafutaji wa mafuta na gesi katika usimamizi na kutunzaji wa mazingira ni mkubwa, kwani tayari  kampuni hizo zina mpango wa usimamizi mazingira ambao umeeleza masuala yanayopaswa kuzingatiwa, lakini bado wanapaswa kuzingatia jambo hili wakati wote kutokana na umuhimu wa wake”, alieleza Mushi.

Kuhusu wachimbaji wadogo ameeleza kuwa, bado wanafanya shughuli zao za uchimbaji bila kuzingatia sheria na kanuni za usimamizi wa mazingira. “Wachimbaji wadogo bado hawazingatii suala hili lakini Wizara inafanya jitihada mbalimbali za mara kwa mara kuhakikisha wachimbaji wanafuata taratibu ikiwemo kuwaelimisha kuhusu usalama na mazingira”,aliongeza.

 Hivyo, amewataka wachimbaji wadogo kuwa na mpango wa utunzaji mazigira kwa kuwa utaonesha namna ya  kuhifadhi na kutunza mazingira na hivyo kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na kanuni husika.

Akieleza zaidi kuhusu jitihada zinazofanywa na wizara katika kusimamia masuala ya   uhifadhi na utunzaji wa mazingira, hususan katika sekta za nishati na madini,  ameeleza kuwa, Wizara imeshatoa mafunzo kadhaa kuhusu masuala hayo kwa maafisa mazingira mazingira wa halmashauri katika Wilaya mbalimbali za  mikoa ya Mwanza, Iringa  na Mbeya kuhusu sheria na kanuni za madini na athari za uchimbaji usiozingatia uhifadhi mazingira.

Vilevile ameongeza kuwa,  wizara mafunzo mengine ni pamoja na mpango kazi wa mazingira wa wizara ambapo maafisa mazingira hao wanatakiwa kuingiza masuala ya madini kwenye mpango kazi yao. Mafunzo hayo pia yanatarajiwa kuendelea kufanyika katika miningine katika mwaka wa fedha ujao.

Aidha, ameeleza  kuwa, wizara imekuwa ikishirikiana na taasisi kadhaa zenye uhusiano wa masuala mazingira kama vile Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira  (NEMC) na wizara nyingine katika masuala yanayohusu  miradi ya nishati na madini jambo ambalo limeleta matokeo mazuri kwa kuwa miradi yote ya nishati na madini haiwezi kuanza   bila kufanyiwa tathmini ya athari kwa mazingira.

Siku ya mazingira duniani huazimishwa kila mwaka tarehe 1 - 5 Juni, ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yanaongozwa na kaulimbiu  Ndoto Bilioni  Saba. Dunia Moja. Tumia Rasilimali kwa Uangalifu”. Aidha, maonesho hayo yalifunguliwa  rasmi na tarehe 1 Mei,2015, na Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta  (Mb)kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal.
 
Chanzo: Matukio Michuzi Blog

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

    Zilizo Somwa Zaidi

Proudly Powered by EAMG .