Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

Katumbi ashitakiwa kwa kuajiri Mamluki

Katumbi ashitakiwa kwa kuajiri Mamluki

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mmiliki wa TP Mazembe aliyetangaza kugombea wadhifa wa Urais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Moise Katumbi (pichani kulia) ameshtakiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni,msemaji wa serikali amesema kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Bw Katumbi alitangaza wiki mbili zilizopita kwamba atawania urais katika uchaguzi wa mwezi Novemba. Msemaji wa serikali Lambert Mende aliambia AFP kwamba agizo la kukamatwa kwa Katumbi ambaye ndiye mmiliki wa kilabu ya TP Mazembe tayari limetolewa.
Bwana Katumbi awali alikana madai kwamba amekuwa akiwaajiri mamluki wa kigeni kuwa ya uongo na kwamba yalilenga kumzuia kuwania urais katika uchaguzi unaotarajiwa nchini humo.
Haijulikani iwapo uchaguzi utafanyika mnamo mwezi Novemba na iwapo rais Joseph Kabila anapanga kuondoka uongozini baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

RAILA AKIFANYA HAYA ATASHINDA URAIS, UCHAGUZI MKUU 2017.

RAILA AKIFANYA HAYA ATASHINDA URAIS, UCHAGUZI MKUU 2017.

No comments
By danielmjema.blogspot.com
KENYA inajiandaa kuingia katika uchaguzi mkuu mwaka 2017, ambayo inatarajiwa kufanyika mapema mwezi Agosti ambapo mchukuano mkali unatarajiwa kuwa kati ya muungano wa Jubilee ya Rais Uhuru Kenyatta na muungano wa CORD inayoongozwa na Raila Odinga.
 
Kwa muda mrefu sasa, Raila Amollo Odinga, amekuwa akitoa upinzani mkubwa kwa chama tawala, lakini kwa bahati mbaya, mara zote amejikuta akishindwa kutimiza ndoto yake ya kuingia Ikulu. 



Ndani ya CORD, kuna mvutano mkubwa wa nani anastahili kupeperusha bendera ya muungano huo dhidi ya muungano wa Jubilee unaoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, itakapotimu Agosti mwakani.

Raila wa Orange Democratic Party ambaye mwaka 2013 alishindwa na Uhuru Kenyatta tayari ameonesha nia ya kukiuka makubaliano (MOU) ya muungano wa CORD ambayo inadaiwa ilieleza wazi kuwa endapo Raila angeshinda (2013), angehudumu kwa kipindi kimoja na kumpa pasi Kalonzo Musyoka wa Wiper.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, uchaguzi wa mwaka ujao, ni Kalonzo ndiye anayestahili kupeperusha bendera ya CORD, lakini wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa Ford Kenya, ambayo ni chama tanzu ndani ya muungano wa CORD, naye ametangaza nia ya kukaa meza kuu.


Hizo zinaitwa 'Sihasa' za Siasa. ikiwa ni mwaka wake wa mwisho (umri umemtupa mkono) kugombea nafasi hiyo nyeti katika uongozi wa taifa hili, Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga anapaswa mambo kadhaa endapo anamatumaini ya kumrithi Uhuru Muigai Kenyatta.
  Kama nilivyosema hapo awali uchaguzi mkuu ujao, utakuwa wa mwisho kwa Raila katika juhudi zake za kuingia Ikulu. Haitakuwa kazi rahisi, itakuwa ni kazi ngumu kuliko uchaguzi uliopita.

Rais Uhuru Kenyatta kwa sasa ana umaarufu mara mbili ya alivyokuwa mwaka 2013 na ana 'advantage' nyingine ambayo ni uwepo wake madarakani. Anaingia katika Uchaguzi ujao akiwa na uzoefu wa kazi (urais) wa miaka mitano, hii inampa kiburi cha kushinda zaidi ya alivyokuwa wakati anatafuta njia ya kuelekea Ikulu.

Wakati Uhuru akiwa na uzoefu wa miaka mitano kama Rais, Raila yeye ana uzoefu wa miaka mitano kama  Waziri Mkuu hivyo kwa mtazamo wa haraka haraka, mafahali hawa wawili wana sifa sawa. hapa ndipo sasa Wakenya watakapohitaji kitu kingine cha ziada cha kuwashawishi kumpigia Raila kura na sio Uhuru.

Mbali na uzoefu alionao, kitu kingine kinachomfanya Uhuru awe na kiburi, ni sapoti aliyonayo kutoka ndani ya Muungano wa Jubilee huku pia kukiwa na hali ya utulivu tofauti na Raila ambaye mpaka sasa bado hana uhakika wa asilimia 100 ya sapoti ya Muungano wa CORD, kwani wote watatu wanataka (Raila, Kalonzo na Wetangula).


Ningekuwa Raila, huu ndio ungekuwa muda wa kufanya kazi kwa juhudi zangu zote kuwashawishi Wakenya ni kwanini nafaa kuwa Rais na sio Wetangula, Kalonzo au Rais Uhuru Kenyatta. haya ni baadhi ya mambo sita ambayo jicho pevu la SAUTI KUU inadhani Raila anapaswa kufanya ili afanikishe ndoto ya kuingia Ikulu:

1. Aache kuishambulia IEBC


Naomba nisieleweke vibaya katika hili, tume huru ya uchaguzi nchini (IEBC) kama jina lake linavyoelevya ni tume 'huru' na kwa maoni yangu ni huru kuliko ile ya Marehemu Kivuitu (ICK). Najua wengi wenu mnaweza msikubaliane nami kuhusu hili lakini ifike mahali ieleweke kuwa, IEBC ni Taasisi ambayo wajumbe wake wanachaguliwa kwa kuzingatia sifa zao (Vetted) na sio wa kuteuliwa na mtu mmoja kama wengi wanavyofikiria.

Hivyo basi kwa kuzingatia ukweli huo, IEBC ndiyo msimamizi sahihi wa uchaguzi huru na haki. kama mnakumbuka ni IEBC hii ambayo sasa hivi wapinzani wanaiona haifai ndiyo iliyoendesha na kusimamia uchaguzi wa wabunge na maseneta wakiwemo wabunge na maseneta kutoka mrengo wa upinzani na kwa tafsiri nyepesi unapoishambulia IEBC, unajaribu kusema kuwa hata wabunge wako na maseneta hawako ofisini kihalali.

Kuendelea kuishambulia IEBC, kunaweza kumshushia sifa na hadhi Raila ambayo ametumia muda mrefu kuijenga. pia binafsi ni kupoteza muda wakati kuna mambo mengi ya kufanya.

2. Ajue kucheza vizuri na namba

Raila anapaswa kuhakikisha kama sio kujaribu kugawa kura za kanda ya Bonde la Ufa (Rift Valley) huku akiendelea kutunza kura za Nyanza, Magharibi (Western) na (Pwani (Coast), vinginevyo kutokana na tamaduni ya siasa za Kenya ambayo mara nyingi huzingatia mahesabu ya namba, ajiandae kushindwa tena.

Itakumbukwa kuwa, Rais mstaafu Daniel Arap, alifanikiwa kuitawala Kenya kwa miaka 24, kutokana na sapoti kubwa ya bonde la Ufa (wingi wa kura kutoka Rift Valley). Ili kupata kura za Rift Valley, Raila anahitaji kumpata Ruto au Rutto au amuibue kingunge mwengine kutoka Rift Valley, japo nadhani kwa sasa zikiwa zimesalia miezi 18 tu, ni ngumu sana.

3. Ahamasishe wapiga kura wake wajiandikishe kwa wingi

Namba hubadilika na msukumo wa kuchagua nayo hubadilaka, lakini ni ukweli usiopingika kuwa utamaduni wa Wakenya ni kuchaguana kwa misingi ya Kikabila na Ukanda. Hivyo basi, Raila anapaswa kulizingatia hili na kuhakikisha Ngome zake zinakuwa imara kwa kuwashawishi wapiga kura wake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.

Katika shughuli ya Harambee, Shilingi milioni moja hupatikana pale watu milioni moja wanapoamua kuchangia kila mmoja shilingi moja. katika uchaguzi hali huwa hivyo. ili upate kura milioni moja au sita au 12, ni lazima uwe na wapiga kura milioni moja, milioni sita au milioni 12. Raila popote ulipo, anza mapema kukusanya watu kabla hujachelewa.


4. Atumie Mitandao ya kijamii (Social Media) kujitangaza

Unaweza ukachukulia kirahisi lakini nguvu ya mitandao ya kijamii ni kubwa sana na muhimu sana kwa Mwanasiasa yoyote yule. Raila hawezi kulikwepa hili, ukiangalia idadi ya wafuasi wa Uhuru na Raila katika mitandao ya Twitter na Facebook, utagundua Uhuru ana wafuasi wengi sana kuliko Raila.

Wakenya wengi  wanatumia mitandao ya kijamii na Kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2017 utaegemea ushiriki wa mgombea kwenye majukwaa ya mitandao hii hasa katika kuzipata kura za vijana. 

Wanasiasa ni lazima kuelewa kuwa wapiga kura wengi ni viabarua ambao huwa wanafanya kazi kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi, jumapili wanaenda ibadani (hawana mapumziko). Hivyo ni rahisi kuwapata kupitia mitandao ya jamii.

5. Raila anapaswa kupunguza Safari za nje za mara kwa mara

Raila huu ni muda wa kupunguza au kufuta kabisa safari za nje zisizokuwa za lazima. sio vibaya kusafiri au kuwa na marafiki nje ya nchini, lakini nadhani kuelekea uchaguzi mkuu ujao, ni vyema kuwa na marafiki wa ndani, kwa maana ya wakenya wa kawaida (wapiga kura). kura zinapigwa na Wakenya na sio hao marafiki walioko nje ya mipaka ya Taifa letu.
Raila Odinga alipomtembelea Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli nyumbani kwake, Chato, Tanzania hivi karibuni
6. Awahimize Wapiga kura wake kujitokeza kupiga kura.
Mwisho, Raila anapaswa kuwafunda mashabiki wake kuachana na kasumba ya kupiga kura za ndotoni (wawe wapiga wa vitendo) kwa kujitokeza katika vituo vya kupigia kura na sio kupiga porojo tu vitendo hakuna.

#Roadto2017 #Generalelection2017

MCHAKATO WA KUMPATA MRITHI WA BAN KI-MOON WAANZA

MCHAKATO WA KUMPATA MRITHI WA BAN KI-MOON WAANZA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Kwa mara ya kwanza Umoja wa Mataifa umeweka wazi mchakato wa kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa baada ya kutoa nafasi kwa mataifa yote kuwauliza maswali wagombea waliojitokeza kuwania nafasi hiyo. 

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Hatua hii inaonekana kuvunja sasa mazingira ya siri yaliyokuwepo hapo kabla katika mchakato wa kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ikiwa ni miaka 70 tangu kuanzishwa kwa umoja huo.

Wagombea watatu miongoni mwa tisa waliojitokeza kuwania nafasi hiyo walipata nafasi ya kuulizwa maswali na kuelezea mipango yao ya baadaye katika utendaji wao iwapo watafanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kumalizika muda wa uongozi wa Katibu Mkuu wa sasa Ban Ki-moon hapo January 1, mwakani.

Kwa miongo kadhaa sasa mchakato wa uchaguzi wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanyika katika mazingira ya siri chini ya usimamizi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloundwa na wajumbe kutoka nchi wanachama wa baraza hilo ambazo ni pamoja na Uingereza, Ufaransa, China, Urusi na Marekani.
Katibu Mkuu wa sasa wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon


Hata hivyo, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana lilipiga kura kubadilisha utaratibu huo na kuwataka wagombea wa nafasi hiyo kuwasilisha barua za maombi, kutoa muhtasari wa malengo yao pamoja na kuwa tayari kujieleza na kuulizwa maswali.

Uamuzi wa mwisho wa uteuzi wa nafasi hiyo bado unabakia katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini hatua hiyo ya kuweka uwazi katika mchakato huo utaweka msukumo kwa mataifa hayo yenye nguvu kuteua jina la mtu ambaye atakuwa anakubalika kwa kiwango kikubwa.

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mogens Lykketoft alisikika akisema kuwa haya ni mabadiliko muhimu. " Iwapo kutakuwa na idadi kubwa ya nchi zinazomuunga mkono mgombea mmoja sidhani kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuja na jina tofauti na hilo " alisema.

Waziri wa Mambo ya nje wa Montenegro Igor Luksic mwenye umri wa miaka 39 ambaye ni mgombea kijana kuliko wote waliojitokeza kuwania nafasi hiyo alikuwa wa kwanza kujieleza mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akielezea jinsi atakavyotumia uzoefu wake wa nafasi alizowahi kushika katika nchi yake ikiwemo uwaziri mkuu katika kuwania nafasi hiyo.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi, Elimu na Utamaduni-UNESCO Irina Bokova pamoja na mtendaji mkuu wazamani wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia masuala ya wakimbizi ambaye pia amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Ureno Antonio Guterres ni miongoni mwa waliopata nafasi ya kujieleza mbele ya baraza hilo.
Kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huchaguliwa na wajumbe kutoka nchi wanachama 193 wa umoja huo kutokana na mapendekezo yaliyowasilishwa na wajumbe kutoka nchi wanachama 15 zinazounda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

LOWASSA ACHANGIAWA FEDHA ZA KUCHUKUA FOMU NA WANA CCM MKOA WA TABORA

LOWASSA ACHANGIAWA FEDHA ZA KUCHUKUA FOMU NA WANA CCM MKOA WA TABORA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mzee wa CCM wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Yusuf Bundala Kasubi, (kulia),  akimkabidhi Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa,  zaidi ya shilingi milioni  moja, zilizochangwa na wanachama wa CCM mkoani Tabora, ili kumuwezesha mtangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ili azitumia kulipia ada ya kuchukua fomu za kuwani urais kupitia chama hicho. Hafla ya kukabidhi fedha hizo ilifanyika nyumbani kwa Mtangaza nia huyo, mjini Dodoma JAlhamisi Juni 4, 2015. Badaaye jioni Lowassa anatarajiwa kuchukua fomu hizo, makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, ambaye tayari ametangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, Edward Lowassa, akisalimiana na ujumbe wa wana CCM kutoka mkoani Tabora, walipofika nyumbani kwake mjini Dodoma leo Alhamisi Juni 4, 2015, ili kumpatia mchango wao wa nkumuwezesha kulipia ada ya fomu ya kuwani urais.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, ambaye tayari ametangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, Edward Lowassa, akisalimiana na ujumbe wa wana CCM kutoka mkoani Tabora, walipofika nyumbani kwake mjini Dodoma leo Alhamisi Juni 4, 2015, ili kumpatia mchango wao wa nkumuwezesha kulipia ada ya fomu ya kuwani urais.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, ambaye tayari ametangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, Edward Lowassa, akiwashukuru wana CCM kutoka mkoani Tabora, baada ya kumkabidhi mchangio wa zaidi ya shilingi milioni 1 ili azitumia kulipia ada ya kuchukua fomu za kuwania urais katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake mjini Dodoma, leo Alhamisi Juni 4, 2015.
Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Majaliwa Bilali, (kulia), akizungumza sababu zilizowapelekea wana CCM mkoani humo kuchanga fedha za kumuwezesha Mtangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, (kushoto), wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mchango huo wa shilin gi milioni 1 zilizofanyika nyumbani kwa mtangaza nia huyo, mjini Dodoma, Alhamisi Juni 4, 2015. Badaaye jioni Lowassa anatarajiwa kuchukua fomu hizo, makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA UKUMBI WA CHAKULA ULIOFADHILIWA NA TANAPA

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA UKUMBI WA CHAKULA ULIOFADHILIWA NA TANAPA

Posted in ,
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Rombo mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari Olele iliyopo kata ya Olele kwa ajili ya kukabidhi Mradi wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa , Tanzania (TANAPA).
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakifurahia nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanafunzi wa shule ya  sekondari ya Olele wakati alipofika kwa ajili ya uzinduizi na makabidhiano rasmi ya ukumbi wa chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
RC ,Gamana iongozi wengine wakiskiliza nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na kwaya ya shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Kutokana na hali ya mvua iliyokuwepo wakati wa makabidhiano ya ukumbi wa chakula,mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama alilazimika kubadili meza kuu na wao wakaa eneo ambalo pia lilikuwa na mvua huku akisema ni vyema mvua ikawanyeshea wote pamoja na wananchi.
Jengo la Ukumbi wa Chakula lililojengwa kwa ufadhili wa Shirika la  Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Meneja Ujirani Mwema kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ahmed Mbugi akitoa taarifa kuhusiana na ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari Olele.
Baadhi ya wananchi katika kata ya Olele. 
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania,TANAPA,Ibrahim Musa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mradi wa ujirani mwema wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
RC,Gama na DC,Kipuyo wakilowa kutokana na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Wanafunzi katika shule ya sekondari Olele wakifuatilia hotuba ya viongozi waliofika shuleni hapo kwa ajili ya makabidhiano ya ukumbi wa chakula uliojengwa na TANAPA.
Mkuu wa wilaya ya Rombo ,Lembris Kipuyo akizungumza katika hafla hiyo.
Wakazi wa kata ya Olele.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akihutubia wananchi waliofika katika hafla fupi ya makabidhiano ya ukumbi wa chakula uliojengwa katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro ,Leonidas Gama akikagua jengo hilo.
Na Dixon Busagaga wa Globu aya Jamii Kanda ya Kaskazini.

NASSARI ASHIRIKI UJENZI WA CHANZO CHA MAJI KIJIJI CHA KARANGAI KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

NASSARI ASHIRIKI UJENZI WA CHANZO CHA MAJI KIJIJI CHA KARANGAI KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

Posted in ,
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar aiwa amepanda kwenye Lori lililokuwalikibeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji kwa ajili ya kumwagilia katika kijiji cha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akishirikiana na wananchi katika kijiji cha Karangai kuweka mawe katika chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Mbunge Nassar akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo hilo.
Mbunge Joshua Nassar akizungumza na mmoja a wanakiji cha Karangai huku akiwa amembea mtoto muda mfupi baada ya kumaliza hatua za awali za uwekaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Mbunge Joshua Nassar akizungumza na baadhi ya kina mama ambao mingoni mwao wanajishughulisha na shughuli za kilimo alipotembelea kijiji cha Karangai kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya umagiliaji katika kijiji hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

Mheshimiwa Sitta ajiweka mbali na lawama za wivu wa uwaziri mkuu!

Mheshimiwa Sitta ajiweka mbali na lawama za wivu wa uwaziri mkuu!

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mh Samuel Sitta akitangaza nia leo mchana Itetemia Tabora
Mheshimiwa Samuel Sitta leo hii alitangaza rasmi nia yake kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Alitangaza nia yake hiyo mbele ya mamia ya wakazi wa kata ya Itetemia, Tabora mjini na wilaya za jirani na mji wa Tabora.

Akieleza sababu tano zilizomfanya atangaze nia yake ambazo ni 

Mambango nayo yalikuwepo!

Mh Sitta akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Tabora leo mchana.
Mh Magreth Sitta akisalimia wananchi wa Itetemia

1.Muungano
Toka pande zetu mbili za muungano zinatolewa kauli na pia vitendo vyenye kuashiria nchi zetu zilizomo katika muungano yaani Tanganyika na Zanzibar zitengane. Kutoka Zanzibar, tunashuhudia wanasiasa wanaodai kuwa Zanzibar itanufaika zaidi ikiwa nje ya muungano na kuwa na uhuru kamili kama nchi. Na kutoka bara tunasikia.

2. Mchakato wa katiba
Pamoja na kuwa na muafaka kamili kuhusu katiba mpya haujapatikana, lakini katiba inayopendekezwa ina maeneo mengi ya msingi ambayo yanaweza kutuleta karibu ikiwa ni hatua ya awali inayotuwezesha kusonga mbele kwa amani.



Mama Magreth Sitta akiwa na Mwenekiti wa UWT Mkoa wa Tabora Mama Mchemba.
Mtemi wa Unyanyembe Mtemi Msagata Fundikira, Mh Samuel Sitta na mwenekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini
Binafsi naamini kuwa pande zinazosigana kuhusu katiba zina wazalendo ambao wanaweza kukubaliana kuwa na kipindi cha mpito cha utulivu na maelewano kitakachotuwezesha kama taifa kusonga mbele. Viongozi a kijamii na ki saisa washawishiwe kukubali hoja mbili.

3.Mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwanda Ili kukuza uchumi wa nchi kwa kasi inayopunguza umasiikini kwa haraka na huku tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya aserikali kutosheleza  huduma za ubora wa huduma za jamii kama vile afya , elimu na maji,hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa uendeshaji uwe ni wa motisha kwa wazalisha mali. Mifumo ya nchi zilizopiga hatua za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira  chanya ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii haijatimia hapa kwetu.




4.Mikakati ya dhati ya kupambana na rushwa
Rushwa kubwa zimekuwa na athari mbaya sana kwa uchumi wa nchi yetu. Mikataba mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na hata rushwa katika ajira, vimesababisha hasara ya matrilioni ya shilingi kwa taifa. Uchumi unakosa afya kutokana na kubanwa na rushwa ambayo sasa imeenea mpaka vijijini.

5. Kuimarisha CCM kiuchumi
Chama tawala madhubuti ni nyenzo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zote kwa ufanisi zilizoahidiwa kwenye ilani. Katika hili ni wajibu wa mwenyekiti wa chama kuhakikisha kwamba vitengo na vitega uchumi vya chama vinakuwa na tija inayokiwezesha chama kuendesha shughuli zake  kwa kujitegemea badala ya kutegemea ruzuku toka serikalini. Chama tawala kinachojitegemea ki uchumi ni kinga dhidi ya rushwa kwa sababu itazuia mazoea yaliyopo ya wafanyabiashara wasio waaminifu kujijenga kwa mwanya wa kuwa ni "wafadhili" 


Mh Magreth Sitta akifuatiwa na Mussa Ntimizi mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui



Magreth Sitta Kijo akiwa na mumewe Kefa Kijoh Itetemia leo



Aidha Mh Sitta akijibu swali toka kwa mwandishi wa habari aliyeuliza "Mh Sitta unasemaje juu ya shutuma za waziri mkuu aliyejiuzuru wadhfa wake kuwa wewe na Mh Mwakyembe mlikuwa na wivu naye ndio maana mkamuonea mpaka ikabidi ajiuzuru? Mh Sitta akajibu "Bwana mwandishi kwa nini swali hilo humuulizi yeye mwenyewe aseme ni kipi alichoonewa? Mchakato wa uchunguzi ulifanyika mwaka 2008 mpaka sasa ni miaka 7 hivi sasa muda wote huu alikuwa wapi hata leo aseme alionewa? Jibu ambalo lilipelekea vicheko na vigerere toka kwa wananchi walioudhuria hafla hiyo. 

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .