ONYO: UKIVUNJA AHADI YA NDOA NI UBAKAJI
Posted in
Jamii
No comments
Wednesday, February 17, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Polisi nchini India wamemkamata
mwanamume mmoja raia wa Scotland kwa madai ya ubakaji baada ya kuvunja
ahadi ya ndoa na mwanamke aliyeshiriki ngono naye. Mtu huyo alituhumiwa kwa kosa hilo baada ya aliyekuwa mpenziwe kumshataki kuwa amevunja ahadi ya kufunga ndoa.
Mwanamme huyo alikuwa akifanya kazi kwenye ukumbi wa mazoezi mjini Delhi na inaarifiwa kuwa alikuwa katika uhusiano na mwanadada huyo kwa muda wa miezi 5. Baada ya mwanamme huyo kuvunja uhusiano kati yao, mwanadada huyo alimshtaki.
Anasema kuwa aliitikia kushiriki mapenzi naye kwani mwanamme huyo alimwarifu kuwa angemwoa. Mwanamume huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka kumi gerezani iwapo atapatikana na hatia na mahakama ya nchi hiyo.
India iko katika njia panda kuhusiana na mabadiliko ya maadili na mtazamo dhidi ya kushiriki mapenzi nje ya ndoa. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kesi kadha zinazokabiliana na kuvunjwa kwa ahadi ya ndoa na kuibua swali iwapo ni kosa la ubakaji ukishiriki ngono na mwanamke kisha uvunje ahadi ya kumuoa.
Habari Zingine
- Jamii Media na Kongamano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ICT
- ONYO: UKIVUNJA AHADI YA NDOA NI UBAKAJI
- SEREKALI YAOBWA KUPITIA UPYA SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 1971 KWANI INAWAATHIRI WATOTO WENGI
- MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA UKUMBI WA CHAKULA ULIOFADHILIWA NA TANAPA
- NASSARI ASHIRIKI UJENZI WA CHANZO CHA MAJI KIJIJI CHA KARANGAI KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :