MBIO ZA NYIKA TAIFA ZIMEFANYIKA LEO MJINI MOSHI; ARUSHA WATESA
Posted in
No comments
Sunday, March 10, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
DICKSON MARWA AKIMALIZA
WANARIADHA WA KILOMETA 12 KATUIKA MBIO ZA NYIKA
WANARIADHA WA KILOMETA 12 WALIPOANZA KUTIMUA MBIO
MBIO za Taifa za
Nyika zimefanyika leo, mjini Moshi katika viwanja vya gofu za Moshi Club na
kushuhudia wanariadha kutoka katika mkoa wa Arusha wakitawala mbio hizo kwa
kuchukua nafasi za mwanzo katika mbio za kilomita 12, 8 na 6 zilizoshirikisha
wakimbiaji 100.
Katika mbio za
utangulizi za kilomita 6 wanawake , Anjeline Irene 21:19;57, Selina Amosi
21:31:86, Fadhila Salum wote kutoka Arusha mbio za km 8 wanawake Jaeldine
Sakilu (JWTZ-Arusha) 27:00:34, Zakia Mrisho
(Arusha) 27:24:58 na Catherine Lange (Manyara) 28:12:91.
Katika upande wa
wanaume km 8, Dotto Ikangaa 23:53:95 JWTZ-Arusha, Joseph Theophil Mbulu
23:56:41 na Mohammed Ally 24:13:54 JWTZ- Arusha huku mbio za km 12 wanaume
akichukua Dickson Marwa 36:34:52 kutoka Holili-Kilimanjaro.
Awali akizungumza
na waandishi wa habari mapema kabla ya kuanza kwa mbio hizo, Rais wa Shirikisho
la Riadha Taifa, (RT), Anthony Mtaka alisema kuwa madhumuni ya mbio hizo, ni kuandaa
kikosi kitakacho iwakilisha Taifa katika mbio za Nyika za dunia zitakazofanyika
Machi 24, nchini Poland
pamoja na kuibua vipaji vya riadha nchini.
Mtaka amesema kuwa
sababu za kuhamishia mbio hizo mkoani Kilimanjaro ni kutokana na mdhamini waliyempta
hapo awali kujiondoa na hivyo kuwalazimisha kutafuta mdhamini mwengine ambapo
alisema, Executive Solution walisaidia sana.
Rais Huyo amesema
kuwa RT kwa sasa inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo la udhamini na
kuongeza kuwa mbio hizo kwa mkoa wa Morogoro kujiondoa na hivyo wakalazimika
kutafuta namna ya kufanikisha mbio msaada ambao alisema waliupata kutoka kwa
uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumzia
juhudi za RT kuokoa riadha nchini, Mtaka amesema kwa sasa wameshaanda programu
ya kukuza vipaji ambapo alisema kuwa tayari kuna vijana 12 ambao wameshawaombea
katika chuo cha polisi ili kuhakikisha wanakuwa pamoja kambini na lengo ni kufuta
uteja katika riadha.
Kuhusu tatizo la
maandalizi ya timu ya taifa ya Riadha ambapo kwa miaka mingi watu wamekuwa
wakiilalamikia RT, Mtaka amesema kuwa wao kama RT hawana timu, wao majukumu yao ni wasimamizi wa timu
na kuhakikisha kuwa timu inapata huduma zote kabla ya mashindano.
Nao baadhi ya
wanariadha walioshiriki mbio hizo, Jaeldine Sakilu, aliyeshinda mbio za km 8
wanawake na Dickson Marwa, aliyeshinda mbio za km 12 wanaume, wamesema wako
tayari kuiwakilisha nchi katika mbio za Poland lakini walisisitiza umuhimu wa
kuwepo kwa maandalizi na ushirikiano kutoka kwa wadau wa Riadha.
Jumla ya
wakimbiaji wapatao 100 kutoka katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Manyara, Singida,
Mara, Zanzibar,
mbeya, Dar es salaam na kilimanjaro walichuana jana katika mbio za Nyika za
taifa zilizofanyika katika uwanja wa gofu wa Moshi Club ulioko katika Manispaa
ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo mshindi wa kwanza alipokea zawadi ya Sh.
60,000.
MWISHO.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :