Jamii Media na Kongamano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ICT
Posted in
Jamii
No comments
Saturday, July 15, 2017
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
Kampuni
ya Jamii Media ya Tanzania inayoendesha mitandao ya JamiiForums na
FikraPevu kwa kushirikiana na CIPESA(The Collaboration on International
ICT Policy in East and Southern Africa) iliyo na makao makuu yake nchini
Uganda imefanya Kongamano la kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (ICT) nchini hasa wanaohusika moja kwa moja katika
kulinda faragha za wateja wao ili kujadili masuala mbalimbali ya Huduma
za Habari na Mawasiliano katika jukumu lao kuwa kiunganishi kati ya
mteja na huduma watoazo pamoja na namna ya kulinda usiri wa taarifa za
wateja wanaotumia huduma hizo.
Kabla
ya kufanyika kwa Kongamano hilo siku ya Jumatano tarehe 12 Julai, Jamii
Media ilifanya mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 10 hadi 11 Julai
kwa vijana mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati na wadau wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Mafunzo hayo yalilenga kujenga
uelewa kuhusu sera zinazohusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,
Usalama wa Data Mtandaoni, Hali ya Uhuru Mitandaoni na Mambo
yanayoathiri uhuru Mitandaoni nchini Tanzania.
Katika
Kongamano hilo, Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Dawson
Msongaleli kutoka kitengo cha Makosa ya Mtandaoni alifanya pia
Uwasilishaji kuhusu Sheria ya Makosa Mtandaoni na kueleza kuwa Usiri na
Usalama wa taarifa za watumiaji wa mtandao ni vitu viwili
vinavyokanganya na kwamba inafika wakati ili kutekeleza kimoja inabidi
misingi ya kingine ivunjwe.
Aidha,
alibainisha kuwa kukosekana kwa kanuni za usimamizi wa Sheria ya Makosa
ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) ni changamoto kubwa kwani
inapelekea tafsri ya Sheria hiyo kubadilika kulingana na mazingira na
mtu anayetafsiri kitu ambacho kinaathiri kazi yao kama watekelezaji wa
Sheria na kuahidi kuwa mamlaka zinashughulikia chamgamoto hiyo.
Mara
baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Jamii Media, Bw.
Maxence Melo alisema hili ni Kongamano la kwanza la aina hii kufanyika
tangu kuanzishwa kwa JamiiForums miaka 11 iliyopita na limekuwa na
matokeo chanya baada ya wadau kujadili kwa kina masuala mbalimbali
yahusuyo usalama wa watumiaji.
Aliongeza kuwa wadau wengi kwenye
kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za kusimamia
huduma nzima ya matumizi ya mitandao lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa
fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa
watumiaji wa huduma hizo.
Mkurugenzi
huyo aliongeza kuwa kampuni yake itaendelea kutoa mafunzo kwa wadau
mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo wamiliki wa blogu na
watumiaji wa kawaida wa mitandaonya kijamii ili kuhakikisha wanakuwa na
matumizi mazuri ya huduma hiyo ili kupunguza mkanganyiko kwao na kuwapa
fursa adhimu ya kunufaika na uwepo wa mitandao hiyo.
Mwisho
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :