MWALIMU NDIYE MLIPUAJI WA NDEGE SOMALIA
Posted in
afrika mashariki
No comments
Wednesday, February 17, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
![]() |
Tundu lililosababishwa na mlipuko huo |
Mwalimu mmoja wa shule ya Madrasa,
ametambuliwa kuwa mshukiwa aliyetekeleza shambulio la bomu ambalo
lilisababisha shimo kubwa katika tanki ya mafuta ya ndege moja ya abiria
nchini Somalia, iliyokuwa ikielekea nchini Djibouti, tarehe mbili
Februari mwaka huu.
Abdullahi Abdisalam Borleh, alirushwa na
mlipuko uliotokea katika ndege hiyo aina ya Airbus 321, wakati bomu hilo
lilipolipuka muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka uwanja wa
ndege wa Mogadishu.
Maafisa wa idara ya ujasusi wanaamini kuwa
Borley, ambaye anatoka eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland,
alibeba bomu hiyo kimakusudi.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab, lilidai kuhusika na
mlipuko huo, lakini halijatoa majina ya waliohusika moja kwa moja.
Hamna aliyeuawa wakati wa mlipuko huo, ambao ulitokea dakika kumi na tano baada ya ndege hiyo kupaa. Ndege hiyo ililazimika kurejea na kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Mogadishu nchini Somalia.
Habari Zingine
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :