RAILA AKIFANYA HAYA ATASHINDA URAIS, UCHAGUZI MKUU 2017.
Posted in
afrika mashariki
,
Siasa
No comments
Sunday, April 17, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
KENYA inajiandaa kuingia katika uchaguzi mkuu mwaka 2017, ambayo inatarajiwa kufanyika mapema mwezi Agosti ambapo mchukuano mkali unatarajiwa kuwa kati ya muungano wa Jubilee ya Rais Uhuru Kenyatta na muungano wa CORD inayoongozwa na Raila Odinga.
Kwa muda mrefu sasa, Raila Amollo Odinga, amekuwa akitoa upinzani mkubwa kwa chama tawala, lakini kwa bahati mbaya, mara zote amejikuta akishindwa kutimiza ndoto yake ya kuingia Ikulu.
Ndani ya CORD, kuna mvutano mkubwa wa nani anastahili kupeperusha bendera ya muungano huo dhidi ya muungano wa Jubilee unaoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, itakapotimu Agosti mwakani.
Raila wa Orange Democratic Party ambaye mwaka 2013 alishindwa na Uhuru Kenyatta tayari ameonesha nia ya kukiuka makubaliano (MOU) ya muungano wa CORD ambayo inadaiwa ilieleza wazi kuwa endapo Raila angeshinda (2013), angehudumu kwa kipindi kimoja na kumpa pasi Kalonzo Musyoka wa Wiper.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, uchaguzi wa mwaka ujao, ni Kalonzo ndiye anayestahili kupeperusha bendera ya CORD, lakini wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa Ford Kenya, ambayo ni chama tanzu ndani ya muungano wa CORD, naye ametangaza nia ya kukaa meza kuu.
Hizo zinaitwa 'Sihasa' za Siasa. ikiwa ni mwaka wake wa mwisho (umri umemtupa mkono) kugombea nafasi hiyo nyeti katika uongozi wa taifa hili, Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga anapaswa mambo kadhaa endapo anamatumaini ya kumrithi Uhuru Muigai Kenyatta.
Kama nilivyosema hapo awali uchaguzi mkuu ujao, utakuwa wa mwisho kwa Raila katika juhudi zake za kuingia Ikulu. Haitakuwa kazi rahisi, itakuwa ni kazi ngumu kuliko uchaguzi uliopita.
Rais Uhuru Kenyatta kwa sasa ana umaarufu mara mbili ya alivyokuwa mwaka 2013 na ana 'advantage' nyingine ambayo ni uwepo wake madarakani. Anaingia katika Uchaguzi ujao akiwa na uzoefu wa kazi (urais) wa miaka mitano, hii inampa kiburi cha kushinda zaidi ya alivyokuwa wakati anatafuta njia ya kuelekea Ikulu.
Wakati Uhuru akiwa na uzoefu wa miaka mitano kama Rais, Raila yeye ana uzoefu wa miaka mitano kama Waziri Mkuu hivyo kwa mtazamo wa haraka haraka, mafahali hawa wawili wana sifa sawa. hapa ndipo sasa Wakenya watakapohitaji kitu kingine cha ziada cha kuwashawishi kumpigia Raila kura na sio Uhuru.
Mbali na uzoefu alionao, kitu kingine kinachomfanya Uhuru awe na kiburi, ni sapoti aliyonayo kutoka ndani ya Muungano wa Jubilee huku pia kukiwa na hali ya utulivu tofauti na Raila ambaye mpaka sasa bado hana uhakika wa asilimia 100 ya sapoti ya Muungano wa CORD, kwani wote watatu wanataka (Raila, Kalonzo na Wetangula).
Ningekuwa Raila, huu ndio ungekuwa muda wa kufanya kazi kwa juhudi zangu zote kuwashawishi Wakenya ni kwanini nafaa kuwa Rais na sio Wetangula, Kalonzo au Rais Uhuru Kenyatta. haya ni baadhi ya mambo sita ambayo jicho pevu la SAUTI KUU inadhani Raila anapaswa kufanya ili afanikishe ndoto ya kuingia Ikulu:
1. Aache kuishambulia IEBC
Naomba nisieleweke vibaya katika hili, tume huru ya uchaguzi nchini (IEBC) kama jina lake linavyoelevya ni tume 'huru' na kwa maoni yangu ni huru kuliko ile ya Marehemu Kivuitu (ICK). Najua wengi wenu mnaweza msikubaliane nami kuhusu hili lakini ifike mahali ieleweke kuwa, IEBC ni Taasisi ambayo wajumbe wake wanachaguliwa kwa kuzingatia sifa zao (Vetted) na sio wa kuteuliwa na mtu mmoja kama wengi wanavyofikiria.
Hivyo basi kwa kuzingatia ukweli huo, IEBC ndiyo msimamizi sahihi wa uchaguzi huru na haki. kama mnakumbuka ni IEBC hii ambayo sasa hivi wapinzani wanaiona haifai ndiyo iliyoendesha na kusimamia uchaguzi wa wabunge na maseneta wakiwemo wabunge na maseneta kutoka mrengo wa upinzani na kwa tafsiri nyepesi unapoishambulia IEBC, unajaribu kusema kuwa hata wabunge wako na maseneta hawako ofisini kihalali.
Kuendelea kuishambulia IEBC, kunaweza kumshushia sifa na hadhi Raila ambayo ametumia muda mrefu kuijenga. pia binafsi ni kupoteza muda wakati kuna mambo mengi ya kufanya.
2. Ajue kucheza vizuri na namba
Raila anapaswa kuhakikisha kama sio kujaribu kugawa kura za kanda ya Bonde la Ufa (Rift Valley) huku akiendelea kutunza kura za Nyanza, Magharibi (Western) na (Pwani (Coast), vinginevyo kutokana na tamaduni ya siasa za Kenya ambayo mara nyingi huzingatia mahesabu ya namba, ajiandae kushindwa tena.
Itakumbukwa kuwa, Rais mstaafu Daniel Arap, alifanikiwa kuitawala Kenya kwa miaka 24, kutokana na sapoti kubwa ya bonde la Ufa (wingi wa kura kutoka Rift Valley). Ili kupata kura za Rift Valley, Raila anahitaji kumpata Ruto au Rutto au amuibue kingunge mwengine kutoka Rift Valley, japo nadhani kwa sasa zikiwa zimesalia miezi 18 tu, ni ngumu sana.
3. Ahamasishe wapiga kura wake wajiandikishe kwa wingi
Namba hubadilika na msukumo wa kuchagua nayo hubadilaka, lakini ni ukweli usiopingika kuwa utamaduni wa Wakenya ni kuchaguana kwa misingi ya Kikabila na Ukanda. Hivyo basi, Raila anapaswa kulizingatia hili na kuhakikisha Ngome zake zinakuwa imara kwa kuwashawishi wapiga kura wake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.
Katika shughuli ya Harambee, Shilingi milioni moja hupatikana pale watu milioni moja wanapoamua kuchangia kila mmoja shilingi moja. katika uchaguzi hali huwa hivyo. ili upate kura milioni moja au sita au 12, ni lazima uwe na wapiga kura milioni moja, milioni sita au milioni 12. Raila popote ulipo, anza mapema kukusanya watu kabla hujachelewa.
4. Atumie Mitandao ya kijamii (Social Media) kujitangaza
Unaweza ukachukulia kirahisi lakini nguvu ya mitandao ya kijamii ni kubwa sana na muhimu sana kwa Mwanasiasa yoyote yule. Raila hawezi kulikwepa hili, ukiangalia idadi ya wafuasi wa Uhuru na Raila katika mitandao ya Twitter na Facebook, utagundua Uhuru ana wafuasi wengi sana kuliko Raila.
Wakenya wengi wanatumia mitandao ya kijamii na Kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2017 utaegemea ushiriki wa mgombea kwenye majukwaa ya mitandao hii hasa katika kuzipata kura za vijana.
Wanasiasa ni lazima kuelewa kuwa wapiga kura wengi ni viabarua ambao huwa wanafanya kazi kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi, jumapili wanaenda ibadani (hawana mapumziko). Hivyo ni rahisi kuwapata kupitia mitandao ya jamii.
5. Raila anapaswa kupunguza Safari za nje za mara kwa mara
Raila huu ni muda wa kupunguza au kufuta kabisa safari za nje zisizokuwa za lazima. sio vibaya kusafiri au kuwa na marafiki nje ya nchini, lakini nadhani kuelekea uchaguzi mkuu ujao, ni vyema kuwa na marafiki wa ndani, kwa maana ya wakenya wa kawaida (wapiga kura). kura zinapigwa na Wakenya na sio hao marafiki walioko nje ya mipaka ya Taifa letu.
6. Awahimize Wapiga kura wake kujitokeza kupiga kura.

Raila Odinga alipomtembelea Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli nyumbani kwake, Chato, Tanzania hivi karibuni |
Mwisho, Raila anapaswa kuwafunda mashabiki wake kuachana na kasumba ya kupiga kura za ndotoni (wawe wapiga wa vitendo) kwa kujitokeza katika vituo vya kupigia kura na sio kupiga porojo tu vitendo hakuna.
#Roadto2017 #Generalelection2017
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :