TANZANIA: RC DAR ES SALAAM, SAID MECK SADIKI AZINDUA DUKA LA HUAWEI JIJINI DAR ES SALAAM
                      Posted in 
                      
afrika mashariki
                            , 
                          
Biashara
                            No comments
                          
Monday, February 29, 2016
                      By 
                      danielmjema.blogspot.com
 Mkuu 
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria 
uzinduzi wa  duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu , 
Samora jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania.
 Mkurugenzi
 wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akizungumza na wandishi 
wa habari hawapo pichani juu duka la kuwapatia wananchi bidhaa zenye 
viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda 
sambasamba na mabadiliko ya teknolojia hivyo kuwapatia wateja wao simu 
za mkononi za kisasa,jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu,
Kampuni
 ya simu kutoka nchini China ya Huawei, imezidi kutanua wigo wa huduma 
kwa kuzindua maduka mawili ya simu moja likiwa jengo la JMall na duka la
 pili lenye Kituo cha huduma ya matengenezo ya simu za mkononi likiwa 
jengo la NHC karibu na TTCL mtaa wa Samora..
 Hii ikiwa ni baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei jijini
 Dar es Salaam na pia kuhakikisha kuwa vifaa vya uhakika na orijino 
vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.kwa ukaribu zaidi jijini la Dar es Salaam.
Maduka hayo ya Huawei yana mahali husika panapo ruhusu wateja wake kuangalia na kujaribu simu na vifaa vingine vya Huawei. Maduka
 hayo pia yanatoa nafasi nzuri kwa wateja kupata huduma bora na kuzoea 
bidhaa za Huawei na hata kwa kujaribu baadhi ya vifaa vyetu vya mtandao 
vyenye uwezo wa 3G/4G LTE Smartphone.
Maisha
 ya wateja wetu yana badilika kila siku na matarajio yao ni kuona ubora 
na ukuaji wa huduma katika kiwago cha juu zaidi. Kama wadau wakubwa 
Huawei imekuwa ikijitahidi katika kukidhi mahitaji ya kila siku ya 
wateja na pia kuahidi kuwaonyesha wateja thamani ya pesa yao. 
“Dar
 es salaam kama kitovu katika ukuaji wa uchumi, tunaamini maduka yetu ya
 simu na pia kituo cha matengenezo ya simu za mkononi yataongeza ufanisi
 na kusaidia ufikiaji wa huduma za mawasiliano kwa ukaribu Zaidi. Maduka
 yetu yamejikita katika ubora wa kutoa bidhaa kwa wateja wa rejareja na 
kuwapa wauzaji uwezo wa kupata vifaa halisi, bora na pekee”.
Maduka mapya ya Huawei, mbali na uuzaji wa Simu za mkonon , Pia  yatatoa huduma baada ya mauzo wataalam wa mauzo wataweza watatoa msaada wa  kifundi na utumiaji na matengenezo
Katika
 kusherekea ufunguzi huu wa maduka ya Huawei na kituo cha huduma za 
simu, Huawei inatoa punguzo la bei kuanzia tarehe 25 mpka tarehe 29 
mwezi huu ikiwa pamoja na promosheni za simu zao P8 na G8. Manunuzi ya 
simu hizi mbili za P8 na G8 yataambatana na zawadi kama selfie stiki, 
spika za Bluetooth na tisheti.
Huawei
 Tanzania imejipanga kuhakikisha ina weza kuwafikia wateja wake wote 
Tanzania kote katika ubora na huduma zenye ufanisi Zaidi.
Maduka
 yetu yatakuwa yanatoa huduma itakayo fanya manunuzi yako yawe ya 
kihistoria, pia tupo kwenye msimu wa kuhakikisha uwepo wetu unajulikana 
Tanzania kwa ujumla kwa kuanza na Dar es salaam” aliongeza meneja wa Huawei nchini.
 Maduka hayo yatatoa huduma siku zote za wiki saa 2 asubuhi hadi saa 
kumi na moja jioni jumatatu hadi Ijumaa na jumamosi yatakuwa wazi 
kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa saba mchana. Maduka
 ya Huawei yatakuwa kwa ajili ya kuboresha utumiaji sahihi wa  
teknolojia  katika njia sahihi zaidi, Wateja Wote mnakaribishwa 
Kuhusu Huawei
Huawei
 ni vinara wa teknolojia na mawasiliano hususani katika kutimiza matakwa
 ya wateja wao, katika kuhakikisha wanawapa wateja wao kile kilicho bora
 katika viwango vya juu, umuhimu wa mawasiliano na vifaa vya mawasiliano
 vinatumika katika nnchi Zaidi ya 170 na mikoa yake, Huawei ilishika 
nafasi ya 228 ulimwenguni kwa mwaka kutokana na mapato yake mwaka 2014 
kati ya makampuni 500.
Mapato ya kampuni yamefikia kiasi cha dolla za 
kimarekani bilioni 46.5. Huawei imeshika nafasi ya 3 kwenye usambazaji 
wa simu kwa mwaka 2015 kwa kusambaza zaidi ya simu milioni 100 duniani 
kote, Kampuni ya Huawei ipo katika kuhakikisha inatoa ushirikiano katika
 kukuza na kuboresha vifaa vya mawasiliano  duniani kote.
Kampuni
 ya Huawei inajihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za 
intaneti kwa njia ya modemu na vifaa vya matumizi ya nyumbani. Huawei
 imeimarisha mahusiania ya biashara na makampuni kama Tigo, Vodacom, 
Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, 
CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, 
NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom.
Hotuba ya Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Peter Philip
Uongozi wa Huawei
Wadau mbalimbali wa Huawei
Waandishi wa Habari
Mabibi na Mabwana
------------------------------ ------------------------------ ------------------------------ ------------
Nina
 furaha kubwa kuwa miongoni mwenu leo pamoja na timu nzima ya Huawei. 
Katika dunia ambayo teknolojia ya mawasiliano inabadilika kwa kasi 
kushiriki  katika mabadiliko hayo ya maendeleo ni upendeleo mkubwa.
Mabibi
 na Mabwana, Christine Qiang mwana Uchumi wa Benki ya Dunia alisema” 
Wigo wa simu za mkononi unakuwa kwa kasi, ukiwa ni njia moja kuu ya 
kutanua fursa za kiuchumi na huduma za msingi kwa mamilioni ya watu” 
Kuunganishwa kupitia Intaneti au simu za mkononi kunaleta taarifa za 
masoko, huduma za kifedha na huduma za kiafya sehemu za mbali 
zisizofikika kiurahisi na ina saidia kubadilisha maisha ya watu kwa 
namna za kipekee.
Mabibi
 na Mabwana Ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza Huawei Tanzania 
kwa hatua hii nzuri katika kuendeleza sekta ya mawasiliano na teknolojia
 nchini Tanzania.
Sekta
 ya mawasiliano na teknolojia nchini Tanzania inakua kwa kasi na kuwa 
moja ya nguzo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Maendeleo 
haya ya kasi katika mawasiliano na teknolojia yamepelekea wawekezaji 
Wengi kuwekeza katika sekta hii nchini kwetu. Kwa sasa sekta hii inakua 
kwa kasi ya asilimia kumi na tano na asilimia ishirini kwa mwaka, 
kiwango ambacho kinaonyesha kua cha juu katika ukanda wa afrika 
mashariki.
Nchi
 Zaidi ya thelathini duniani hutengeneza simu za mkononi, hata hivyo 
ubora umekua alama ya utofautishaji katika makampuni haya ya simu. 
Kampuni ya Huawei imethibitisha mara kwa mara uwezo wao katika 
kuridhisha wateja wao kwa kuwapatia bidhaa zenye viwango vya uhakika, 
huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda sambasamba na 
mabadiliko ya teknolojia ivyo kuwapatia wateja wao simu za mkononi za 
kisasa.
Mabibi na Mabwana
Duka
 hili jipya na huduma matengenezo ya simu za mkononi la Huawei 
haliashirii ongezeko katika utajiri au mauzo yao ila inaashiria kutambua
 mahitaji ya wateja wao na fursa ya kupata bidhaa zenye uhakika na 
zilizo bora.
Nina
 Imani kuwa Huawei itaendelea kuwatosheleza wateja wake. Nchi ya 
Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi katika sekta ya teknolojia ivyo 
natumai na naamini Huawei watatumia fursa hiyo kuongoza soko la simu za 
mkononi nchini Tanzania.
Mabibi
 na Mabwana, Kwa mara nyingine nishukuru sana Uongozi mzima na 
menejimenti ya Huawei kwa kunishirikisha katika tukio hili tunapo fungua
 rasmi duka la Huawei na huduma za simu hapa J Mall.
Nina uhakika kila mteja atakae pita katika malango haya ya Huawei atapata kumbukumbu njema na mguso wa teknolojia ya uhakika.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :