BURUNDI: KABURI LA ALAIKI LAGUNDULIKA MUTAKURA KASKAZINI MWA BUNJUMBURA
Posted in
afrika mashariki
No comments
Monday, February 29, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Maafisa wa polisi na utawala wa mji
mkuu wa Bujumbura Burundi wamegundua kaburi la halaiki linaloshukiwa
kuwa na takriban miili 30. Mwandishi wa BBC aliyeko huko Prime
Ndikumagenge anasema kuwa miili 3 na fuvu la kichwa ilipatikana katika
eneo la Mutakura Kaskazini mwa Bujumbura.
Kitongoji hicho cha
Mutakura ni moja ya ile iliyosheheni wafuasi wa upinzani ambao
walijitokeza barabarani wakiandamana kupinga kauli ya rais Pierre
Nkurunziza kuwania muhula wa tatu uongozini. Nkurunziza alitangaza
nia ya kuwania muhula wa tatu mwezi Aprili mwaka uliopita kinyume cha
katiba akidai kuwa mhula wa kwanza hakuchaguliwa na umma.
Wapinzani wake hata hivyo wanadai kuwa alikiuka katiba ya taifa. Meya wa mji wa Bujumbura Freddy Mbonimpa anasema walipokea habari hiyo kutoka kwa ''wahuni waliojisalimisha kwa utawala''.
Haikuelezwa kwa hakika waliuawa lini au na nani na nani aliyewazika pahala hapo. Meya huyo hata hivyo alidai kuwa waliopatikana wameuawa walikuwa ni wafuasi wa rais Nkurunziza.
Kuwepo kwa makaburi ya halaiki kuligunduliwa kwanza na kundi
linalopigania haki za kibinadamu la Amnesty International mwezi
Januari. Ripoti hiyo ya kundi la kutetea haki za binadamu la
lilichapishwa tarehe 11 Desemba mwaka uliopita siku moja baada ya
serikali kukiri kuwa wamewaua watu 79 na kupoteza maafisa 8 wa polisi.
Meya huyo leo amekiri kuwa utawala wake ulizika miili ya watu 58 katika makaburi ya halaiki katika makaburi yanayofahamika. Umoja
wa Mataifa unasisitiza kuwa zaidi ya watu 430 waliuawa nchini Burundi
tangu kauli ya rais Nkurunziza kubainika mwezi Aprili.
SOURCE: BBC SWAHILI
SOURCE: BBC SWAHILI
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :